37-Kitaab At-Tawhiyd: Miongoni Mwa Shirki Kutenda ‘Amali Njema Kwa Ajili Ya Manufaa Ya Kidunia

Mlango Wa 37

بَابٌ مِنَ الشِّرْكِ إِرَادَةُ الْإِنْسَانِ بِعَمَلِهِ الدُّنْيَا

Miongoni Mwa Shirki Kutenda ‘Amali Njema Kwa Ajili Ya Manufaa Ya Kidunia


 

وَقَوْلُهُ تَعَالَى:

Na kauli Yake Ta’aalaa:

مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لَا يُبْخَسُونَ ﴿١٥﴾

((Anayetaka uhai wa dunia na mapambo yake Tutawalipa kikamilifu ‘amali zao humo, nao hawatopunjwa humo)) 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ إِلَّا النَّارُ ۖ وَحَبِطَ مَا صَنَعُوا فِيهَا وَبَاطِلٌ مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٦﴾

((Hao ndio wale ambao hawatokuwa na chochote katika Aakhirah isipokuwa moto. Na yataporomoka yale waliyoyafanya humo (duniani), na ni yenye kubatilika yale waliyokuwa wakiyatenda)) [Huwd (10: 15-16)]

 

وفِي الصَّحِيحِ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((تَعِسَ عَبْدُ الدِّينَارِ، تَعِسَ عَبْدُ الدِّرْهَمِ، تَعِسَ عَبْدُ الْخَمِيصَةِ، تَعِسَ عَبْدُ الْخَمِيلَةِ، إِنْ أُعْطِيَ رَضِي، وَإِنْ لَمْ يُعْطَ سَخِطَ، تَعِسَ وَانْتَكَسَ، وَإِذَا شِيكَ فَلا اِنْتَقَشَ، طُوبَى لِعَبْدٍ آخِذٍ بِعِنَانِ فَرَسِهِ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، أَشْعَثَ رَأْسُهُ، مُغْبَرَّةٍ قَدَمَاهُ، إِنْ كَانَ فِي الْحِرَاسَةِ كَانَ فِي الْحِرَاسَةِ، وَإِنْ كَانَ فِي السَّاقَةِ كَانَ فِي السَّاقَةِ، إِنْ اِسْتَأْذَنَ لَمْ يُؤْذَنْ لَهُ، وَإِنْ شَفَعَ لَمْ يُشَفَّعْ))

Na katika Swahiyh, Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah(رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Ameangamia mtumwa wa dinari! Ameangamia mtumwa wa dirham! Ameangamia mtumwa wa Al-Khamiyswah! Ameangamia mtumwa wa Al-Khamiylah! Anapopewa huridhika, asipopewa hukasirika. Ameangamia na amehiliki mtu huyo. Na kama akichomwa na mwiba asipate mtu wa kumchomoa. Twuwbaa ashikaye khitamu za farasi wake katika njia ya Allaah hali nywele zake timu timu na miguu yake mavumbi matupu. Akiwekwa katika [kikosi cha] ulinzi huridhika na kazi yake ya ulinzi, na akiwekwa kikosi cha nyuma jeshini huifurahia kazi yake. [Hana makuu wala tamaa. Machoni mwa watu ni mtu duni] kiasi ambacho akiomba ruhusa [kwa mtawala] haruhusiwi; na akishufia, maombezi yake hukataliwa [kwa sababu ya unyenyekevu wake] [Al-Bukhaariy]

 

Al-Khamiysah:     mali na nguo nzuri za fakhari na anasa.

Al-Khamiylah:      nguo za makhmeli.

Twuwbaa:             hongera, furaha au mti wa Jannah unaoitwa hivyo.

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Mtu kutamani mambo ya kidunia kwa kisingizio cha kutenda ya Aakhirah.

 

2-Tafsiri ya Ayaah katika Suwrah ya Huwd (11:15-16).

 

3-Muislamu kuitwa mtumwa wa dinar, dirham, khamiysah (yaani mali na nguo za fakhari na anasa).

 

3-Maelezo kuwa: Yeye anapopewa tu vitu hivyo huridhika, anaponyimwa hukasirika.

 

4-Maana ya maneno: ta'isa wa intakasa: “Ameangamia na amehiliki mtu kama huyo.”

 

5-Maana ya maneno: “akichomwa na mwiba asipate mtu wa kumchomoa.”

 

6-Kuwasifu anayepigana jihaad kwa sifa zilizoelezwa (katika Hadiyth).

 

 

 

 

Share