Duaa Mbali Mbali Za Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
Du'aa ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم baada ya kutoka Twaaif
اَلَّلهُمَّ إِنِّي أَشْكُو إِلَيْكَ ضَعْفَ قُُوَّتِي, وَقِلَّةَ حِيْلَتِي, وَهَوَانِي عَلَى النَّاسِ, يَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِين, أَنْتَ رَبُّ الْمُسْتَضْعَفِينَ وَاَنْتَ رَبّي إِلَى مَنْ تَكِلْنِي؟ إِلَى بَعِيدٍ يَتَجَهَّمُنِي أَمٍ إِلَى عَدُوٍ مَلَّكْتَهُ أَمْرِي؟ إِنْ لَمْ يَكُنْ بِكَ غَضَبٌ عَلَىَّ فَلاَ أُبَاِلي، وَلَكِنَّ عَافِيَتَكَ أَوْسَعُ لِي مِنْ ذُنُوبِي, أَسْأَلُكَ بِنُورِ وَجْهِكَ الَّذِي أَشْرَقَتْ لَهُ الظُّلُمَاتُ، وَصَلَحَ عَلَيْهِ أَمْرُ الدُّنْيَا وَالأَخِرَةِ مِنْ أَنْ يُنْزِلَ عَلَيَّ غَضَبُكَ أَوْ يَحُِلَّ عَلَىَّ سَخَطُُكَ وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِكَ
Allaahumma Inniy Ashkuu Ilayka Dhwa'fa
Ya Allaah , Kwako peke yako nalalamika udhaifu wa nguvu zangu, na uchache wa uwezo wangu na unyonge wangu (wa kukabili adha) za watu. Wewe ndiye mwenye wingi wa Rehma na wingi wa huruma na upole.
Wewe ni Mola wa wasiojiweza na wadhaifu. Nawe ni Mola Wangu. Unanitupa kwenye mikono ya nani (atakayenisaidia)? Kwenye mikono ya jamaa yangu aliye mbali na asiye na huruma na mimi? Ambaye ananihamakia kwa chuki na kunidharau? Au kwenye adui aliyepewa utawala juu ya mambo yangu? Lakini kama ghadhabu Yako haitoanguka kwangu au haitonifikia basi hakuna kitu nitakachojali, Na hakika msamaha Wako ni mkubwa kuliko dhambi zangu.
Nakuomba kutokana na Nuru ya Wajihi wako, ambayo inaangazia mbingu na inaondoa kiza na kutawala mambo yote ya dunia na akhera ili hasira Yako isinifikie au ghadhabu Yako isiniangukie. Na hakuna mamlaka wala nguvu na uwezo ila Wako peke yako.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
