55-Kitaab At-Tawhiyd: Anayeomba kwa Jina la Allaah Hakataliwi

Mlango Wa 55

بَابٌ لا يُرَدُّ مَنْ سَأَلَ بِاَللَّهَ

Anayeomba kwa Jina la Allaah Hakataliwi


 

 

عَنِ اِبْنِ عُمَرَ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((مَنْ سَأَلَ بِاَللَّهِ فَأَعْطُوهُ، وَمَنِ اسْتَعَاذَ بِاَللَّهِ فَأَعِيذُوهُ، وَمَنْ دَعَاكُمْ فَأَجِيبُوهُ، وَمَنْ صَنَعَ إِلَيْكُمْ مَعْرُوفًا فَكَافِئُوهُ، فَإِنْ لَمْ تَجِدُوا مَا تُكَافِئُونَهُ فَادْعُوا لَهُ حَتَّى تَرَوْا أَنَّكُمْ قَدْ كَافَأْتُمُوهُ))  رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ وَالنَّسَائِيُّ بِسَنَدٍ صَحِيحٍ

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayeomba kwa Jina la Allaah, mpeni. Na atakayejikinga kwa Jina la Allaah, mkingeni. Na atakayekualikeni muitikieni. Na atakayekufanyieni wema mlipeni [mema na ihsani]. Msipopata cha kumlipa muombeeni hadi mhisi kuwa mmelipizia wema)) [Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy kwa isnaad Swahiyh]

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Kumpa ulinzi atakayeomba ulinzi kwa Jina la Allaah (سبحانه وتعالى).

 

2-Kumpa aombaye kwa Jina la Allaah (سبحانه وتعالى).

 

3-Kuitikia mwaliko.

 

4-Kumlipa wema aliyekutendea wema.

 

5-Ikiwa mtu hana cha kulipa wema, basi amuombee du’aa badala yake.

 

6-Kauli yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): ((hadi mhisi kuwa mmelipizia wema)).

 

 

Share