213-Aayah Na Mafunzo: Ummah Wetu Ni Wa Mwisho Lakini Wa Kwanza Kuhukumiwa Na Kuingizwa Jannah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Ummah Wetu Ni Wa Mwisho Na Wa Kwanza Kuhukumiwa Na Kuingizwa Jannah

 www.alhidaaya.com

 

كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّـهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ ۚ وَمَا اخْتَلَفَ فِيهِ إِلَّا الَّذِينَ أُوتُوهُ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۖ فَهَدَى اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا لِمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ ۗ وَاللَّـهُ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٢١٣﴾

213. Watu walikuwa ummah mmoja kisha Allaah Akatuma Nabiy wabashiriaji na waonyaji na Akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki ili kihukumu baina ya watu katika ambayo wamekhitilafiana kwayo. Na hawakukhitilafiana katika hayo isipokuwa wale waliopewa hicho (Kitabu) baada ya kuwajia hoja bayana kwa kufanyiana baghi na uhusuda baina yao. Allaah Akawaongoza wale walioamini kuendea haki katika yale waliyokhitilafiana, kwa idhini Yake. Na Allaah Humwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.

 

Mafunzo:

Hudhayfah bin Al-Yamaan (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah Aliwapoteza waliokuwa kabla yetu kutokujua Siku ya Ijumaa. Ilikuwa Mayahudi siku ya Jumamosi na ikawa Manaswara siku ya Jumapili, Akaja Allaah kwetu Akatuongoza (kuifahamu) siku ya Ijumaa Akafanya Ijumaa na Jumamosi na Jumapili na vile vile wao watatufuata sisi siku ya Qiyaamah. Na sisi ni wa mwisho katika watu wa dunia na wa kwanza Siku ya Qiyaamah watakaohukumiwa kabla ya viumbe (wengine).” [Al-Bukhaariy (1415) na katika riwaayah nyengine; “Sisi (Waislamu) watu wa kwanza kuingia Jannah…” [‘Abdur-Raazzaaq (1/82) Tafsiyr Ibn Kathiyr].

 

 

Share