081-Aayah Na Mafunzo: Uthibitisho Kuwa Khidhr Hayuko Hai

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Uthibitisho Kuwa  Khidhr Hayuko Hai

www.alhidaaya.com

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ ۚ قَالَ أَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَىٰ ذَٰلِكُمْ إِصْرِي ۖ قَالُوا أَقْرَرْنَا ۚ قَالَ فَاشْهَدُوا وَأَنَا مَعَكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨١﴾

81. Na pindi Alipochukua Allaah fungamano kwa Manabii (akawaambia) “Kwa yale niliyokupeni kutoka kitabu na hikmah, kisha akakujieni Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi; ni juu yenu kumwamini na kumnusuru.” (Kisha Allaah): Akasema “Je, mmekiri na mmekubali kuchukua juu ya hayo fungamano zito Langu?” Wakasema: “Tumekiri.” (Allaah) Akasema: “Basi shuhudieni na Mimi Niko pamoja nanyi katika wenye kushuhudia.”

 

Mafunzo:

 

Aayah hii ni miongoni mwa dalili za kufariki kwa Khidhwr (عليه السلام) na kuwa yeye amekwishakufa na si kama wanavyodai Masufi kuwa Khidhwr yupo hai,  na  lau kama angelikuwa yupo hai basi angesimama kumnusuru Nabiy Muhammad  (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kauli na matendo.

Share