118-Aayah Na Mafunzo: Kila Nabiy Au Khaliyfah Alikuwa Na Rafiki Mwandani Wawili

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Kila Nabiy Au Khaliyfah Alikuwa Na Rafiki Mwandani Wawili  

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ ۚ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١١٨﴾

118. Enyi walioamini! Msifanye rafiki wandani na msiri (wenu) wasiokuwa nyinyi. Hawatoacha kukuharibieni. Wanatamani kama mngetaabika. Imekwishajitokeza bughudha kutoka midomoni mwao. Na yale yanayoficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Aayaat, (ishara, hoja, dalili) mkiwa mtatia akilini.

 

Mafunzo:

 

Abuu Sa’iyd (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah Hakutuma Nabiy yeyote wala hakumweka Khaliyfah yeyote isipokuwa alikuwa na rafiki mwandani wawili; mmoja anayeamrisha ya kheri na kumsisitiza nayo, na mwengine akiamrisha maovu na kumchochea nayo. Na Al-Ma’swuwm (aliyehifahdiwa asikosee) ni ambaye ma’swuwm (amehifadhiwa asisokee) na Allaah.” [Al-Bukhaariy na An-Nasaaiy].

Share