151-Aayah Na Mafunzo: Miongoni Mwa Matano Aliyopewa Nabiy Ni Kutiwa Kizaazaa Maadui

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Miongoni Mwa Matano Aliyopewa Nabiy Ni Kutiwa Kizaazaa Maadui

 

 

 

سَنُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُوا الرُّعْبَ بِمَا أَشْرَكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا ۖ وَمَأْوَاهُمُ النَّارُ ۚ وَبِئْسَ مَثْوَى الظَّالِمِينَ ﴿١٥١﴾

151. Tutavurumisha kizaazaa katika nyoyo za waliokufuru kwa sababu ya kumshirikisha Allaah na ambayo Hakuyateremshia mamlaka. Na makazi yao ni moto, na ubaya ulioje maskani ya madhalimu

Mafunzo:

 

Abuu Huraryah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nimefadhilishwa juu ya Manabii kwa mambo sita: nimepewa; ‘Jawaami’al-Kalimi’ (mukhtasari unaojumuisha maneno mengi) na nimenusuriwa kwa (kutiwa) kizaazaa (katika nyoyo za maadui) na nimehalalishiwa ghanima na nimefanyiwa ardhi kuwa kitwaharishi na Masjid (mahali pa kuswali) na nimetumwa kwa viumbe wote, na Manabii wamekhitimishwa kwangu.” [Muslim].

 

 

 

Share