125-Aayah Na Mafunzo: Nabiy Muhammad Kutamani Abuu Bakr Awe Khaliyl Wake Duniani

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  Kutamani Abuu Bakr Awe Khaliyl Wake Duniani

 

 

وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۗ وَاتَّخَذَ اللَّـهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا ﴿١٢٥﴾

125. Na nani aliye bora zaidi kwa Dini kuliko yule aliyejisalimisha kwa Allaah naye ni mtendaji mazuri na akafuata mila (Dini) ya Ibraahiym aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki. Na Allaah Amemchukua Ibraahiym kuwa nikipenzi.

 

Mafunzo:

 

Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipotoa khutbah yake ya mwisho alisema: “Ammaa ba’du, enyi watu! Ingekuwa kumfanya khaliyl mtu katika dunia, basi ningelimfanya Abuu Bakr bin Abi Quhaafah kuwa khaliyl wangu, lakini Swahibu wenu ni khaliyl wa Allaah.” (yaani yeye mwenyewe Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 

Share