129-Aayah Na Mafunzo: Tahadharisho La Kumuelemea Mke Mmoja Pekee

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Tahadharisho La Kumuelemea Mke Mmoja Pekee

 

وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَالْمُعَلَّقَةِ ۚ وَإِن تُصْلِحُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٢٩﴾

129. Na wala hamtoweza kuadilisha baina ya wake japokuwa mkipania. Basi msimili muelemeo wote (kwa mke mmoja) mkamuacha (mwengine) kama kining’inio. Na mkisuluhisha na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

Mafunzo:

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Atakayekuwa na wake wawili, kisha akaelemea zaidi kwa mmoja wao, atakuja Siku ya Qiyaamah akipinda upande mmoja (akiuburuza).” [Amehadithia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) ameipokea Abuu Daawuwd].

 

Share