165-Asbaabun-Nuzuwul: Ulipokusibuni Msiba Ingawa Mliwasibu (Maadui) Mara Mbili Yake

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan  165-Ulipokusibuni msiba ingawa mliwasibu (maadui) mara mbili yake

 

أَوَلَمَّا أَصَابَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَدْ أَصَبْتُم مِّثْلَيْهَا قُلْتُمْ أَنَّىٰ هَـٰذَا ۖ قُلْ هُوَ مِنْ عِندِ أَنفُسِكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٦٥﴾

165. Ulipokusibuni msiba ingawa mliwasibu (maadui) mara mbili yake mlisema: “Umetoka wapi huu?” Sema: “Huo ni kutoka kwenu wenyewe.” Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremshwa kuhusu makafiri kutokana na wao kulipiza kisasi ya yale yaliyowasibu katika vita vya Badr. Wakauawa Waislamu sabini siku ya Uhud na yakavunjwa meno ya mbele ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na likavunjwa yai juu ya kichwa chake, na damu zikatirika juu ya uso wake, na hapo ikashuka kauli ya Allaah: Ulipokusibuni msiba ingawa mliwasibu (maadui) mara mbili yake mlisema: “Umetoka wapi huu?” Sema:…” [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amepokea Ahmad]

 

 

 

Share