051-Asbaabun-Nuzuwul: Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini itikadi potofu na twaghuti na...

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

An-Nisaa 051-Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini itikadi potofu na twaghuti na ...

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا هَـٰؤُلَاءِ أَهْدَىٰ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا سَبِيلًا ﴿٥١﴾

51. Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini itikadi potofu na twaghuti na wanasema juu ya wale waliokufuru kuwa: “Hawa wameongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini.”

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَمَن يَلْعَنِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ نَصِيرًا ﴿٥٢﴾

52. Hao ndio wale Allaah Aliowalaani. Na ambaye Allaah Amemlaani basi hatopata wa kumnusuru.

 

Sababun-Nuzwul:

 

Aayah hii imeteremshwa kama alivyohadithia ‘Ikrimah kwamba: Huyay bin Akhtab na Ka’b Al-Ashraf (Wakuu wa Kiyahudi) walikuja kwa watu wa Makkah (washirikina) wakawaambia: Nyinyi (Mayahudi) ni Ahlul-Kitaab na wenye ‘ilmu, hivyo basi tujulisheni (tofauti zetu) kuhusu sisi na kuhusu Muhammad. Wakasema: Jielezeni kuhusu nyinyi na kuhusu Muhammad. Wakasema: Sisi tunaunga ujamaa wa uhusiano wa damu, tunachinja ngamia (kwa ajili ya mafukara), tunasamehe madeni, tunawapa maji Mahujaji. Ama Muhammad, yeye hana watoto wa kiume, amekata ujamaa wa uhusiano wa damu, na wevi wa Mahujaji (kabila la) Ghifaar wanamfuata. Basi je, sisi bora au yeye? Wakasema: Nyinyi bora zaidi na mlioongoka zaidi njia. Hapo Allaah Akateremsha: Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini itikadi potofu na twaghuti na wanasema juu ya wale waliokufuru kuwa: “Hawa wameongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini... mpaka kauli Yake:basi hatopata wa kumnusuru.” (4: 52).

 

 

Share