094-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 094: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا ضَرَبْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَتَبَيَّنُوا

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa  094-Enyi walioamini! Mnapotoka kwenda kwenye Jihaad basi hakikini kila jambo..

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا ضَرَبْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَتَبَيَّنُوا وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَىٰ إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا تَبْتَغُونَ عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٌ ۚ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبْلُ فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَتَبَيَّنُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿٩٤﴾

Enyi walioamini! Mnapotoka kwenda kwenye Jihaad basi hakikini kila jambo, na wala msimwambie anayekuamkieni kwa As-salaam: Wewe si Muumin kwa sababu ya kutamani mafao yapitayo ya uhai wa dunia na hali kwa Allaah kuna ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyokuwa kabla na Allaah Akakufanyieni ihsaan, basi fanyeni uhakiki. Hakika Allaah daima kwa yale myatendayo Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. (4:94).

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka kumzungumzia bwana mmoja ambaye alionekana kwenye vita akiwa ana msururu wa ghanima (ngawira) kisha Waislamu wakamfuata mbio. Yule bwana alipoona Waislamu wamemfikia aliwasalimia, lakini Waislamu walimuua na wakachukua ghanima zake. Na hapo ikateremka hii Aayah hii:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا ضَرَبْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَتَبَيَّنُوا وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَىٰ إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا تَبْتَغُونَ عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٌ ۚ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبْلُ فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَتَبَيَّنُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿٩٤﴾

Enyi walioamini! Mnapotoka kwenda kwenye Jihaad basi hakikini kila jambo, na wala msimwambie anayekuamkieni kwa As-salaam: Wewe si Muumin kwa sababu ya kutamani mafao yapitayo ya uhai wa dunia na hali kwa Allaah kuna ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyokuwa kabla na Allaah Akakufanyieni ihsaan, basi fanyeni uhakiki. Hakika Allaah daima kwa yale myatendayo Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. (4:94).

[Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) na imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]  

Na At-Tirmidhiy na Imaam Ahmad wamerekodi kwamba:

Wakanong’onezana kwamba: “Anasema As-Salaam apate kujihami tu!” Wakamuua kisha wakaenda kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na kondoo hao, ndipo ikateremshwa Aayah hii

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا ضَرَبْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَتَبَيَّنُوا وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَىٰ إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا تَبْتَغُونَ عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٌ ۚ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبْلُ فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَتَبَيَّنُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿٩٤﴾

Enyi walioamini! Mnapotoka kwenda kwenye Jihaad basi hakikini kila jambo, na wala msimwambie anayekuamkieni kwa As-salaam: Wewe si Muumin kwa sababu ya kutamani mafao yapitayo ya uhai wa dunia na hali kwa Allaah kuna ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyokuwa kabla na Allaah Akakufanyieni ihsaan, basi fanyeni uhakiki. Hakika Allaah daima kwa yale myatendayo Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.

(4:94).  

Na Imaam Ahmad amerekodi kwamba Al-Qa’qaa’ bin ‘Abdillaah bin Abiy Hadrad amehadithia kwamba baba yake ‘Abdullaah bin Abiy Hadrad alisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitutuma (maeneo ya) ‘Adhwam. Nikatoka pamoja na kundi la Waislamu ambamo alikuweko Abuu Qataadah, Al-Haarith bin Rab’iy na Muhallam bin Juthmaamah bin Qays. Tukaendelea mpaka tukafika eneo la ‘Adhwam ambako ‘Aamir Al-Ashja’iy alitupitia akiwa amepanda ngamia wake. Alipotupitia akatusalimia na hatukumhujumu. Lakini Muhallam bin Juthmaamah alimuua na kuchukua ngamia wake kwa sababu ya matatizo baina yao. Tuliporudi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) tukamuhadithia yaliyotokea, hapo ikatuteremkia Qur-aan:

Share