100-Asbaabun-Nuzuwul: Na anayehajiri katika njia ya Allaah atapata katika ardhi…

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

 

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

An-Nisaa 100-Na anayehajiri katika njia ya Allaah atapata katika ardhi…

 

وَمَن يُهَاجِرْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ يَجِدْ فِي الْأَرْضِ مُرَاغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً ۚ وَمَن يَخْرُجْ مِن بَيْتِهِ مُهَاجِرًا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ يُدْرِكْهُ الْمَوْتُ فَقَدْ وَقَعَ أَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٠﴾

100. Na anayehajiri katika njia ya Allaah atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia kujihifadhi na rizki. Na atakayetoka nyumbani kwake akiwa ni mwenye kuhajiri kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake, kisha mauti yakamfikia, basi ujira wake umehakikika kwa Allaah. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Ilipoteremka kauli ya Allaah: “Hakika wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamejidhulumu nafsi zao” (4: 97).  Palikuweko mtu mmoja Makkah akiitwa Dhwamrah, yeye alikuwa ni mgonjwa akaiambia familia yake: “Nitoeni Makkah kwani nahisi joto kali la maradhi.” Familia yake wakamuuliza: “Tukupeleke wapi?” Akaashiria kwa mkono wake kuwa wampeleke Madiynah. Hapo ikateremka Aayah hii: “Na anayehajiri katika njia ya Allaah atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia na wasaa. Na atakayetoka nyumbani kwake…” (4; 100). [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ameipokea Ibn Jariyr].

 

Share