082-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Maaidah Aayah 082: ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنْهُمْ قِسِّيسِينَ وَرُهْبَانًا وَأَنَّهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Maaidah 082-Hivyo ni kwa kuwa miongoni mwao kuna Makasisi na Wamonaki  na kwamba wao hawatakabari.

 

 

لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا ۖ وَلَتَجِدَنَّ أَقْرَبَهُم مَّوَدَّةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنْهُمْ قِسِّيسِينَ وَرُهْبَانًا وَأَنَّهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٨٢﴾

82. Bila shaka utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa wale walioamini, ni Mayahudi na wale washirikina. Na bila shaka utawakuta walio karibu zaidi kimapenzi kwa Waumini ni wale wanaosema: “Sisi ni Manaswara.” Hivyo ni kwa kuwa miongoni mwao kuna Makasisi na Wamonaki  na kwamba wao hawatakabari.

 

وَإِذَا سَمِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَى الرَّسُولِ تَرَىٰ أَعْيُنَهُمْ تَفِيضُ مِنَ الدَّمْعِ مِمَّا عَرَفُوا مِنَ الْحَقِّ ۖ يَقُولُونَ رَبَّنَا آمَنَّا فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨٣﴾

83. Na wanaposikia yale yaliyoteremshwa kwa Rasuli utaona macho yao yanachuruzika machozi kutokana na yale waliyoyatambua ya haki. Wanasema: “Rabb wetu tumeamini, basi Tuandike pamoja na wenye kushuhudia.”

 

وَمَا لَنَا لَا نُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا جَاءَنَا مِنَ الْحَقِّ وَنَطْمَعُ أَن يُدْخِلَنَا رَبُّنَا مَعَ الْقَوْمِ الصَّالِحِينَ ﴿٨٤﴾

84. “Na kwa nini Tusimwamini Allaah na haki iliyotufikia na hali tunatumai Rabb wetu Atuingize (Jannah) pamoja na Swalihina?”

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii na zinazofuatia (5: 82-85) zimeteremshwa kumzungumzia An-Najaashiy ambaye alikuwa mfalme wa Habash pamoja na watu wake. Aliwakilisha wajumbe wamwendee Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ili wamsikilize maneno yake na watambue sifa zake. Walipokutana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), aliwasomea Qur-aan. Wakalia kwa machozi tele na wakanyenyekea na wakaingia Uislamu. Kisha wakarudi kwa An-Najaashiy kumjulisha yaliyojiri. [Athar kutoka kwa Saiy’d bin Jubayr, As-Suddi na wengineo.  Tafsiyr Ibn Kathiyr]  

 

Pia Sababun-Nuzuwl: Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba: Waislamu walipohajiri kutoka Makkah kwenda Habash wakiwa katika uongozi wa Ja’far bin Abiy Twaalib na Ibn Mas’uwd (رضي الله عنهم), walimkuta mfalme wao An-Najaashiy akiwa mkarimu na mwenye huruma kwao. Akawauliza kama wana chochote cha Wahyi kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Walipomsomea Aayaat za Qur-aan wakati alikuwa pamoja na makasisi na wamonaki wake, walimiminikwa na machozi kutokana na kutambua haki. Ndipo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

 

ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنْهُمْ قِسِّيسِينَ وَرُهْبَانًا وَأَنَّهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٨٢﴾

 

Hivyo ni kwa kuwa miongoni mwao kuna Makasisi na Wamonaki na kwamba wao hawatakabari.

 

وَإِذَا سَمِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَى الرَّسُولِ تَرَىٰ أَعْيُنَهُمْ تَفِيضُ مِنَ الدَّمْعِ مِمَّا عَرَفُوا مِنَ الْحَقِّ ۖ يَقُولُونَ رَبَّنَا آمَنَّا فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨٣﴾

Na wanaposikia yale yaliyoteremshwa kwa Rasuli utaona macho yao yanachuruzika machozi kutokana na yale waliyoyatambua ya haki. Wanasema: Rabb wetu tumeamini, basi Tuandike pamoja na wenye kushuhudia.

 

 

وَمَا لَنَا لَا نُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا جَاءَنَا مِنَ الْحَقِّ وَنَطْمَعُ أَن يُدْخِلَنَا رَبُّنَا مَعَ الْقَوْمِ الصَّالِحِينَ ﴿٨٤﴾

Na kwa nini Tusimwamini Allaah na haki iliyotufikia na hali tunatumai Rabb wetu Atuingize (Jannah) pamoja na watu Swalihina? (5:82-84).

 

Na katika riwaayah nyengine: “Ja’far (رضي الله عنه) aliwasomea Suwrat Maryam wakamiminikwa machozi…”

 

  

 

 

Share