089-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Maaidah Aayah 089: فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

Al-Maaidah    089-Basi kafara yake ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu

 

 

 

 لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٨٩﴾

Allaah Hatokuchukulieni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini Atakuchukulieni kwa (kuvunja) viapo mlivyoapa kwa niyyah mlioifunga thabiti. Basi kafara yake ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu, au kuwavisha nguo, au kuacha huru mtumwa. Lakini asiyeweza kupata (katika hayo), basi afunge Swiyaam siku tatu. Hiyo ndio kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na hifadhini yamini zenu. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na hukmu) Zake ili mpate kushukuru. [Al-Maaidah (5:89)]

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ  

 

Basi kafara yake ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu. (5:89).

 

Imeteremka kutokana na mtu ambaye alikuwa akilisha familia yake chakula kingi cha kutosheleza, lakini akilisha wengine anawapa chakula hafifu kisichotosheleza. Hapo ikateremshwa:

 

مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ  

cha wastani mnachowalisha ahli zenu.

 

[Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) , imepokelewa na Ibn Maajah]

 

 

 

 

Share