13-Imaam Ibn Baaz: Watoto Waamrishwe Swiyaam Wanapofikisha Miaka Saba

Watoto Waamrishwe Swiyaam Wanapofikisha Miaka Saba

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, mvulana ambaye kakomaa anapaswa kuamrishwa swiyaam? Je, Swawm yake ni sahihi ikiwa atabaleghe wakati wa Swawm (katika Ramadhwaan)?

 

JIBU:

 

Ikiwa wavulana na wasichana wanafikisha umri wa miaka saba wanapaswa kuamrishwa kuanza swiyaam ili wajizoeze. Wazazi wao ni juu yao kuwaamrisha Swawm hali kadhalika kama wanavyopasa kuwaamrisha Swalah. Wanapobaleghe, Swawm imewawajibikia. Ikiwa watakomaa wakati wa Swawm, siku zao (wanazofunga) ni sahihi. Ikiwa mvulana atafikisha miaka kumi na tano mchana wakati yuko na Swawm, siku yake ni sahihi. Mwanzo wa siku hiyo (Swawm kwake) ilikuwa ni Sunnah na mwisho wake itakuwa ni waajib ikiwa tayari kishatokwa na nywele za sehemu za siri au kishaanza kutokwa na manii. Hali kadhalika inawahusu wanawake ambao wanabaleghe kwa kutokwa na damu ya hedhi.

 

[Fataawa Ibn Baaz Hukmu Amr Asw-Swabiy Al-Mumayyiz Bisw-Swiyaam]

 

 

Share