11-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Hakulipa Swawm Alipokuwa Katika Hedhi Miaka Yote Iliyopita Ya Ramadhwaan

Hakulipa Swawm Alipokuwa Katika Hedhi Miaka Yote Iliyopita Ya Ramadhwaan

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI: 

 

Bibi mtu mzima mwenye umri wa miaka 60 alikuwa hajui hukumu ya kulipa Swawm alizokuwa hafungi wakati alipokuwa katika hedhi miaka mingi.  Miaka yote iliyompita hakulipa siku zake za Swawm za Ramadhwaan akifikiri kwamba kulikuwa hakuna haja ya kuzilipa.  Hivi ni kutokana na alivyosikia kutoka kwa watu.

 

 

JIBU:

 

Inampasa aombe maghfirah na tawbah kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kutokuuliza wenye elimu. 

Kisha alipe siku zote alizokuwa hakufunga na alipe kafara kwa kulisha maskini mmoja nusu pishi (vibaba viwili ambavyo ni sawa na 1.5kg) ya shayiri au tende au mchele au chakula chochote kinachotumika (sana) katika nchi anayoishi. Hivyo ni kama anao uwezo, na ikiwa hana uwezo wa kulisha maskini basi inamtosha kulipa tu siku alizokuwa hakufunga.

 

Wa biLLaahi at-tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

 

[Al-Lajnah Ad-Daaimah - Halmashauri ya kudumu ya Utafiti Wa Kiislaam Inayoongozwa:

Kiongozi Mkuu: Shaykh 'Abdul 'Aziyz ibn 'Abdillaah  ibn Baaz

Msaidizi Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdullaah ibn Ghudayyaan

Mwanachama: Shaykh 'Abdullaah Ibn Ghudayyan

Mwanachama: Shaykh ‘Abdullah ibn ‘Awd

Fataawa Ramadhwaan - Mjalada 2, Ukurasa  583, Fatwa Namba 567]
Fataawa al-Lajnah ad-Daaimah lil-Buhuuth al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. - Fatwa Namba 1790]

 

 

Share