16-Imaam Ibn Baaz: Anayemuona Mtu Anakula Ramadhwaan Kwa Kusahau Amkumbushe?

 

Anayemuona Mtu Anakula Ramadhwaan Kwa Kusahau Amkumbushe?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, nimkumbushe mtu ambaye anakula na kunywa (Ramadhwaan) kwa kusahau?

 

 

JIBU:

 

Ndiyo, anatakiwa amtanabahishe ikiwa anamuona mtu huyo  anakula au kunywa na amwambie “Wewe umefunga”. Amtanabahishe kwa sababu ni munkari, munkari ulio wazi.

 

Hata kama mtu ni mwenye kughufuriwa kwa sababu ya kusahau kwake, si katika wakati ule. Anatakiwa kukumbushwa mtu kama huyo.

 

 

[Nuwr 'Alaa Ad-Darb, Fatwa na. 9834]

 

Share