23-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Inajuzu Kwa Mu’takif Apige Simu Kukidhi Haja Za Baadhi Ya Waislamu?

 

 

Inajuzu Kwa Mu’takif Apige Simu Kukidhi Haja Za Baadhi Ya Waislamu?

 

 Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

23. Je, Inajuzu Kwa Mu’takif Apige Simu Kukidhi Haja Za Baadhi Ya Waislamu?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

a. Inajuzu kwa Mu’takif kutumia simu kwa ajili ya kuwakidhia haja za Waislamu ikiwa simu iko katika Msikiti ambao anatekeleza I’tikaaf, kwa sababu hatoki nje ya Msikiti.

 

b. Ama ikiwa nje ya Msikiti basi asitoke kwa ajili ya jambo hilo. Na kuwakidhia haja Waislamu ikiwa mtu huyo ndiye mwenye jukumu nao basi asikae I’tikaaf kwa sababu kuwakidhia haja Waislamu kuna umuhimu zaidi kuliko kutekeleza I’tikaaf. 

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/180)]

 

Share