28-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kuwapa Zakaatul-Fitwr Jamaa

Kuwapa Zakaatul-Fitwr Jamaa

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya  Zakaatul-Fitwr kupewa jamaa walio masikini?

 

JIBU:

 

Inaruhusiwa kutoa Zakaatul-Fitwr na Zakaah ya mali kuwapa jamaa walio masikini. Na hakika kuwapa jamaa ni bora kuliko kuwapa watu wageni kwa sababu kuwapa jamaa huwa ni sadaka na pia kuunga ukoo. Lakini sharti isiwe kwa ajili ya kuhifadhi mali yake ambayo ndivyo itakavyokuwa hali ikiwa jamaa yenyewe aliye maskini ni ambaye mwenye jukumu naye kumhudumia. Kwa hali hiyo hairuhusiwi kumtimizia mtu haja kwa chochote katika Zakaah yake kwa sababu akifanya hivyo atakuwa anahifadhi mali yake kutokana na anachokitoa (kwa maana atakuwa anataoa Zakaah yake kwa kumpa mtu ambaye ni wajibu wake kumhudumia) Nayo haipasi wala kuruhusiwa.

 

Lakini ikiwa hana majukumu naye basi anaweza kumpa Zakaah bali kutoa Zakaah yake kwa jamaa ni bora kuliko kumpa mtu mgeni kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)   amesema: ((Swadaqah zenu kwa jamaa ni swadaqah na pia ni kuunga ukoo))

 

 [Majmuw' Fataawaa Shaykh Ibn 'Uthaymiyn (18/301]

 

 

Share