Imaam Muqbil Al-Waadi’iy: Nasiha Kwa Anayeiga Kisomo Cha ‘Abdul-Baasitw ‘Abdusw-Swamad Na Kumsikiliza

 

Nasiha Kwa Anayeiga Kisomo Cha ‘Abdul-Baasitw ‘Abdusw-Swamad Na Kumsikiliza

 

Shaykh Muqbil Bin Haadiy Al-Waadi’iy (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Amesema Shaykh Muqbil Al-Waadi’iy (Rahimahu Allaah) katika kubainisha hali ya ‘Abdul-Baasitw ‘Abdusw-Swamad (aliyekuwa msomaji Qur-aan maarufu wa Misri) na dalili ya kuwa kwake mbali na Sunnah na kutoipa kwake umuhimu (hiyo Sunnah).

 

Amesema (Shaykh Muqbil – Rahimahu Allaah):

“Kuna watu (wanaposoma Qur-aan) hawanyanyui kichwa (hawajibidiishi) katika kuisoma kwa sauti nzuri.

Na kuna wengine wanaovuka mipaka (katika kuremba sauti) kama ‘Abdul-Baasitw. Utakapomsikia akisoma nawe uko mbali (humuoni) basi hutoweza kujua kama hiyo ni nyimbo au kisomo cha Qur-aan!

 

 

[Qam’u Al-Mu’aanid, uk. 435]

 

 

Na Aliulizwa (Rahimahu Allaah) kuhusiana na njia sahihi ya kuhifadhi Qur-aan, na katika yale aliyoyasema kujibu:

“Vilevile ni kuchukua (kusoma) kutoka kwa Mashaykh na kuhifadhi chini yao, na usipopata, basi nakunasihi utosheke na kanda za wasomaji waliomakinika ambao wanasoma kisomo kilichosalimika na wala hawasomi kwa kuvuta kupita kiasi (kwa kuremba hadi anavunja ahkaam za usomaji) kama anavyofanya ‘Abdul-Baasitw.

 

 

[Tuhfatu Al-Mujiyb, uk. 157]

 

 

Na akasema tena sehemu nyingine (Rahimahu Allaah):

“Alienda Iran (Kwa Mashia) na akaadhini, na akasema katika adhana yake “Ash-hadu Anna ‘Alliyyan waliyuLLaah”!

Anafanya bid’ah ovu wala hajali ! (Kwa kuwaridhisha Mashia).

 

 

[Al-Makhraj Minal Fitan, uk. 20]

 

 

 

Share