Imaam Muqbil Al-Waadi'y: Mirungi Haina Khayr Bali Inasababisha Madhara Na Ufisadi

Hukmu Ya Kula Mirungi

 

Imaam Muqbil bin Haadiy Al-Waadi'iy (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Ni ipi hukmu ya kishari'ah ya kula Mirungi?

 

 

JIBU:

 

Mirungi ni mti ambao hauna khayr ndani yake.

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amewatahini watu wa Yemen na Wahabashi kwa mti huu muovu. Na jambo sahihi ni kuwa (mti huu wa mirungi) umeleta uharibifu kwa uchumi wetu, umeleta uharibifu kwa afya zetu, na umepoteza wakati wetu, bali umepoteza akili zetu. Wengi vichaa kwa sababu ya mirungi.

 

Hivyo, ninawanasihi kila ndugu ajiweke mbali na mti huu muovu, ambao umewapotezea watu wa Yemen wakati wao (mkubwa), na umewapotezea umri wao, na umewafanya watu wengi kuwa ni waraibu (wa mirungi).

 

Huo ni mti muovu wenye kusababisha madhambi, namnasihi kila Muislamu kujiepusha mbali nao.

 

Na ninapenda Allaah Awawafiqishe watu wa Yemen na Awabadilishie kwayo kwa mazao mema yenye kunufaisha nchi yao.

 

Ni waajib kwa 'Ulamaa na Madaktari na Walinganiaji katika njia ya Allaah (wawatahadharishe) watu (kukimbia mbali kuuacha) mti huu muovu ambao umetuacha tukiwa tunasubiri kutoka Marekani na kwengineko nafaka kama thomu na shamari.

 

Na hivi ndivyo, kila jambo  sisi tumekuwa tegemezi kwa maadui zetu, pamoja na kuwa Yemen ilikuwa ikijulikana hadi kupachikwa jina 'Yemen ya Kijani' (kwa uzalishaji mazao), lakini sasa kwa sababu ya Mirungi, inapaswa kupachikwa jina 'Yemen ya vumbi' (kwa ukame)'.

 

 

[Kutoka katika kanda: 'As-ilah Ba'adhw Al-Akhawaat Min Ta'iz']

 

 

Share