أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
031: Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu katika kila Masjid
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿٣١﴾
31. Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu katika kila Masjid; na kuleni na kunyweni; na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu.
Sababun-Nuzwul:
Sa’iyd bin Jubayr amehadithia kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba: Washirikina wanawake na wanaume walikuwa wakitufu Al-Ka’bah. Wanaume wakitufu mchana na wanawake wakitufu usiku. Wanawake wakisema wanapotufu: Leo baadhi yake (uchi) au wote uonekane na kitakachoonekana sikitolei ruhusa. Hapo ikateremka: “Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu katika kila Masjid” (7: 31).