162-Aayah Na Mafunzo: Du’aa Mojawapo Ya Kufungulia Swalaah

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-An’aam:  162

 

162-Du’aa Mojawapo Ya Kufungulia Swalaah

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٢﴾

Sema: Hakika Swalaah yangu, na ‘Ibaadah yangu ya kuchinja, na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee Rabb wa walimwengu.

 

 

لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ ﴿١٦٣﴾

Hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza (katika ummah huu).

 

 

Mafunzo:

 

Faida: Aayah (6: 161- 162) ni mojawapo ya du’aa ya kufungulia Swalaah: Pia Aayah hii ni dalili mojawapo ya haramisho la kuchinja kwa kukusudia asiyekuwa Allaah (سبحانه وتعالى).

 

Du’aa Mojawapo Ya Kufungulia Swalaah:

 

وَجَّهـتُ وَجْهِـيَ لِلَّذي فَطَرَ السَّمـواتِ وَالأَرْضَ حَنـيفَاً وَمـا أَنا مِنَ المشْرِكين، إِنَّ صَلاتـي، وَنُسُكي، وَمَحْـيايَ، وَمَماتـي للهِ رَبِّ العالَمين، لا شَريـكَ لَهُ وَبِذلكَ أُمِرْتُ وَأَنا مِنَ المسْلِـمين.

 

Wajjahtu wajhiya liLLadhiy fatwaras-samaawaati wal ardhwa haniyfan wamaa ana minal mushrikiyn. Inna swalaatiy, wanusuky, wamahyaaya wamamaatiy liLLaahi Rabbil ‘aalamiyn. Laa shariyka Lahu wabidhaalika umirtu wa anaa minal Muslimiyn.

 

Nimeuelekeza uso wangu kwa yule Ambaye Ameanzisha mbingu na ardhi hali ya kuelemea katika haki, na sikuwa mimi ni katika washirikina, hakika Swalaah yangu na kuchinja kwangu na uhai wangu, na kufa kwangu ni kwa Allaah Rabb walimwengu, Hana mshirika, na kwa hilo nimeamrishwa nami ni katika Waislamu. 

Na katika riwaaya nyenginezo inaishia kwa:

 

وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ

nami ni Muislamu wa kwanza.

 

Kisha Du'aa inaendelea:

 

اللّهُـمَّ أَنْتَ المَلِكُ لا إِلهَ إِلاّ أَنْت، أَنْتَ رَبِّـي وَأَنـا عَبْـدُك، ظَلَمْـتُ نَفْسـي وَاعْـتَرَفْتُ بِذَنْبـي فَاغْفِرْ لي ذُنوبي جَميعاً إِنَّـه لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إلاّ أَنْت، وَاهْدِنـي لأَحْسَنِ الأَخْلاقِ لا يَهْـدي لأَحْسَـنِها إِلاّ أَنْـت، وَاصْـرِف عَـنّْي سَيِّئَهـا، لا يَصْرِفُ عَـنّْي سَيِّئَهـا إِلاّ أَنْـت، لَبَّـيْكَ وَسَعْـدَيْك، وَالخَـيْرُ كُلُّـهُ بِيَـدَيْـك، وَالشَّرُّ لَيْـسَ إِلَـيْك، أَنا بِكَ وَإِلَيْـك، تَبـارَكْتَ وَتَعـالَيتَ, أَسْتَغْـفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيك

 

Allaahumma Antal-Maliku laa ilaaha illa Anta. Anta Rabbiy wa ana ‘abduka, dhwalamtu nafsiy wa’taraftu bidhambiy faghfirly dhunuwbiy jamiy’an innahu laa yaghfirudh-dhunuwba illa Anta. Wahdiniy liahsanil-akhlaaqi laa yahdiy liahsanihaa illa Anta, waswrif ‘annyi sayyiahaa laa yaswrif ‘anniy sayyiahaa illa Anta. Labbayka wasa’dayka walkhayru kulluhu biyadika, wash-sharru laysa Ilayka, ana bika wa Ilayka, Tabaarakta wa Ta’aalayta, astaghfiruka wa atuwbu Ilayka

 

Ee Allaah, Wewe Ndiye Mfalme, hapana  mwabudiwa wa haki ila Wewe, Wewe Ndiye Rabb wangu na mimi ni mja Wako. Nimedhulumu nafsi yangu, na nimekiri madhambi yangu kwa hivyo nighufurie madhambi yangu yote, hakika haghufurii madhambi, ila Wewe.  Na niongoze kwenye tabia nzuri kwani haongozi kwenye tabia nzuri ila Wewe. Niepushe na tabia mbaya, kwani hakuna mwenye uwezo wa kuniepusha na tabia mbaya ila Wewe.  Naitikia mwito Wako, na nina furaha kukutumikia, na kheri zote ziko mikononi Mwako, na shari haitoki Kwako, mimi nimepatikana kwa ajili Yako, na nitarudi Kwako, Umebarikika na Umetukuka, nakuomba maghfirah na narudi Kwako kutubia [Hadiyth ya ‘Aliy bin Abi Twaalib  (رضي الله عنه) - Muslim (1/534)]

 

Share