180-Aayah Na Mafunzo: ‘Aqiydah Sahihi Kuhusu Majina Mazuri Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Atakayehifadhi Ataingia Jannah

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-A’raaf 180

 

180-‘Aqiydah Sahihi Kuhusu Majina Mazuri Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Atakayehifadhi Ataingia Jannah

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٨٠﴾

Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopotoa na kuharibu Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [Al-A'raaf: 180]

 

 

Mafunzo:

 

Kumpwekesha Allaah Katika Majina Yake Na Kuthibitisha Sifa Za Allaah (سبحانه وتعالى) Na Ndio Aqiydah Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kuhusiana Na Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Na Sifa Zake:

 

Aqiydah ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah kuhusiana na Majina Mazuri kabisa ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Sifa Zake ni Tawqiyfiyyah;  Yanathibitishwa Aliyoyathibitisha Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى) katika Qur-aan na Sunnah bila kuzifanyia Ta'twiyl (kuzipinga, kukanusha uwezekano), wala Tamthiyl (kumithilisha, kufafanisha, kulinganisha), wala Takyiyf (kuainisha maana na kuziulizia namna yake au kuuliza ni vipi Sifa hiyo ipo, kuchunguza ni kwa “namna gani” zimefungamana au kuambatana na Allaah), wala Tahriyf (kubadilisha maana, kupotosha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutoa maana isiyo sahihi).

 

Rejea: An-Nisaa (4:164).

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه ـ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ إِنَّ لِلَّهِ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ اسْمَا مِائَةً إِلاَّ وَاحِدًا مَنْ أَحْصَاهَا دَخَلَ الْجَنَّةَ ‏"‏‏.‏

Amesimulia Abuu Hurayrah(رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaaah  (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Ana Majina tisini na tisa,  atakayeyahifadhi ataingia Jannah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Maana ya أَحْصَاهَا ni: Kufahamu maana Zake, kuyahifadhi, kuyafanyia kazi, kuyatumia katika kuomba Du’aa. 

 

 

 

Share