001-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Anfaal Aayah 001: يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

Al-Anfaal: 1

01- Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira. Sema: Ngawira ni ya Allaah na Rasuli.

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١﴾

Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira. Sema: Ngawira ni ya Allaah na Rasuli. Basi mcheni Allaah na suluhisheni yaliyo baina yenu. Na mtiini Allaah na Rasuli Wake mkiwa ni Waumini. [Al-Anfaal: 1]

Sababun-Nuzuwl: 

Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Musw’ab bin Sa’d (رضي الله عنه) kutoka kwa baba yake kwamba: “Aayah nne za Qur-aan zimeteremshwa kuhusu mimi. Niliukuta upanga (katika ngawira za vita). Ukaletwa kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Baba yangu akasema: Ee Rasuli wa Allaah, nipatie mimi. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Uweke hapa! Kisha (baba yangu) akasimama na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Uweke ulipoukuta.” Kisha akasimama akasema: Ee Rasuli wa Allaah, nipatie mimi. Akamwambia: “Uweke!” Akasimama akasema tena: Ee Rasuli wa Allaah nipatie. Je, nitafanywa kama ambaye hana sehemu (ya ngawira)?  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Uweke ulipoukuta.” Hapo ikataremshwa:

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١﴾

Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira. Sema: Ngawira ni ya Allaah na Rasuli.

 [Muslim Kitaab Al-Jihaad was-Siyar, Baab Al-Anfaal]

Pia Musw-‘ab bin Sa’d amehadithia kutoka kwa baba yake (Sa’d bin Abiy Waqqaasw): “Nilikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) siku ya Badr nikiwa na upanga nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, hakika Allaah Amenipa shifaa ya kifua changu kutokana na adui leo, basi nipe upanga.” Akasema: “Upanga si wangu wala si wako.”  Nikaondoka huku nikisema: “Leo atapewa huo (upanga) mtu ambaye hakutiwa mtihanini kama mimi.” Mara akaja mjumbe akaniambia: “Itikia.”  Nikadhani kwamba imeteremshwa Wahy kuhusu mimi kutokana na kauli yangu. Nikaenda kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ulinitaka nikupe upanga huu lakini huu haukuwa wangu wala wako. Lakini sasa Allaah Amenipa mimi kwa hiyo sasa ni wako.” Kisha akasoma:

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١﴾

Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira. Sema: Ngawira ni ya Allaah na Rasuli.

 [Abuu Daawuwd, Kitaab Al-Jihaad

Share