017-Asbaabun-Nuzuwl: Hamkuwaua Nyinyi Lakini Allaah Ndiye Aliyewaua. Na Wala Hukurusha...

 

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

Al-Anfaal:  17

 

 

17- Hamkuwaua nyinyi, lakini Allaah Ndiye Aliyewaua. Na wala hukurusha..

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

  

فَلَمْ تَقْتُلُوهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ قَتَلَهُمْ ۚ وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ رَمَىٰ ۚ وَلِيُبْلِيَ الْمُؤْمِنِينَ مِنْهُ بَلَاءً حَسَنًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١٧﴾

17. Hamkuwaua nyinyi, lakini Allaah Ndiye Aliyewaua. Na wala hukurusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم mchanga) pale uliporusha lakini Allaah Ndiye Aliyerusha; ili Awajaribu Waumini jaribio zuri kutoka Kwake. Hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Kuhusu kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Na wala hukurusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم mchanga) pale uliporusha lakini Allaah Ndiye Aliyerusha.”  Amehadithia Hakiym bin Hizaam kwamba Imeteremshwa siku ya Badr pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoamrisha akateka changarawe za mawe mkononi akatukabili kwazo na kuturushia akasema: “Nyuso zinyauke.” Tukashindwa. Allaah (عز وجل) Akateremsha: Na wala hukurusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم mchanga) pale uliporusha lakini Allaah Ndiye Aliyerusha.”  [Atw-Twabaraaniy].

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share