019-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Anfaal Aayah 019: إِن تَسْتَفْتِحُوا فَقَدْ جَاءَكُمُ الْفَتْحُ ۖ وَإِن تَنتَهُوا فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَإِن تَعُودُوا نَعُدْ

 

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

Al-Anfaal: 19

 

 

 

019- Mkitafuta hukmu (enyi makafiri), basi imeshakujieni hukmu. 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

إِن تَسْتَفْتِحُوا فَقَدْ جَاءَكُمُ الْفَتْحُ ۖ وَإِن تَنتَهُوا فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَإِن تَعُودُوا نَعُدْ وَلَن تُغْنِيَ عَنكُمْ فِئَتُكُمْ شَيْئًا وَلَوْ كَثُرَتْ وَأَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٩﴾

Mkitafuta hukmu (enyi makafiri), basi imeshakujieni hukmu. Na mkikoma (ukhalifu) basi hivyo ni kheri kwenu. Na mkirudia (kuhujumu) Nasi Tutarudia, na wala kundi lenu halitokufaeni kitu chochote japo likikithiri. Na Hakika Allaah Yu Pamoja na Waumini. [Al-Anfaal: 19]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Amesimulia ‘Abdullaah bin Tha’labah bin Swughayr  (رضي الله عنه)   kwamba aliyeomba hukmu siku ya Badr alikuwa ni Abuu Jahl. Alisema pale majeshi mawili yalipokutana: “Ee Allaah, muangamize miongoni mwetu yeyote yule anayekata undugu na akaleta ambayo hatukupatapo kuyajua.” Hiyo ndiyo hukmu aliyoiomba na Allaah Akateremsha:

 

إِن تَسْتَفْتِحُوا فَقَدْ جَاءَكُمُ الْفَتْحُ ۖ  

Mkitafuta hukmu (enyi makafiri), basi imeshakujieni hukmu.    [Ibn Jariyr (9/208), Musnad (5/431), Al-Haakim amesema Hadiyth Swahiyh]

 

 

 

Share