Custard Ya Fruti Ya Kupambwa Kwa Vipipi

 

Custard Ya Fruti Ya Kupambwa Kwa Vipipi

 

 

 

Vipimo

 

Unga wa custard – vijiko 3 vya kulia.

Sukari – vijiko 3 vya kulia takriban kiasi upendavyo

Maziwa – vikombe 2

Vanilla – vijiko 2 vya chai

Fruti zilokatwakatwa upendazo kama ndizi, embe, machungwa, apple, peaches, plums, kiwi na kadhaalika

Biskuti – 200 gms

Cream tamu iliyopigwa (Whipped) – 250 ml

 

 

Kwa Ajili Ya Kupambia:

 

Slaisi za matunda

Chokoleti ilokunwa (grated)

Vipipi vya rangi rangi vya kupambia keki

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

 

  1. Changanya unga wa custard na sukari na ½ kikombe cha maziwa. Changanya vizuri kusiweko na madonge.
  2. Weka sufuria katika moto mimina maziwa yaliyobakia kisha mimina mchanganyiko wa custard uache ichemke huku ukikoroga bila kuachia mkono.
  3. Ichemshe kiasi dakika chache mpaka iwe nzito kiasi.
  4. Epua iache ipoe. Kisha mimina vipande vya fruti ulivyokatakata.
  5. Ponda biskuti kisha gawa  katika vibakuli vya kupakulia custard.
  6. Mimini mchanganyiko wa custard kiasi kiasi juu ya biskuti.
  7. Piga cream mpaka iwe nzito kisha tia icing sugar, uchanganye.
  8. Pakaza mchangayiko wa icing sugar na cream juu ya custard.
  9. Pambia slaisi za fruit na vipipi vya rangi rangi au chokoleti.
  10. Weka katika friji ikiwa tayari.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

Share