Ramadhaan Kariym Swawm Maqbul InshaAllaah
Namauomba Rahmani
Awape Maisha Mema Yastara Na Amani
Na Dawama Ya Neema Awazidishe Imani
Mupate Njema Khatima Muifunge Ramadhani
Kwa Kheri Na Kwa Salama
Mikono Nainyanyua
Kwa Dua KUwaombea
Mola Ajaalie Kheri Kuwafungulia
Duwa Kuwatakabalia
Dhambi Zote Kuwafutia
Thawabu Tele Kuwaandikia
Dhiki Zote Kuwaondolea
Furaha Nyingi Kuwatilia
Jahanamu Kuwaepushia
Firdausi Kuwaruzukia
Si Kwa Ibada Munazomfanyia
Inshallah Peponi Mutaingia
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
