Alama Za Mnafiki
Mtungaji: 'ALIY 'UMAR 'UTHMAAN
Alama za wanafiki, ni tatu bora uzijue
Katu nae haaminiki, japo ahadi azitoe
Pia na hasadikiki, hatumizi maaganoe
Alama yake ya pili, mnafiki ni mrongo
Maisha hana ukweli, wala mizuri mipango
Yake usiyakubali, atakukoroga bongo
Akiaminiwa hukhini, mnafiki ni sifaze
Hachi na hana dini, hudhulume nduguze
Usimtie nyumbani, na sirizo simjuze
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
