Imaam Muqbil Al-Waadi’iy: Je, Allaah Yuko Wapi?

 

Je, Allaah Yuko Wapi?

 

Imaam Muqbil Al-Waadi’iy (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya anayesema: “Allaah Hayuko chini wala juu wala kuliani wala kushotoni, na wala Hayuko nje ya dunia hii wala ndani yake… “ na (maneno) kama  hayo?

 

JIBU:

 

Huyo ni  mzushi (mubtadi’).

 

Sisi tunaamini kwamba hakika Allaah Yuko juu ya ‘Arshi Yake na kupanda Kwake ni namna inayolingana na Utukufu Wake  Mwenyewe kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾

Ar-Rahmaan; Yuko juu (Istawaa[1]) ya ‘Arsh. [Twahaa: 5]

 

Nasi tunaamini kauli Zake Allaah na tunakanusha kauli za Mu’tazilah na ninasisitiza isomwe

العلو للعلي الغفار

 

“Al-‘Uluww lil-‘Aliyy Al-Ghafaar”

 

cha Imaam Adh-Dhahabiy na mukhatasari wake wa Shaykh Al-Albaaniy.”

 

[Ijaabatu-saail ‘alaa Ahammil-Masaail Swali Namba 152 Uk. 300]

 

 

 

 

[1] Maana ya Istawaa: Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah.  

Share