Mazungumzo Na Shaytwaan
Sheikh 'Aidh Al-Qarniy
Imefasiriwa na WWW.ALHIDAAYA.COM
Nilizungumza na shaytwaan aliyewekwa mbali na Rehma za Allah katika usiku wa
Nilimwambia: Ninaogopa kupitwa na faradhi.
Akaniambia: Wakati ni mrefu na mpana.
Nikamwambia: Ninahofia kuikosa Swalah ya jamaa.
Akaniambia: Usiifanyie mikazo nafsi yako katika ibada.
KWA HIYO SIKUAMKA HADI JUA LILIPOCHOMOZA.
Akaninong’oneza: Usisikitikie yaliyokupita, kwani siku nzima ni nyakati.
NILIKAA
Nikamwambia: Umenishughulisha na mengine nikaacha du'aa.
Akaniambia: Achana nayo sasa, utafanya jioni.
NIKAWEKA NIA
Akaniambia: Starehe na ujana wako.
Nikamwambia: Naogopa mauti.
Akaniambia: Umri wako bado ni mrefu.
NIKAKAA
Akaniambia: Jiburudishe kwa nyimbo (Muziki).
Nikamwambia: Nyimbo (Muziki) ni haramu.
Akasema: Baadhi ya maulamaa wana maoni tofauti kuhusu
Nikamwambia: Ninazo Hadiyth zinazoharamisha katika kitabu.
Akasema: Hadithi zote hizo ni dhaifu.
KISHA AKAPITA MSICHANA MZURI
Akaniuliza: Unasemaji kuhusu kuangalia?
Nikamjibu: Kuna hatari.
Akasema: Fikiria katika uzuri, kwani kutafakari ni halali.
NIKAENDA KATIKA NYUMBA KONGWE, NAYE AKANISIMAMISHA NJIANI.
Akaniuliza: Nini sababu ya safari hii?
Nikamjibu: Nakwenda kufanya ‘Umrah.
Akaniambia: Vipi unajitia hatarini kwa sababu ya ‘Umrah hii wakati ambapo milango ya kheri ni mingi, na mambo mema yamejazana chungu mbovu?!
Nikamjibu: Ni lazima tuzitengeneze vyema hali.
Akasema: Mtu haingii peponi kwa vitendo vyake.
NIKAENDA KUTOA NASAHA KWA WATU.
Akaniambia: Usije ukajifedhehesha bure.
Nikamwambia: Hili lina manufaa kwa waja.
Akaniambia: Ninakuhofia kupata umashuhuri, kwani umashuhuri ndio hasa kiini cha ufisadi.
Nikamuuliza: Una rai gani juu ya baadhi ya watu?
Akasema: Nitakujibu kwa walio mashuhuri na watu wa kawaida.
Nikamuuliza: Unasemaji kuhusu Ahmad bin Hanbali?
Akajibu: Ameniua kwa neno
Nikamuuliza: Na Ibn Taymiyah je?
Akajibu: Mapigo yake yanakisumbua kichwa changu nyakati zote.
Nikamuuliza: Na Al Bukhaariy?
Akajibu: Ameichoma nyumba yangu kwa kitabu chake.
Nikamuuliza: Unasemaji kuhusu Hajjaaj?
Akajibu: Laiti katika watu wangelikuwepo mfano wa Hajjaaj watu elfu moja. Sera yake imetufurahisha na aliyoyafanya kwa watu ndio dawa kwetu.
Nikamuuliza: Na Firauni je?
Akajibu: Sisi tunamuunga mkono na tunamsaidia kwa nguvu zetu zote.
Nikamuuliza: Unasemaji kuhusu Swalaah-Ud-Diyn Shujaa wa Hatin?
Akajibu: Achana na huyo! Alitugaragaza topeni.
Nikamuuliza: Na Muhammad bin Abdul Wahhaab je?
Akajibu: Kwa ulinganio wake, amewasha moto kifuani mwangu na amenichoma kwa vimondo vyote.
Nikamuuliza: Na Abu Jahl naye?
Akajibu: Sisi ni nduguze na jamaa zake.
Nikamuuliza: Na Abu Lahab, je?
Akajibu: Sisi tuko naye popote aendapo.
Nikamuuliza: Na Lenin je?
Akajibu: Tumemfunga motoni pamoja na Stalin.
Nikamuuliza: Unasemaji kuhusu majarida ya habari za ngono na picha za kinyume na maadili?
Akajibu: Hayo kwetu sisi ndio sheria.
Nikamuuliza: Na chaneli za satelaiti kwenye runinga (TV)?
Akajibu: Tunawafanya watu kuwa
Nikamuuliza: Na migahawa je?
Akajibu: Tunamkaribisha hapo kila yule asiyekuwa na la maana la kufanya.
Nikamuuliza: Nini nyiradi zenu?
Akajibu: Nyimbo.
Nikamuuliza: Nini amali zenu?
Akajibu: Ni kuwa na matarajio mema.
Nikamuuliza: Mnasemaje kuhusu masoko?
Akajibu: Tumejua kwamba huko kuna mtangamano mbaya na huko ndiko marafiki hukutana.
Nikamuuliza: Unasemaji kuhusu chama cha kijamaa cha Baath?
Akajibu: Nimegawana nacho
Nikamuuliza: Ni vipi wewe unawapoteza watu?
Akajibu: Kwa kuwachochea matamanio, kuwatilisha shakashaka, vipumbazisho, kuwapa matumaini mazuri na kwa nyimbo.
Nikamuuliza: Ni vipi unawapoteza wanawake?
Akajibu: Kwa kujikwatua, kuvaa mavazi ya utovu wa heshima, kuacha maamrisho na kufanya waliyokatazwa.
Nikamuuliza: Ni vipi unawapoteza maulamaa?
Akajibu: Kwa kupenda kuonekana, kujiona mimi ndio kiboko na husuda iliyojaa vifuani mwao.
Nikamuuliza: Ni vipi unawapoteza watu wa kawaida?
Akajibu: Kwa kusengenya, kufitini, na kuwaingiza katika mazungumzo machafu yasiyokuwa na faida yoyote.
Nikamuuliza: Ni vipi unawapoteza wafanyabiashara?
Akajibu: Kwa kufanya riba katika mikataba
Nikamuuliza: Ni vipi unawapoteza vijana?
Akajibu: Kwa kutongoza wasichana, kuwa na ashiki kali, mapenzi haramu, kuzidharau na kuzikejeli hukumu za dini na kufanya mambo ya haramu.
Nikamuuliza: Unasemaji kuhusu Dola ya Kiyahudi (
Akajibu: Tahadhari kusengenya, kwani huo ni msiba, na
Nikamuuliza: Unasemaji kuhusu Abu Nuwas?
Akajibu: Huyo ni mtu wetu. Mashairi yake ndio katiba yetu.
Nikamuuliza: Na watu wa kisasa je?
Akajibu: Hao wamechukua elimu
Nikamuuliza: Unasemaje kuhusu kuitenga dini na siasa”?
Akajibu: Imani yetu ndiyo hiyo, nao ni watu wa uongo na matarajio.
Atakayewaita, basi bila shaka ameniita mimi.
Nikamuuliza: Unasemaje kuhusu
Akajibu: Khatibu wangu yuko huko akipiga blaa blaa, na jeshi langu kambi yake iko huko na hiyo ndiyo nchi yangu.
Nikamuuliza: Unasemaje kuhusu walinganiaji wa dini?
Akajibu: Wamenitesa, wamenikong’ota na wamenizeesha. Wanavibomoa nilivyovijenga, ninapoimba wao husoma na wanajilinda nami wakati ninapokuja.
Nikamuuliza: Unasemaje kuhusu magazeti?
Akajibu: Tunawapotezea kwayo wakati watu waliojisahau, tunaumaliza kwayo umri wa watu wa anasa na tunachukua kwayo
Nikamuuliza: Unasemaje kuhusu B.B.C, (C.N.N)?
Akajibu: Kupitia kwayo, tunatia sumu katika vinono, tunawapiga vita Waarabu na wasio Waarabu na tunamsifia mdhulumiwa na dhalimu.
Nikamuuliza: Ulifanya nini kwa kunguru?
Akajibu: Nilimsalitishia kwa nduguye akamuua na akamzika katika mchanga mpaka akatoweka.
Nikamuuliza: Ulimwambia nini Firauni?
Akasema: Nilimwambia: Ewe mtukufu wa kasri! Sema: Je, si wangu mimi ufalme wa Misri?! Basi ushindi utakujia.
Nikamuuliza: Ulimwambia nini mnywa pombe?
Akasema: Nilimwambia: Kunywa zabibu, kwani inaondosha mawazo, inaondosha ghamu, na mlango wa toba unajulikana.
Nikamuuliza: Ni kitu gani kinachokuua?
Akajibu: Ni Ayat Al Kursiy. Kwa aya hiyo, pumzi zangu zinanibana, kifungo changu kinarefuka na ninakua katika balaa.
Nikamuuliza: Ni mtu gani unayempenda zaidi?
Akajibu: Waimbaji, washairi wapotevu, wafanyaji maasi na kila mbaya aliyefitinika.
Nikamuuliza: Ni mtu gani unayemchukia zaidi?
Akajibu: Ni watu walioshikamana na misikiti, kila anayerukuu na kusujudu, kila aliyeipa dunia mgongo na kufanya ibada na kila mpiganaji jihadi.
Nikamwambia: Najilinda kwa Mwenyezi Mungu nawe. Akapotea na kutoweka na kuwa
Ndugu mpenzi! Hapa ndipo yalipoishia mazungumzo kati ya shaytwaan na mwanadamu. Lakini kazi yake bado haijamalizika, kwani kila mmoja wetu ana shaytwaan wake. Lakini je, mmoja wetu anaweza kumshinda?
Jibu la swali hili ni: NDIYO. Kwa uwezo wa Allaah سبحانه وتعالى na Msaada Wake pamoja na kufanya tawbah ya kikwelikweli.
Mazungumzo yetu bado yanaendelea mpaka mwisho wa maisha yetu na hadi kiyama madhali ni ya kuutumikia Uislamu.
Hii ndio dini yetu. Hii ndio 'aqiydah yetu. Naapa kwa Mwenyezi Mungu, kisha naapa, kisha naapa. Sisi hatukuiacha na wala hatutoiacha dini yetu hata sekunde moja. Hatutoiacha hata
Hii ndiyo Dini ya Mwenyezi Mungu na nyinyi ni Waja wa Mwenyezi Mungu. Basi yeyote atakayeweza kufanya lolote katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuuhudumia Uislamu, basi anaweza kwa uchache kuusambaza ujumbe huu kwa rafiki zake.
Tunatumai ujumbe huu umetoa faida kwa Uwezo wa Allah.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


