|
|
User loginPokea Makala |
FeatureKikokotoo (Calculator) Cha ZakkahZingatio La WikiMgeni BoraKwa hakika tumejiwa na mgeni bora kuliko wote. Hayupo kwa muda mrefu na siku chache tu atatuacha. Huyu si mwengine bali ni mwezi mtukufu wa Ramadhaan. Kama tulivyoanza kwa hisabu ya Ramadhaan ya kwanza ndivyo tutakavyofika hadi Ramadhaan ya 29 au 30 insha Allaah. |
|
|
Assalaam alaikum
Assalaam alaikum warahmatullaah taala wabarakatuh,
waama katika habari nilizokuwa nikizitafuta muda mrefu katika maisha ni ishiyo ni haya,
nina uhakika haswa majibu ya maswali mbali mbali ambayo huwa napambana nayo kwa namna moja au nyingine yamepata majibu, HONGERA saana kwa kufanya kazi nzuri ya kuuelimisha umma huu kwa njia hii ya mtandao,naamini kwa muumin haswa mpenda kuufuatilia uislam na kupenda kuufahamu vilivyo, hatoshindwa kukaa japo dakika kumi kupata mawili matatu kila siku, Inshaallaah mwenyezi mungu awapeni nguvu muendelee kupekua kila mlionalo litatutoa gizani na kuweza kutupeperushia, nasi tutajitahidi kuyafuatilia na pia kuwafikishia wenzetu ambao hawakupata bahati ya kuyaona ndani ya mtandao
Wabillah tawfiq.
Assalaamu
Assalaamu 'alaykum
Tunamshukuru Allaah Subhaanahu wa Ta'ala kujua kwamba unafaidika na tovuti yenu hii na tunakushukuru kwa maoni yako pamoja na du'aa zako nzuri. Allaah Akupe nawe kila la kheri za dunia na mafanikio mema ya Akhera.
Ndugu Zako
AL HIDAAYA
Assalaamu alaikum, Nimepata
Assalaamu alaikum,
Nimepata fursa ya kuweza kusoma jarida lenu la Al-Hidaaya na nimevutiwa mno na makala tofauti yenye kuleta manufaa katika mujtamaa wetu wa ki-islamu.
Natoa shukurani zangu za dhati kwa wale walojitahidi kuunda chama hiki.Allah s.w. awajaze kila la kheri duniani na kesho akhera insha-Allah katika kuendeleza dini yetu hii ya haki Amin.
Jazakumullah alfu kheir.
Wardah
Mombasa, Kenya
Wa 'alaykumus-salaam wa
Wa 'alaykumus-salaam wa RahmatuLLahi wa Barakaatuh,
Tunamshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa Neema Zake nying. Shukurani pia kwako wewe ndugu yetu kwa maoni na du'aa zako nzuri ambazo ndizo zinazotutia nguvu zaidi na kutuwezesha kutekeleza hizi kazi. Kila mnaponufaika na kupata Alhidaaya (uongofu) ndipo lengo la hii da'awa linafikia. AlhamduliLLah.
Hatuna tunaloliomba ila mzidi kutuombea, Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atufanyie wepesi kuzitekeleza hizi kazi na Atutaqabalie sote.
Ndugu zako
AL HIDAAYA