Skip navigation.
Home kabah

Mukhtasari Wa 'Aqiydah Swahiyh Ya Muislamu - 1

SUALI

JAWABU

DALILI KUTOKA QUR'AAN

DALILI KUTOKA HADITHI 

1- Kwa nini Allah Katuumba?

Katuumba Ili tumuabudu na tusimshirikishe Naye kwa chochote.

 (وماخلقت الجن والإنس إلا ليعبدون)   

Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi

(Adhaariyaat 56)

 ) حق الله على العباد أن يعبدوه ولا يشركوا به شيئا (

Haki ya Allah kutoka kwa mja wake  (mja anapaswa kumfanyia) ni kumuabudu bila ya kumshirikisha

2- Jinsi gani tumuabudu Allaah سبحانه وتعالى

Kama Alivyotuamrisha Allah na Mtume صلى الله عليه وسلم  kwa ikhlaas

 (وما امروا إلا ليعبدوا الله مخلصين له الدين)  

Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini,

(Al-Bayyinah 5)

 (من عمل عملا ليس عليه أمرنا

 فهو رد )

Atakayefanya kitendo kisichokuwa chetu (kisicho katika  Dini) kitarudishwa (hakitakubaliwa)

3- Je, tumuabudu Allaah سبحانه وتعالى kwa kumuogopa (adhabu Yake) na kutumaini (pepo Yake)?

Ndio tunamuabudu kwa kumukhofu na kuwa na matumaini

(وأدعوه خوفا وطمعا  (أي خوفا من ناره وطمعا في جنته   

Na muombeni kwa kuogopa na kwa kutumai. (kukhofu moto Wake na kutumaini pepo Yake)

(A'araf 56 )

 ( اسأل الله الجنة وأعوذ به

من النار )

Namuomba Allah Pepo na najikinga Kwake na moto

4- Nini Ihsaan katika ibada?

Kujichunga (kuwa makini) katika ibada kwa ajili yake  Allaah سبحانه وتعالى Pekee.

  (ان الله كان عليكم رقيبا)  النساء

 (الذي يراك حين تقوم) الشعراء

Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni. (An-Nisaa 1)

Ambaye anakuona unapo simama,(Ash-Shu'araa 218) 

(الإحسان أن تعبد الله كانك تراه فأن لم تكن تراه فأنه يراك )

Ihsaan ni kumuabudu Allaah سبحانه وتعالى kama vile unamuona, na kama humuoni basi Yeye Anakuona

5- Kwa nini Allaah سبحانه وتعالى Ametuma Wajumbe (Mitume)?

Kutuita katika kumuabudu na kuepukana na kumshirikisha

 (ولقد بعثنا في كل أمة رسولا أن اعبدوا الله وأجتنبوا الطاغوت)

Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani.(An-Nahl 36)

) والانبياء إخوة ودينهم واحد(

Na Manabii ni ndugu na dini yao ni moja 

6- Nini Tawhiid ya Ilaah?

Kumfanyia Yeye Pekee ibada, dua, nadhiri na  Hukumu.

(فأعلم أنه لا إلاه إلا الله)

Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, (Muhammad 19)

(فليكن أول ما تدعوهم اليه شهادة

 أن لا إله إلا الله)

Jambo la kwanza liwe mnapowalingania wao Kwake ni "Kuthibitisha kwamba hakuna mola apasaye kuabudiwa isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى)

7- Nini maana ya Laa Ilaaha illa Allaah?

Hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى.

 (ذلك بأن الله هو الحق وأن مايدعون من دونه الباطل )

Hivi ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ndiye wa kweli, na hakika wanacho kiomba ni cha uwongo (Luqman 30)

(من قال لا إله إلا الله  وكفر بما يعبد من دون الله حرم ماله ودمه )

Atakayesema 'Laa ilaaha illa Allah  na akawapinga wanaoabudiwa wasio Allaah سبحانه وتعالى  italindwa (itakuwa haramu mtu kuchukua) mali yake na damu yake (uhai(.

8- Nini maana ya Tawhiid katika sifa za Allaah سبحانه وتعالى

Kuthibitisha alivyojisifu Mwenyewe Allaah سبحانه وتعالى  au alivyosifiwa na Mtume wake.

 ) ليس كمثله شيء وهو السميع البصير)

Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona  (As-Shura 11) 

 (ينزل ربنا تبارك وتعالى في كل ليلة إلى السماء الدنيا)

Mola wetu huteremka  kila usiku katika mbingu ya dunia

9- Nini faida ya Tawhiid kwa Muislamu?

Kupata Hidaaya duniani na kuwa katika amani  akhera

 (الذين أمنوا ولم يلبسوا إيمانهم بظلم أولئك لهم الأمن وهم مهتدون )

Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma - hao ndio watakao pata amani na wao ndio walio ongoka (An-'Aam 82)

( حق العباد على الله أن لايعذب من لا يشرك به شيئ )

Haki ya mja kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى (Mwenyeezi Mungu anayomfanyia) kuwa Hamuadhibu yule asiyemshirikisha Yeye na chochote.

10- Je, Allaah سبحانه وتعالى yuko wapi?

Allaah سبحانه وتعالى yuko mbinguni juu ya 'Arshi

 (الرحمن على العرش أستوى)

Ar-Rahmani, Mwingi wa Rehema, aliye tawala juu ya Kiti cha Enzi (Twaha  5)

) إن الله كتب كتاباً إن رحمتي سبقت غضبي فهو مكتوب عنه فوق العرش )

Allaah سبحانه وتعالى Ameandika maandishi kwamba Rahma yangu imeshinda  ghadhabu  yangu, nayo yameandikwa  kumhusu Yeye juu ya 'Arshi

11- Je, Allaah سبحانه وتعالى yuko na sisi kwa dhati yake au kwa elimu yake?

Allaah سبحانه وتعالى yuko na sisi kwa elimu yake anatuona na anatusikia

( قال لا تخافا إنني معكما أسمع وأرى)  

Akasema: Msiogope! Hakika Mimi ni pamoja nanyi. Nasikia na ninaona (Twaha 46).

(إنكم تدعون سميعا قريبا وهو معكم)

Hakika nyinyi mnamuomba Mwenye kusikia, Aliye karibu na Yeye yuko pamoja nanyi.

12- Dhambi gani ni kubwa kabisa?

Dhambi kubwa kabisa ni kumshirikisha Allaah سبحانه وتعالى

(يابني لاتشرك بالله إن الشرك لظلم عظيم)

Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa. (Luqman 13)

(سئل أي الذنب أعظم؟قال أن تدعو لله ندا وهو خلقك )

Aliulizwa dhambi gani kubwa? Akasema ni kumuomba Allaah pamoja na mshirika Na hali Yeye ndiye Aliyekuumba.    

13- Shirki gani iliyokuwa kubwa?

Kufanya ibada kwa kumuelekea asiye Allaah سبحانه وتعالى kama duaa

 )قل إنما أدعو ربي ولا أشرك به أحدا(

Sema: Hakika mimi namwomba Mola wangu Mlezi, wala simshirikishi Yeye na yeyote

(Al-Jinn 20)

(أكبر الكبائر الإشراك بالله)

Dhambi kubwa ni kumshirikisha Allaah سبحانه وتعالى

14- Ni yapi madhara ya kumshirikisha Allaah سبحانه وتعالى

Kumshirikisha Allaah سبحانه وتعالى husababisha kudumu milele motoni 

(إنه من يشرك بالله فقد حرم الله عليه الجنة وماواه النار)

Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni (AL-Maida 72)

(من مات يشرك بالله شيئا دخل النار)

Atakayekufa na huku amemshirikisha Allaah سبحانه وتعالى  kwa chochote, ataingia motoni.

15- Je, Kitendo chema kinafaa kikiwa kimemshirikisha Allaah سبحانه وتعالى

Hakifai kitu kitendo ambacho kina kumshirikisha Allaah سبحانه وتعالى

(ولو أشركوا لحبط عنهم ما كانوا يعلمون)

Na lau wangeli mshirikisha yangeli waharibikia waliyo kuwa wakiyatenda (An-'Aam 88)

(من عمل عملا أشرك فيه معي غيري تركته وشركه)

Atakayefanya kitendo na huku kanishirikisha Mimi kwa kitendo hicho na mwengine, namwacha yeye na shirki yake.

16- Je, Shirki ipo kwa Waislamu?

Ndio, ni masikitiko kuwa  ipo tena nyingi

(وما يؤمن أكثرهم بالله إلا وهم مشركون)

Na wengi katika wao hawamuamini Mwenyezi Mungu pasina kuwa ni washirikina

(Yusuf 106)

(لاتقوم الساعة حتى تلحق قبائل من أمتي بالمشركين وحتى تعبد الأوثان )  

Qiyama hakitasimama mpaka kutafika wakati watu wa baadhi ya makabila katika umma wangu wataungana na washirikina na hadi watakapoabudu asiye Allah!

17- Nini hukumu ya kumuomba asiye Allaah سبحانه وتعالى kama Mawalii 'Vipenzi vyake? 

Kuwaomba ‘Mawalii’ ni shirki yenye kumpeleka mtu motoni.

(فلا تدع مع الله الها آخر فتكون من المعذبين) 

Basi usimwombe mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa

(As-Shu'araa  213)

(من مات وهو يدعو من دون الله ندا دخل النار)

Atakayekufa katika hali kumuomba asiye Allaah سبحانه وتعالى ataingia motoni.

18- Je, Kuomba dua ni ibada ya Allaah سبحانه وتعالى

Ndio, kuomba duaa ni ibada ya Allaah سبحانه وتعالى

(وقال ربكم أدعوني استجب لكم)

Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikien (Ghaafir 60)

(الدعاء هو العبادة )

 

Dua ni ibada

19- Je, waliokufa wanasikia dua?

Waliokufa hawasikii dua

(إنك لا تسمع الموتى )

 (وما انت بمسمع من في القبور(

Kwa hakika wewe huwezi kuwafanya maiti wasikie,(An-Naml  80)

Wala wewe si wa kuwasikilizisha walio makaburini. (Fatir 22)

(إن لله ملائكة سياحين في الأرض يبلغوني عن أمتي السلام)

Hakika Allaah سبحانه وتعالى Anao malaika wanaozunguka katika ardhi  wakinifikishia salamu kotoka kwa umma wangu.

20- Je, nafaa tuwaombe maiti na wasiopo watuokoe?

Hatuwaombi wao watuokoe bali tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى

( اذ تستغيثون ربكم فاستجاب لكم)

Mlipo kuwa mkimuomba msaada Mola wenu Mlezi, naye akakujibuni (Al-A'araaf 9)

(كان إذا أصابه هم أو غم قال: ياحي ياقيوم برحمتك أستغيث)

Alikuwa akifikwa na hamu au majonzi anasema 'Ewe uliye na uhai wa maisha, uliyesimamia kila jambo, kwa rahma zako nakuomba uniokoe.

21- Je, Inafaa  kuomba msaada pasipo na Allaah?

Haifai kuomba msaada kwa mwengine asiye Allaah سبحانه وتعالى

(إياك نعبد وإياك نستعين)

Wewe tu ndiye tunayekuabudu na Wewe tu ndiye tunayekuomba msaada (Al-Fatiha 5)

(إذا سألت فأسال الله وإذا أستعنت فأستعن بالله )

Unapoomba muombe Allaah na unapotaka msaada taka msaada kwa Allaah سبحانه وتعالى

22- Je, Inafaa kuomba msaada kwa walio hai?

Ndio kwa kadiri wanavyoweza

(وتعاونوا عل البر والتقوى ولا تعاونوا على الإثم والعدوان)

Na msaidiane  katika wema na ucha Mungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui

(Al-Maida 2)

(والله في عون العبد ما دام العبد في عون أخيه )

Allaah سبحانه وتعالى yuko katika kumsaidia mja wake vile anavyoendelea  kumsaidia mwenzake.

23- Je, Inafaa  kuweka nadhiri pasipo na Allaah سبحانه وتعالى?

Haipasi kuweka nadhiri isipokuwa kwa sababu ya Allaah سبحانه وتعالى.

(رب إني نذرت لك ما في بطني محررا

 فتقبل مني )

Mola wangu Mlezi! Nimekuwekea nadhiri kilichomo tumboni mwangu kuwa wakfu; basi nikubalie.

(Al-Imraan 35)

 (من نذر أن يطيع الله فليطعه ومن نذر أين يعصيه فلا يعصه )

Anayeweka nadhiri kumtii Allaah سبحانه وتعالى basi amtii, na aliyeweka nadhiri kumuasi Allaah سبحانه وتعالى basi asimuasi.

24- Je, Inafaa  kuchinja bila kumkusudia Allaah سبحانه وتعالى?

Haifai kuchinja kwa malengo yasiyo ya Allaah سبحانه وتعالى  kwa sababu ni shirki kubwa.

(فصل لربك وأنحر)

Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi (Al-Kauthar 2)

 (لعن الله من ذبح لغير الله(  

Allaah سبحانه وتعالى humlaani anayechinja bila ya sababu ya Allaah سبحانه وتعالى.

25- Je, Inafaa kutufu makaburi?

Haifai kuzunguka makaburi, bali kuzunguka (kutufu) Kaaba pekee.

(وليطوفوا بالبيت العتيق )

na waizunguke Nyumba ya Kale

(Al-Hajj 29)

(من طاف بالبيت سبعا وصلى ركعتين كان كعتق رقبة )

Atakayezunguka Kaaba mara saba kisha akaswali rakaa mbili ni kama mfano kamwacha huru mtumwa mmoja

26- Je, Inafaa kuswali na kaburi liko mbele yako?

Haifai kuswali kulielekea kaburi.

(فول وجهك شطر المسجد الحرام  (

Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu

 (Al-Baqara 144)

(لاتجلسوا على القبور ولا تصلوا إليها)

Msikalie makaburi wala msiswali kuyaelekea.