06-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Miongoni Mwa Hayaa Zake Alimsitahi Allaah Alipofaradhisha Swalaah Tano

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

06-Miongoni Mwa Hayaa Zake Alimsitahi Allaah Alipofaradhisha  Swalaah Tano 

www.alhidaaya.com

 

 

Pindi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipopandishwa mbinguni siku ya Israa Wal-Mi’raaj ambako ndipo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alimfaradhishia nguzo ya Swalaah kwa Waislamu, na wakati alipopewa amri hiyo ya Swalaah akiwa anarejea, Nabiy Muwsaa ('Alayhis-Salaam) akamtaka arudi kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ili zipunguzwe hizo Swalaah tano, lakini  Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimstahi Rabb wake (‘Azza wa Jalla). Hadiyth ifuatayo imethibitisha: 

   

 أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ وَابْنُ حَزْمٍ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((فَرَضَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ عَلَى أُمَّتِي خَمْسِينَ صَلاَةً فَرَجَعْتُ بِذَلِكَ حَتَّى أَمُرَّ بِمُوسَى عَلَيْهِ السَّلاَمُ فَقَالَ: مَا فَرَضَ رَبُّكَ عَلَى أُمَّتِكَ؟ قُلْتُ فَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسِينَ صَلاَةً‏.‏ قَالَ لِي مُوسَى: فَرَاجِعْ رَبَّكَ عَزَّ وَجَلَّ فَإِنَّ أُمَّتَكَ لاَ تُطِيقُ ذَلِكَ‏.‏ فَرَاجَعْتُ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ فَوَضَعَ شَطْرَهَا فَرَجَعْتُ إِلَى مُوسَى فَأَخْبَرْتُهُ فَقَالَ: رَاجِعْ رَبَّكَ فَإِنَّ أُمَّتَكَ لاَ تُطِيقُ ذَلِكَ.‏ فَرَاجَعْتُ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ فَقَالَ: هِيَ خَمْسٌ وَهِيَ خَمْسُونَ لاَ يُبَدَّلُ الْقَوْلُ لَدَىَّ‏.‏ فَرَجَعْتُ إِلَى مُوسَى فَقَالَ رَاجِعْ رَبَّكَ فَقُلْتُ قَدِ اسْتَحْيَيْتُ مِنْ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik na Ibn Hazm kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  ((Allaah ('Azza wa Jalla) Alifaradhisha Swalaah khamsini kwa Ummah wangu, nikazikubali na nikarejea hadi nilipopita kwa Muwsaa ('Alayhis-Salaam) ambaye alisema:  Je, Rabb wako Amekufaradhishia nini kwa Ummah wako? Nikasema: Amewafaridhisha Swalaah khamsini. Muwsaa akaniambia: Rudi kwa Rabb wako ‘Azza wa Jalla kwani ummah wako hawatoziweza hizo.  Nikamrejea Rabb wangu Allaah ('Azza wa Jalla)  Naye Akanipunguzia idadi zake, nikarudi kwa Muwsaa nikamwelezea akasema: Rudi kwa Rabb wako  kwani ummah wako hawatoziweza hizo. Nikarudi kwa Rabb wangu Allaah ('Azza wa Jalla) Akasema: Hizo (Swalaah) ni tano lakini ni thawabu khamisini na Kauli Yangu haibadiliki.  Nikarudi kwa Muwsa akasema: Rudi kwa Rabb wako. Nikasema: Hakika namstahi Rabb wangu Allaah 'Azza wa Jalla)) [A-Nasaaiy, Ibn Maajah na katika riwaayah ndefu ya Al-Bukhaariy]

 

 

Share