121-Hiswnul-Muslim: Takbiyr Katika Kurusha Kijiwe Kwenye Jamarah

Hiswnul-Muslim

121-Takbiyr Katika Kurusha Kijiwe Kwenye Jamarah

www.alhidaaya.com

 

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

[239]

 

يُكَبِّرُ كُلَّمَا رَمَى بِحَصَاةٍ عِنْدَ الْجِمار الثَّلاث، ثُمَّ يَتَقَدَّم، وَيَقِفُ يَدْعُو مُسْتَقْبِلَ الْقِبْلَةِ، رَافِعًا يَدَيْهِ بَعْدَ الْجَمرْةِ الأُولَى والثَّانِيَة، أمَّا جَمْرَةُ الْعَقَبَة فَيَرْمِيهَا وَيُكَبِّرُ عِنْدَ كُلِّ حَصَاةٍ وَيَنْصَرِفُ وَلا يَقِفُ عِنْدَهَا

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) Alikuwa  kila aliporusha kijiwe katika Jamarah (nguzo) tatu alisema:

 

أَللّهُ أَكْبَرُ

Allaahu Akbar

 

Allaah ni Mkubwa

 

...kisha akisogea na kusimama akielekea Qiblah akiomba du’aa huku akiinua mikono yake. Akifanya hivyo aliporusha vijiwe katika Jamarah ya kwanza na ya pili. Ama Jamarah ya tatu (Al-’Aqabah) alirusha na akamtukuza Allaah (Allaahu Akbar) kwa kila kijiwe kisha alikuwa hasimami bali akimaliza anaondoka”[1]

 

 

 

 

[1]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنهما)  - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (3/583-584), na taz tamshi yake huko. Na Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (3/581) na ameipokea Muslim pia [1296] Hadiyth ya ibn Mas-‘uwd (رضي الله عنه).

 

 

Share