27-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Atakuwa Wa Kwanza Na Ummah Wake Kuvuka Swiraatw

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

27-Atakuwa Wa Kwanza Na Ummah Wake Kuvuka Swiraatw

www.alhidaaya.com

 

Kutoka katika Hadiyth ndefu kabisa iliyothibiti kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Ummah wake tutakuwa wa kwanza kabisa kuvuka Asw-Swiraatw:

 

عَنْ عَطَاءِ بْنِ يَزِيدَ اللَّيْثِيِّ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ النَّاسَ، قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ هَلْ نَرَى رَبَّنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ هَلْ تُضَارُّونَ فِي الْقَمَرِ لَيْلَةَ الْبَدْرِ ‏"‏‏.‏ قَالُوا لاَ يَا رَسُولَ اللَّهِ‏.‏ قَالَ ‏"‏ فَهَلْ تُضَارُّونَ فِي الشَّمْسِ لَيْسَ دُونَهَا سَحَابٌ ‏"‏‏.‏ قَالُوا لاَ يَا رَسُولَ اللَّهِ‏.‏ قَالَ ‏"‏ فَإِنَّكُمْ تَرَوْنَهُ كَذَلِكَ، يَجْمَعُ اللَّهُ النَّاسَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَيَقُولُ مَنْ كَانَ يَعْبُدُ شَيْئًا فَلْيَتَّبِعْهُ‏.‏ فَيَتْبَعُ مَنْ كَانَ يَعْبُدُ الشَّمْسَ الشَّمْسَ، وَيَتْبَعُ مَنْ كَانَ يَعْبُدُ الْقَمَرَ الْقَمَرَ، وَيَتْبَعُ مَنْ كَانَ يَعْبُدُ الطَّوَاغِيتَ الطَّوَاغِيتَ، وَتَبْقَى هَذِهِ الأُمَّةُ فِيهَا شَافِعُوهَا ـ أَوْ مُنَافِقُوهَا شَكَّ إِبْرَاهِيمُ ـ فَيَأْتِيهِمُ اللَّهُ فَيَقُولُ أَنَا رَبُّكُمْ‏.‏ فَيَقُولُونَ هَذَا مَكَانُنَا حَتَّى يَأْتِيَنَا رَبُّنَا فَإِذَا جَاءَنَا رَبُّنَا عَرَفْنَاهُ فَيَأْتِيهِمُ اللَّهُ فِي صُورَتِهِ الَّتِي يَعْرِفُونَ فَيَقُولُ أَنَا رَبُّكُمْ‏.‏ فَيَقُولُونَ أَنْتَ رَبُّنَا‏.‏ فَيَتْبَعُونَهُ وَيُضْرَبُ الصِّرَاطُ بَيْنَ ظَهْرَىْ جَهَنَّمَ، فَأَكُونُ أَنَا وَأُمَّتِي أَوَّلَ مَنْ يُجِيزُهَا، وَلاَ يَتَكَلَّمُ يَوْمَئِذٍ إِلاَّ الرُّسُلُ، وَدَعْوَى الرُّسُلِ يَوْمَئِذٍ اللَّهُمَّ سَلِّمْ سَلِّمْ‏.‏

 

Kutoka kwa ‘Atwaa’ bin Yaziyd Al-Laythiy kuwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Watu (yaani Maswahaba) walisema:  “Ee Rasuli wa Allaah! Je, tutamuona Rabb wetu Siku ya Qiyaama?” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akasema: ((Je, mna shida yoyote ya kuuona mwezi usiku ambao mwezi ni mpevu?)) Wakasema: “Hapana ee Rasuli wa Allaah.” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Je, mna shida ya kuliona jua siku isiyokuwa na mawingu?)) Wakasema: “Hapana  ee Rasuli wa Allaah.”  Akasema: ((Hakika nyinyi mtamuona, kama hivyo. Allaah Atawakusanya watu wote Siku ya Qiyaamah, Naye Atasema: “Yeyote aliyekuwa akiabudu kitu (duniani) akifuate hicho (kitu)”  Kwa hiyo, yule aliyekuwa akiabudu jua atalifuata jua; na yeyote aliyekuwa akiuabudu mwezi ataufuata mwezi; na yeyote aliyekuwa akiabudu twaghuti  atamfuata twaghuti. Na utabakia Ummah huu peke yake na watu wake wazuri na wanafiki miongoni mwao)). Allaah Atakuja kwao na kusema: “Mimi Ndiye Rabb wenu.” Wao (watu watamkanusha) kwa kusema: “Hii ni sehemu yetu, nasi tutaketi hapa mpaka atakapokuja Rabb wetu. Pindi Atakapokuja tutamjua.” Kwa hivyo, Allaah Atakuja kwao katika Surah Yake ambayo wataijua, Naye Atasema: “Mimi Ndiye Rabb wenu.” Watu watasema: “Wewe Ndiye Rabb wetu.” Nao (watu) watamfuata. Kisha Asw-Swiraatw (Njia) itawekwa juu ya Moto (wa Jahannam).. Mimi na Ummah wangu tutakuwa wa kwanza kuivuka na hakuna atakayezungumza Siku hiyo isipokuwa Rusuli. Na Du‘aa ya Rusuli Siku hiyo itakuwa:

اللَّهُمَّ سَلِّمْ سَلِّمْ

 

Allaahumma Sallim (Ee Allaah! Jaalia salama, Jaalia salama)) [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share