24-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! Vipi Kujiepusha Na Shirki

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

24-Vipi  Kujiepusha Na Shirki

 

Alhidaaya.com

 

Ndugu Muislamu! Hakika shirki ni dhulma kubwa mno! Kwa kumfanyia shirki Rabb wako Aliyekuumba, Ambaye unaishi katika ardhi Yake, Ambaye Anakuruzuku na Akakujaalia neema nyingi mno zisizohesabika, Ambaye Anakurehemu na Akakujaalia fadhila na neema za kila aina. 

 

Miongoni mwa neema Zake Allaah ('Azza wa Jalla) ni kukujaalia uhai mpaka hii leo uweze kutambua yanayomshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ili urudie kutubia Kwake kabla ya kufariki kwako. Basi hii ni fursa adhimu kwa kila aliyekuwa akimshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) atekeleze yafuatayo ambayo yatasaidia kumuepusha na shirki In Shaa Allaah:    

 

1. Tawbah ya kweli:

 

Rudi kwa Rabb wako kwa kutubia tawbah ya nasuha (kwelikweli) kama Anavyoamrisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّـهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّـهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ ۖ نُورُهُمْ يَسْعَىٰ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٨﴾

Enyi walioamini! Tubieni kwa Allaah tawbah ya nasuha (kwelikweli); asaa Rabb   wenu Akakufutieni maovu yenu, na Akakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito. Siku ambayo Allaah Hatomfedhehesha Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na wale walioamini pamoja naye. Nuru yao itatembea mbele yao na kuliani mwao, watasema: “Rabb wetu! Tutimizie Nuru yetu, na Tughufurie, hakika Wewe juu ya kila kitu ni Muweza. [At-Tahriym: 8]

 

Twabah ya nasuha ina masharti yafuatayo:

 

Share
Subscribe to Alhidaaya.com RSS