SWALI:
A/alaykum, mimi ni binti nilieolewa huku ulaya, nimejaaliwa mtoto mmoja, lakini ndoa yetu haina raha ndani yake, na tatizo kuu ni huyu mume wangu, tangu mimi kuja nchi hii amekua akiwasiliana na wasichana kwa njia ya simu (txt msgs) na hizo msg zimejaa mahaba ndani yake, nimeshamuuliza ni kina nani, nae husema ni rafiki ambao hawezi kuachana kuwasilana nao, jambo hili hunikera sana, kwani huona ni kinyume cha sharia, na pia humwambia kua ni haram kuwa na rafiki wa kike hasa ikiwa yupo kwenye ndoa, lakini huona mimi ni mpuuzi na huona mimi na mtaabisha hata imefikia wakati kuniambia mimi niende kwetu kwa maudhiko ya mara kwa mara, jee nifanye nini kwa sababu mimi nimetoa uaminifu kwake.
W/ alaykum
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati dada yetu kwa swali lako zuri. Hakika ni kuwa hili ni tatizo sugu katika jamii yetu ya Waislamu. Maswali kama ya matatizo ya kindoa yamekua yakikariri kila uchao. Wanandoa wamekua hawana raha katika ndoa zao mbali na kuwa tumearifiwa na Aliyetukuka kuwa ndoa ni rehema na mapenzi. Kukosekana kwa mapenzi na huruma baina ya wanandoa kunamaanisha kuwa sisi tuna matatizo makubwa hivyo kupata mitihani hiyo.
Tatizo linaanza katika malezi majumbani mwetu na kukosa kuchagua mke au mume aliyeshika Dini. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuelezea sifa za kuangalia wakati unaposa au kuposwa lakini mara nyingi huwa tunatazama sifa zilizokatazwa. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatueleza yafuatayo kuhusu kuposa: 'Mwanamke huolewa kwa moja kati ya sababu nne:
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amewausia wazazi: 'Anapokujieni mnayemridhia Dini na maadili yake muozesheni kwani mkitofanya hivyo kutakuwa na fitina katika ardhi na ufisadi mkubwa' (at-Tirmidhiy).
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuonya tena: 'Mwenye kumuoa mwanamke kwa ajili ya utukufu wake, Allaah Hamzidishii ila udhalilifu; na mwenye kumuoa kwa sababu ya mali Allaah Hamzidishii ila ufukara; na mwenye kumuoa kwa ajili ya nasaba yake, Allaah Hamzidishii ila unyonge; na mwenye kumuoa mwanamke hataki kwake ila kuinamisha macho yake, kuilinda tupu yake au kuunganisha kizazi, Allaah Atambarikia kwake na Atambariki (mwanamke) kwake' (atw-Twabaraaniy).
Huu ni mfumo mzuri wenye kuwasaidia wanandoa pamoja na familia zao na jamii kwa jumla ili kufanikisha zoezi hili. Kuacha mfumo huu ni kuhasirika hapa duniani na kesho Akhera.
Wazazi wanatakiwa watumie busara zao kumuelekeza binti
Kulingana na maelezo ya muulizaji inaonyesha
Kabla hatujakupatia nasaha zetu ni vyema kuangazia juu ya ibara yako uliyosema: 'Hata imefikia wakati kuniambia mimi niende kwetu kwa maudhiko ya mara kwa mara'. Hii ibara ina utata mkubwa kwani amali zote zinategemea nia ya mwenye kufanya. Je, kukuambia kwenda kwenu ni kuwa tayari amekupatia talaka au vipi? Ikiwa nia yake ni talaka itakuwa wewe si mke wake na kwa sababu baada ya kusema hayo amefanya nawe kitendo cha ndoa atakuwa amekurudia. Hautajapita wakati amekuambia tena bila kujali ile athari inayopatikana kwa maneno hayo.
Ama nasaha zetu kwako ni kuwa tunakuomba ufanye yafuatayo, huenda kwayo ukapata ufumbuzi wa tatizo
Katika kufikia upatanishi huu ni lazima uwe na subira na uvumilivu mkuu ili muweze kupata suluhisho. Hakika kufanya kwako huko hakutapotea bure bali utapata thawabu kubwa mbele ya Allaah Aliyetukuka.
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akupatie tawfiki na Aidumishe ndoa yenu na Amuondolee mumeo tatizo hili alilonalo.
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/60
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F2577&title=Mume%20Anawasiliana%20Na%20Wanawake%20Kwa%20Maandishi%20Ya%20Mapenzi%20Kwa%20Njia%20Ya%20Simu%20Ya%20Mkononi%20%E2%80%93%20Nikimkataza%20Ananiambia%20Niende%20Kwetu%20