SWALI:
Muda wa kunyonyesha ni miaka 2 nijuavo jee ukipitisha ikawa umenyonyesha mpaka miaka 2 na nusu inakuaje?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kunyonyesha mtoto. Hakika ya muda ni
“Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anayetaka kutimiza kunyonyesha” (2: 233).
Kwa mujibu wa Aayah hii tunafahamishwa kuwa mama anaweza kumnyonyesha mtoto wake mpaka miaka miwili.
Sasa kwa sababu moja au nyingine ikiwa mama amenyonyesha kwa zaidi ya miaka miwili itakuwaje. Jawabu kwa
Kwa mujibu wa athari (masimulizi kutoka kwa Maswahaba) hizi kunakuwa hakuna tatizo ikiwa mtoto amenyonya kwa zaidi ya miaka miwili.
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/59
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F2606&title=Kunyonyesha%20Kupindukia%20Mipaka%20ya%20Miaka%20Miwili%20Inafaa%3F