SWALI:
Asalam aleikum, kuweka tattoo imekubakiwa katika dini ya kislamu? swalah itakubaliwa? na
Assalam alykum. Mimi nimejichora tattoo mwilini. Sasa nimetambua kuwa ni dhambi, na kuitoa haiwezekani tena. Je, nifanyeje sasa na vipi sala zangu zitakubaliwa? Asanteni.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kujichora tattoo mwilini mwako. Tufahamu kuwa Uislamu ni Dini ambayo inakwenda sambamba na maumbile ya mwanadamu. Sheria inajua kuwa Muislamu
Ikiwa mtu amefanya dhambi bila ya kujua kiuhakika basi Allaah Aliyetukuka Anamsamehe. Na ikiwa amefanya dhambi kwa kujua lakini anataka kurudi kwa Allaah Aliyetukuka, Allaah Anamsamehe madhambi yake ikiwa atatimiza masharti yafuatayo:
Lau atatekeleza hayo masharti matatu basi atasamehewa madhambi aliyofanya kwani Allaah ni msamehevu
Kujichora tattoo ni haramu katika Uislamu, na inatakiwa mtu katika kutubia aondoe ovu. Ikiwa michoro haiwezi kuondoka kwa kuwa inapochorwa ni yenye kudumu daima dawamu, inayohitajiwa ni ile azma yake ya nguvu. Allaah Aliyetukuka Hatamuadhibu mtu kwa kushindwa huko baada ya kujaribu.
Swalaah atakazo swali katika hali hiyo zitakuwa ni zenye kukubaliwa baada ya muhawala wake huko na kweli kujirekebisha katika hali aliyokuwa nayo.
Na Allaah Anajua zaidi.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/101
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F4655&title=Tattoo%3A%20Kujichora%20Mwili%3B%20Swalaah%20Inakubaliwa%3F%20Afanyeje%20Baada%20ya%20Kutubu%20Nayo%20Haitoki%3F