SWALI:
assalam aleykum .kwanza kabisa ningependa kuwashukuruni.
suwala ni
na mimi hata kwenye tendo la ndoa tunafika kukaa mpaka miezi mitatu au zaid bila ya kuingiliana na yeye anatumia usiku mwingi kwenye internet na mimi nishamwambia sipendo mwendo wake huo lakini jibu lake ni kuwa yeye hawezi kuishi bila ya internet anaweza kuishi bila ya mimi lakini sio bila ya internet kwa hiyo mimi mwenyewe najiona mimi kwake yeye sina thamani kuliko ya hiyo internet je ndoa hii inakubalika shekhe?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa swali lako kuhusu mume kuthamini mtandao (internet) kuliko wewe.
Hakika hili ni tatizo sugu katika jamii yetu na huenda mtu akajiuliza ikiwa mume anathamini kitu kingine chochote kuliko mke ingekuwa bora kwake kutoingia katika ndoa.
Mambo ambayo unaweza kufanya ni
Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Mume Anakesha Katika Internet Hampi Mke Haki Yake - Mke Afanyeje? [2]
Twamuomba Allaah Aliyetukuka Akutoe ufumbuzi wa shida hiyo na muweze kuishi na mumeo kwa njia iliyo nzuri.
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/60
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/node/2343
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F5203&title=Mume%20Ana%20Hiari%20Kukaa%20Kwenye%20Mtandao%20Masaa%20Kila%20Siku%2C%20Lakini%20Inapita%20Miezi%20Na%20Hamtimizii%20Mkewe%20Haki%20Ya%20Tendo%20La%20Ndoa