Utengenezaji Wa Caramel Ya Sukari Na Maziwa ya Malai Whipping Cream
Vipimo
Sukari - 1 kikombe
Maji - ¼ kikombe
Maziwa ya malai (whipping cream) -½ kikombe
Siagi - 1 kijiko cha kulia
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika.
1-Weka sukari na maji katika sufuria kisha pika katika moto mdogo mdogo sana. Koroga usiachie mkono mpaka itoke mapovu
2-Ikianza kubadilika rangi ya brown epua. Rangi ya brown upendavyo ukipenda iwe light au ikoze zaidi lakini isiungue.
3-Epua,mimina maziwa ya malai mazito (thick creamy milk au whipping cream)koroga vizuri
4-Tia kidonge cha siagi koroga kidogo katika moto.
5-Epua ipoe
Vidokezo:
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/185
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7316&title=Utengenezaji%20Wa%20Caramel%20Ya%20Sukari%20Na%20Maziwa%20ya%20Malai%20Whipping%20Cream