Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب الثوب الأبيض ، وجواز الأحمر والأخضر
والأصفر والأسود ، وجوازه من قطن وكتان وشعر وصوف وغيرها إِلاَّ الحرير
01-Mlango Wa Kupendeza Kuvaa Nguo Nyeupe na Kujuzu Nyekundu, Kijani, Njano, Nyeusi na Kujuzu Nguo ya Pamba, Katani, Sufi na ya Manyoa na Nyinginezo Isipokuwa ya Hariri
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
يَا بَنِي آدَمَ قَدْ أَنزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا يُوَارِي سَوْآتِكُمْ وَرِيشًا ۖ وَلِبَاسُ التَّقْوَىٰ ذَٰلِكَ خَيْرٌ ﴿٢٦﴾
Enyi wana wa Aadam! Kwa yakini Tumekuteremshieni libasi (nguo) inayositiri tupu zenu na libasi ya mapambo. Na libasi ya taqwa ndiyo bora zaidi. Hizo ni katika Ishara za Allaah ili wapate kukumbuka. [Al-A'raaf: 26]
وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ الْجِبَالِ أَكْنَانًا وَجَعَلَ لَكُمْ سَرَابِيلَ تَقِيكُمُ الْحَرَّ وَسَرَابِيلَ تَقِيكُم بَأْسَكُمْ ۚ ﴿٨١﴾
Na Akakujaalieni katika majabali mahali pa kukimbilia na Amekujaalieni mavazi yanakukingeni na joto na mavazi (ya chuma) yanakukingeni katika vita vyenu. [An-Nahl: 81]
Hadiyth – 1
وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( الْبَسُوا مِنْ ثِيَابِكُمْ البَيَاضَ ؛ فَإنَّهَا مِنْ خَيْرِ ثِيَابِكُمْ ، وَكَفِّنُوا فِيهَا مَوْتَاكُمْ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Vaeni katika nguo zenu nyeupe, kwani hizo ni katika nguo zenu zilizo bora kabisa na pia muwakafini nazo maiti zenu." [Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 2
وعن سَمُرَة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( الْبَسُوا البَيَاضَ ؛ فَإنَّهَا أطْهَرُ وَأطْيَبُ ، وَكَفِّنُوا فِيهَا مَوْتَاكُمْ )) رواه النسائي والحاكم ، وقال : (( حديث صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Vaeni nguo nyeupe, kwani hizo ni safi na ni nzuri na wakafinini katika hizo wafu wenu." [An-Nasaai na Al-Haakim, na akasema ni Hadiyth Swahiyh]
Hadiyth – 3
وعن البراءِ رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَرْبُوعاً ، وَلَقَدْ رَأيْتُهُ في حُلَّةٍ حَمْرَاءَ مَا رَأيْتُ شَيْئاً قَطُّ أحْسَنَ مِنْهُ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Na amesema Al-Baraa' bin 'Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kati na kati (wa umbo, si mrefu wala si mfupi) na kwa hakika nilimuona katika vazi jekundu, sikuona kabisa kitu kizuri sana kuliko vazi hilo." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasai]
Hadiyth – 4
وعن أَبي جُحَيفَةَ وَهْب بن عبد الله رضي الله عنه ، قَالَ : رَأيتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم بِمكّةَ وَهُوَ بالأبْطَحِ في قُبَّةٍ لَهُ حَمْرَاءَ مِنْ أَدمِ ، فَخَرَجَ بِلاَلٌ بِوَضُوئِهِ ، فَمِنْ نَاضِحٍ وَنَائِلٍ ، فَخَرَجَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم وعليه حُلَّةٌ حَمْرَاءُ ، كَأنِّي أنْظُرُ إِلَى بَيَاضِ سَاقَيْهِ ، فَتَوَضّأ وَأذَّنَ بِلاَلٌ ، فَجَعَلْتُ أتَتَبَّعُ فَاهُ هاهُنَا وَهَاهُنَا ، يقولُ يَمِيناً وَشِمَالاً : حَيَّ عَلَى الصَّلاَةِ ، حَيَّ عَلَى الفَلاَحِ ، ثُمَّ رُكِزَتْ لَهُ عَنَزَةٌ ، فَتَقَدَّمَ فَصَلَّى يَمُرُّ بَيْنَ يَدَيْهِ الْكَلْبُ وَالْحِمَارُ لاَ يُمْنَعُ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Amesema Abu Juhayfah Wahb bin 'Abdillaah: Nilimuona Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika sehemu ya Abtwahi, karibu na Makkah akiwa katika hema la ngozi nyekundu. Bilaal alikuja na maji kidogo kwa ajili ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kushikia wudhuu. Baadhi walipata maji kidogo na wengine hawana kabisa na wengine walitosheka kupata umande wa kutoka kwa mikono ya wengine. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka akiwa amevaa joho jekundu kama mimi ninaangalia weupe wa miundi yake. Alishika wudhuu na Bilaal akaadhini. Niliendelea kuangalia harakati za uso wa Bilaal akigeuka kuliani na kushotoni huku akisema: "Njooni katika Swalaah, njooni katika kufaulu." Kisha mkuki mdogo uliwekwa mbele na kuswalisha. Alipokuwa anaswalisha mbwa na punda walipita mbele yake na hawakuwa ni wenye kukatazwa. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أَبي رمْثَة رفَاعَةَ التَّيْمِيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : رأيتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم وعليه ثوبانِ أخْضَرَان . رواه أَبُو داود والترمذي بإسناد صحيح .
Amesema Abu Ramthah Rifaa'ah At-Taymiy (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa na nguo mbili za kijani. [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy kwa Isnaad iliyo Swahiyh]
Hadiyth – 6
وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم دَخَلَ يَوْمَ فَتْحِ مَكَّةَ وَعَلَيْهِ عِمَامَةٌ سَوْدَاء . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia siku ya kufunguliwa Makkah akiwa na akiwa na kilemba cheusi." [Muslim]
Hadiyth – 7
وعن أَبي سعيد عمرو بن حُرَيْثٍ رضي الله عنه ، قَالَ : كأنّي أنْظُرُ إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم وعليه عِمَامَةٌ سَوْدَاءُ ، قَدْ أرْخَى طَرَفَيْهَا بَيْنَ كَتِفَيْهِ . رواه مسلم .
وفي روايةٍ لَهُ : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم خَطَبَ النَّاسَ ، وَعَلَيْهِ عِمَامَةٌ سَوْدَاءُ .
Amesema Abu Sa'iyd 'Amruw bin Hurayth (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba ni kama mimi namuangalia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa na kilemba cheusi, ncha zake mbili zikiwa kwenye mabega yake." [Muslim]
Na katika riwaayah yake nyingine: Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwahutubia watu akiwa amevaa kilemba cheusi.
Hadiyth – 8
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كُفِّنَ رسول الله صلى الله عليه وسلم في ثلاثةِ أثْوَاب بيضٍ سَحُولِيَّةٍ مِنْ كُرْسُفٍ ، لَيْسَ فِيهَا قَمِيصٌ وَلاَ عِمَامَةٌ .متفقٌ عَلَيْهِ .
Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amevishwa sanda ya nguo tatu nyeupe zisizotengenezwa Sahuuliyyah (aina ya nguo kutoka kijiji hicho cha Yemen) kwa pamba, katika nguo hizo hakukuwa na kanzu wala kilemba." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]
Hadiyth – 9
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم ذات غَدَاةٍ ، وَعَلَيْهِ مِرْطٌ مرَحَّلٌ مِنْ شَعرٍ أسْوَد . رواه مسلم .
Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Alitoka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mchana mmoja akiwa amejifunika na nguo ya manyoa meusi iliyokuwa na picha ya ngamia." [Muslim]
Hadiyth – 10
وعن المغيرة بن شُعْبَةَ رضي الله عنه ، قَالَ : كُنْتُ مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ذاتَ لَيْلَةٍ في مسير ، فَقَالَ لي : (( أمَعَكَ مَاءٌ ؟ )) قلتُ : نَعَمْ ، فَنَزَلَ عَنْ رَاحِلَتِهِ فَمَشَى حَتَّى تَوَارَى في سَوَادِ اللَّيْلِ ، ثُمَّ جَاءَ فَأفْرَغْتُ عَلَيْهِ مِنَ الإدَاوَةِ ، فَغَسَلَ وَجْهَهُ وَعَلَيْهِ جُبَّةٌ مِنْ صُوفٍ ، فَلَمْ يَسْتَطِعْ أنْ يُخْرِجَ ذِرَاعَيْهِ مِنْهَا حَتَّى أخْرَجَهُمَا مِنْ أسْفَلِ الْجُبَّةِ ، فَغَسَلَ ذِرَاعَيْهِ وَمَسَحَ بِرَأسِهِ ، ثُمَّ أهْوَيْتُ لأَنْزَعَ خُفَّيْهِ ، فَقَالَ : (( دَعْهُمَا فَإنِّي أَدْخَلْتُهُمَا طَاهِرَتَيْنِ )) وَمَسحَ عَلَيْهِمَا . متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية : وَعَلَيْهِ جُبَّةٌ شَامِيَّةٌ ضَيِّقَةُ الكُمَّيْنِ .
وفي رواية : أنَّ هذِهِ القَضِيَّةَ كَانَتْ في غَزْوَةِ تَبُوكَ .
Amesema Mughiyrah bin Shu'bah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Usiku mmoja tulikuwa katika safari pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Akaniuliza: "Je, una maji?" Nikasema: "Ndio." Hapo alishuka juu ya kipando chake na kutembea kwenye njia kwa miguu mpaka akatoweka katika giza la usiku. Aliporudi nilimwagia maji kutoka katika chombo, naye akaosha uso wake. Wakati huo alikuwa amevaa juba la sufi na hivyo hakuweza kutoa mikono yake mpaka alipoitoa kutoka katika sehemu ya chini ya hilo juba. Aliosha mikono yake na kupangusa kichwa chake. Kisha nilitaka kumsaidia ili atoe soksi zake, akaniambia: "Ziache kama zilivyo kwani nilizivaa nikiwa katika hali ya tohara na usafi." Hivyo akapangusa juu yake." [Al-Bukhaariy na Muslim].
Na katika riwaayah: Alikuwaamevaa juba la Kishaam liliokuwa na mikono miwili.
Na katika riwaayah nyingine: Hakika tukio hili lilitokea katika Vita vya Taabuk.
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب القميص
02-Mlango Wa Kupendeza Kuvaa Kamisi (Kanzu)
Alhidaaya.com [4]
عن أُمِّ سَلَمَة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ أحَبُّ الثِّيَابِ إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم الْقَمِيص . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Amesema Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nguo bora kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ilikuwa ni kanzu." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema hii ni Hadiyth Hasan].
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب صفة طول القميص والكُم والإزار وطرف العمامة وتحريم إسبال شيء من ذلك على سبيل الخيلاء وكراهته من غير خيلاء
03-Mlango Wa Sifa ya Urefu wa Kanzu, Mikono Yake, Kikoi na Ncha ya Kilemba na Uharamu wa Kuburuza Chochote Katika Hizo Kwa Njia ya Kiburi na Karaha kwa Kufanya Hivyo Bila Kiburi
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أسماءَ بنتِ يزيد الأنصاريَّةِ رَضِيَ الله عنها ، قالت : كَانَ كُمُّ قَمِيص رسول الله صلى الله عليه وسلم إِلَى الرُّسْغِ . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Amesema Asmaa' bint Yaziyd Al-Ansaariyyah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Ilikuwa urefu wa mikono ya kanzu ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ikifika kwenye vifundo vya vitanga." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 2
وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ جَرَّ ثَوْبَهُ خُيَلاءَ لَمْ يَنْظُرِ اللهُ إِلَيْهِ يَوْمَ القِيَامَةِ )) فَقَالَ أَبُو بكر : يَا رسول الله ، إنَّ إزاري يَسْتَرْخِي إِلاَّ أنْ أَتَعَاهَدَهُ ، فَقَالَ لَهُ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّكَ لَسْتَ مِمَّنْ يَفْعَلُهُ خُيَلاءَ )) رواه البخاري وروى مسلم بعضه .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi, Hatamuangalia Allaah mtu huyo Siku ya Qiyaamah." Akasema Abu Bakr: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika kikoi changu kinanivuka bila kukusudia mpaka ninapokipandisha." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakika wewe si katika wale wanaofanya hivyo kwa kiburi." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لا يَنْظُرُ اللهُ يَوْمَ القِيَامَةِ إِلَى مَنْ جَرَّ إزاره بَطَراً )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Hamuangalii mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi." [Al-Bukhaariy, Muslim na Maalik]
Hadiyth – 4
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَا أسْفَل مِنَ الكَعْبَيْنِ مِنَ الإزْارِ فَفِي النار )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kilicho chini ya fundo mbili katika kikoi kitakuwa motoni." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 5
وعن أَبي ذر رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( ثلاثةٌ لا يُكَلِّمُهُمُ اللهُ يَوْمَ القِيَامَةِ ، وَلاَ يَنْظُرُ إلَيْهِمْ ، وَلاَ يُزَكِّيهِمْ ، وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ )) قَالَ : فقَرأها رسول الله صلى الله عليه وسلم ثلاثَ مِرار ، قَالَ أَبُو ذرٍّ : خَابُوا وَخَسِرُوا ! مَنْ هُمْ يَا رسول الله ؟ قَالَ : (( المُسْبِلُ ، وَالمنَّانُ ، وَالمُنْفِقُ سِلْعَتَهُ بِالحَلِفِ الكاذِبِ )) رواه مسلم .
وفي رواية لَهُ : (( المُسْبِلُ إزَارَهُ )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Hatazungumza na watu aina tatu Siku ya Qiyaamah wala Hatawaangalia na wala Hatawatakasa na watakuwa na adhabu iumizayo." Akasema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliikariri kauli hii mara tatu." Akasema Abu Dharr: "Watu hao wamehasirika, ni kina nani ee Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Mwenye kuburuza nguo kwa kiburi; na mwenye kujionyesha kwa fadhila aliomfanyia mtu mwengine; na mwenye kuuza mali duni kwa kiapo cha uongo." [Muslim]
Na katika riwaayah nyingine: "Mwenye kuburuza kikoi chake kwa kiburi."
Hadiyth – 6
وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( الإسْبَالُ في الإزار ، وَالقَمِيصِ ، وَالعِمَامةِ ، مَنْ جَرَّ شَيْئاً خُيَلاءَ لَمْ ينْظُرِ الله إِلَيْهِ يَوْمَ القِيَامَةِ )) رواه أَبُو داود والنسائي بإسناد صحيح .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Hatawaangalia wale watu walioburuza nguo zao kama kikoi na kanzu na kilemba kwa kiburi." [Abu Daawuwd na An-Nasaaii kwa Isnaad Swahiyh]
Hadiyth – 7
وعن أَبي جُرَيٍّ جابر بن سُلَيْم رضي الله عنه ، قَالَ : رَأَيْتُ رَجُلاً يَصْدُرُ النَّاسُ عَنْ رَأْيهِ ، لا يَقُولُ شَيْئاً إِلاَّ صَدَرُوا عَنْهُ ، قُلْتُ : مَنْ هَذَا ؟ قالوا : رسولُ الله صلى الله عليه وسلم . قُلْتُ : عَلَيْكَ السَّلامُ يَا رسول الله – مرّتين – قَالَ : (( لاَ تَقُلْ : عَلَيْكَ السَّلامُ ، عَلَيْكَ السَّلامُ تَحِيَّةُ المَوْتَى ، قُلْ : السَّلامُ عَلَيْكَ )) قَالَ : قُلْتُ : أنْتَ رسول اللهِ ؟ قَالَ : (( أنَا رسول الله الَّذِي إِذَا أصَابَكَ ضُرٌّ فَدَعَوْتَهُ كَشَفَه عَنْكَ ، وَإِذَا أصَابَكَ عَامُ سَنَةٍ فَدَعَوْتَهُ أَنْبَتَهَا لَكَ ، وَإِذَا كُنْتَ بِأَرْضٍ قَفْرٍ أَوْ فَلاَةٍ فَضَلَّتْ رَاحِلَتُكَ ، فَدَعَوْتَهُ رَدَّهَا عَلَيْكَ )) قَالَ : قُلْتُ : اعْهَدْ إِلَيَّ . قَالَ : (( لاَ تَسُبَّنَ أحَداً )) قَالَ : فَمَا سَبَبْتُ بَعْدَهُ حُرّاً ، وَلاَ عَبْداً ، وَلاَ بَعِيراً ، وَلاَ شَاةً ، (( ولاَ تَحْقِرَنَّ مِنَ المَعْرُوفِ شَيْئاً ، وأَنْ تُكَلِّمَ أخَاكَ وَأنْتَ مُنْبَسِطٌ إِلَيْهِ وَجْهُكَ ، إنَّ ذَلِكَ مِنَ المَعْرُوفِ ، وَارْفَعْ إزَارَكَ إِلَى نِصْفِ السَّاقِ ، فَإنْ أبَيْتَ فَإلَى الكَعْبَينِ ، وَإيَّاكَ وَإسْبَالَ الإزَار فَإنَّهَا مِنَ المخِيلَةِ . وَإنَّ اللهَ لاَ يُحِبُّ المَخِيلَةَ ؛ وَإن امْرُؤٌ شَتَمَكَ وعَيَّرَكَ بِمَا يَعْلَمُ فِيكَ فَلاَ تُعَيِّرْهُ بِمَا تَعْلَمُ فِيهِ ، فَإنَّمَا وَبَالُ ذَلِكَ عَلَيْهِ )) رواه أَبُو داود والترمذي بإسناد صحيح ، وقال الترمذي : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Jurayy Jaabir bin Sulaym (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nilimuona mtu ambaye rai zake zilikuwa zikikubaliwa na watu wote, alichokuwa akisema kilikuwa kikikubaliwa na watu. Niliuliza: "Ni nani huyu?" Nikaambiwa: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." Nikasema: "Amani iwe juu yako ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) - 'Alaykas Salaamu Yaa Rasuulallahi." Nikasema hilo mara mbili. akasema: "Usiseme 'Alaykas Salaamu, kwani 'Alaykas Salaamu ni salamu kwa wafu bali sema: 'As-Salaamu 'Alayka (Amani iwe juu yako)." Akasema (Abu Jurayy): Nikasema: Wewe ni Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Mimi ni Rasuli wa Allaah, ambaye ikiwa umepatikana na dhara aina yoyote nami nikakuombea basi utaondoshewa. Na ikiwa utapatikana katika ardhi yenye ukame (na hakuna kinachomea katika ardhi) nami nikaomba basi mimea itaanza kumea. Na lau utakuwa katika jangwa (lisilokuwa na binadamu wala maji) na kipando chako kikakutoroka, nami nikamuomba Yeye basi Atakurudishia." Nikasema: "Niusie mimi." Akasema: "Usimtusi yeyote." Akasema: "Sikuwahi kumtusi yeyote baada ya hapo, si muungwana wala mtumwa wala ngamia wala mbuzi." Akasema tena: "Usichukie kufanya wema aina yeyote; na unapozungumza na nduguyo basi zungumza naye kwa uso wa bashasha, hakika hilo ni katika wema. Na inyanyue izari (kikoi) yako mpaka katika muundi, ikiwa hutaweza basi juu ya fundo mbili (za miguu). Na nakuonya wewe usiwe ni mwenye kuburuza izari yako kwani hiyo ni ishara ya kiburi. Na hakika Allaah hampendi mwenye kiburi. Na ikiwa mtu atakutukana na kukulaumu na kukupakazia na makosa, kwa anayoyajua lakini wewe usimlaumu kwa makosa aliyo nayo kwa sababu yeye ndiye atakaye chukuliwa hatua kwa makosa yake hapa duniani na kesho Aakhera." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy kwa Isnaad Swahiyh]
Hadiyth – 8
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : بينما رَجُلٌ يُصَلَّي مسبلٌ إزَارَهُ ، قَالَ لَهُ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( اذْهَبْ فَتَوَضَّأ )) فَذَهَبَ فَتَوَضّأَ ، ثُمَّ جَاءَ ، فَقَالَ : (( اذْهَبْ فَتَوَضّأ )) فَقَالَ لَهُ رجُلٌ : يَا رسولَ اللهِ ، مَا لَكَ أمَرْتَهُ أنْ يَتَوَضّأَ ثُمَّ سَكَتَّ عَنْهُ ؟ قَالَ : (( إنّهُ كَانَ يُصَلِّي وَهُوَ مُسْبِلٌ إزَارَهُ ، وَإنَّ اللهَ لاَ يَقْبَلُ صَلاَةَ رَجُلٍ مُسْبلٍ )) رواه أَبُو داود بإسناد صحيح عَلَى شرط مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Alipokuwa mtu mmoja anaswali na huku kikoi chake kinaburuza, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: "Nenda ukashike wudhu." Yule mtu alikwenda akatawadha, kisha akarudi. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Nenda ukatawadhe." Mtu mmoja aliyekuwepo akasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Kuna nini, kwani umemuamrisha akatawadhe kisha umenyamaza?" Akasema: "Hakika yeye alikuwa anaswali na kikoi chake kinaburuza. Na kwa hakika Allaah haikubali Swalaah ya mtu anayeburuza nguo yake." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh kulingana na sharti ya Muslim]
Hadiyth – 9
وعن قيس بن بشر التَّغْلِبيِّ ، قَالَ : أخْبَرَني أَبي - وكان جَلِيساً لأَبِي الدرداء - قَالَ : كَانَ بِدمَشْق رَجُلٌ مِنْ أصْحَابِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم يقال لَهُ سهل بن الْحَنْظَلِيَّةِ ، وَكَانَ رَجُلاً مُتَوَحِّداً قَلَّمَا يُجَالِسُ النَّاسَ ، إنَّمَا هُوَ صَلاَةٌ ، فإذا فَرَغَ فَإنَّمَا هُوَ تَسْبِيحٌ وَتَكْبيرٌ حَتَّى يَأتي أهْلَهُ ، فَمَرَّ بنا وَنَحْنُ عِنْدَ أَبي الدَّرداء ، فَقَالَ لَهُ أَبُو الدرداءِ : كَلِمَةً تَنْفَعُنَا وَلاَ تَضُرُّكَ . قَالَ : بَعَثَ رسول الله صلى الله عليه وسلم سَرِيَّةً فَقَدِمَتْ ، فَجَاءَ رَجُلٌ مِنْهُمْ فَجَلَسَ في المَجْلِسِ الَّذِي يَجْلِسُ فِيهِ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ لِرَجُلٍ إِلَى جَنْبِهِ : لَوْ رَأيْتَنَا حِيْنَ التَقَيْنَا نَحْنُ وَالعَدُوُّ ، فَحَمَلَ فُلانٌ وَطَعَنَ ، فَقَالَ : خُذْهَا مِنِّي ، وَأنَا الغُلاَمُ الغِفَاريُّ ، كَيْفَ تَرَى في قَوْلِهِ ؟ قَالَ : مَا أرَاهُ إِلاَّ قَدْ بَطَلَ أجْرُهُ . فَسَمِعَ بِذلِكَ آخَرُ ، فَقَالَ : مَا أرَى بِذلِكَ بَأساً ، فَتَنَازَعَا حَتَّى سَمِعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ: (( سُبْحَانَ الله ؟ لاَ بَأسَ أنْ يُؤجَرَ وَيُحْمَدَ )) فَرَأَيْتُ أَبَا الدَّرْدَاء سُرَّ بِذلِكَ ، وَجَعَلَ يَرْفَعُ رَأسَهُ إِلَيْهِ ، وَيَقُولُ : أأنْتَ سَمِعْتَ ذَلِكَ مِنْ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ؟ فيقول : نَعَمْ ، فما زال يُعِيدُ عَلَيْهِ حَتَّى إنّي لأَقُولُ لَيَبْرُكَنَّ عَلَى رُكْبَتَيْهِ ، قَالَ : فَمَرَّ بِنَا يَوْماً آخَرَ ، فَقَالَ لَهُ أَبُو الدَّرْداء : كَلِمَةً تَنْفَعُنَا وَلاَ تَضُرُّكَ ، قَالَ : قَالَ لنا رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( المُنْفِقُ عَلَى الخَيْلِ ، كَالبَاسِطِ يَدَهُ بالصَّدَقَةِ لاَ يَقْبضُهَا )) ، ثُمَّ مَرَّ بِنَا يَوماً آخَرَ ، فَقَالَ لَهُ أَبُو الدَّرْداء : كَلِمَةً تَنْفَعنَا وَلاَ تَضُرُّكَ ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( نِعْمَ الرَّجُلُ خُرَيمٌ الأسَديُّ ! لولا طُولُ جُمَّتِهِ وَإسْبَالُ إزَارِهِ! )) فَبَلَغَ ذَلِكَ خُرَيْماً فَعَجَّلَ، فَأَخَذَ شَفْرَةً فَقَطَعَ بِهَا جُمَّتَهُ إِلَى أُذُنَيْهِ ، وَرَفَعَ إزارَهُ إِلَى أنْصَافِ سَاقَيْهِ . ثُمَّ مَرَّ بِنَا يَوْماً آخَرَ فَقَالَ لَهُ أَبُو الدَّرْداء : كَلِمَةً تَنْفَعُنَا وَلاَ تَضُرُّكَ ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إنَّكُمْ قَادِمُونَ عَلَى إخْوانِكُمْ ، فَأصْلِحُوا رِحَالكُمْ ، وَأصْلِحُوا لِبَاسَكُمْ حَتَّى تَكُونُوا كَأنَّكُمْ شَامَةٌ في النَّاسِ ؛ فإِنَّ الله لاَ يُحِبُّ الفُحْشَ وَلاَ التَّفَحُّش )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ حسنٍ ، إِلاَّ قيس بن بشر فاختلفوا في توثِيقِهِ وَتَضْعِيفِهِ ، وَقَدْ روى لَهُ مسلم .
Qays bin Bishr At-Taghlibiy amesema: Amenipasha habari mimi baba yangu ambaye alikuwa ni sahibu wa Abu Dardaa' (Radhwiya Allaahu 'anhu). Alisema: Kulikuwa na mtu Damascus aliyekuwa Swahaaba wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akijulikana kwa jina la Sahl bin Al-Handhaliyyah (Radhwiya Allaahu 'anhu). Na alikuwa ni mtu mwenye kupenda upweke na kujitenga na watu na hivyo hakukaa sana nao. Hakika alitumia muda wake mwingi katika Swalaah na alipomaliza kuswali basi alikuwa akijishughulisha katika kumtaja Allaah kwa kuleta Tasbihi (kusema Subhaana Allaah) na Takbira (Allaahu Akbar) mpaka familia yake wanapokuja kwa mahitaji yao. tulikuwa na Abu Dardaa' siku moja naye akawa anapita tukiwa tumekaa. Abu Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) Akasema: "Tuambie neno ambalo litatufaa sisi wala halitakudhuru wewe." Akasema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituma kikosi cha Mujahidina nacho baada ya muda kikarudi (baada ya kumaliza shughuli waliyotmwa nayo). Akaja mtu mmoja miongoni mwao na kukaa katika baraza ambayo anakaa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Huyu mtu alimwambia mwenziwe aliyekuwa ubavuni mwake: 'Lau ungetuona sisi tulipopambana na maadui. Mmoja wao (kafiri) alichukua fumo (mkuki) na kumchoma nao Muislamu, Na ambaye alisema na hakika mimi ni kijan wa Ghifari. Je, waonaje katika kauli yake hiyo?' Akasema: 'Nadhani kuwa amekosa ujira wake kwa ajili wa kujisifu.' Akasikia hayo mtu mwengine, naye akasema: 'sioni tatizo lolote katika hilo.' Walianza kubishana katika hilo mpaka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasikia, ambaye alisema: 'Ametakasika Allaah! Hakuna madhara yoyote kwa yeye kupatiwa ujira Kesho Aakherah na kumsifu hapa duniani.' Nikamuona Abu Dardaa' amefurahia kusikia hayo. Akawa anayanyua kichwa chake kwake na kusema: 'Wewe umesikia hayo kutoka kwa Rasuli wa Allaah?' Akasema: 'Ndio.' Akawa anaendelea kulikariri hilo swali mpaka nikamwambia kwa nini unamchagiza sana. Akasema (Bishr): Akapita tena siku nyengine, naye Abu Dardaa' akamuuliza: "Twambie neno ambalo litatufaa sisi wala halitakudhuru wewe." Akasema: "Alituambia Rausli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): 'Mwenye kutoa ili kumlisha chakula farasi (anayeandaliwa kwa jihadi katika njia ya Allaah) ni kama aliyeuacha wazi mkono wake kwa kutoa swadaqah na wala hakuufunga (anatoa bila ya kubana)." Kisha akapita tena siku nyengine, Abu Dardaa' akamuuliza tena: "Twambie neno ambalo litatufaa sisi wala halitakudhuru wewe." Akasema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 'Khuraym Al-Asadiy ni mtu bora na mzuri lau si kwa nywele zake ndefu na kuburuza kikoi chake.' Habari hizo zilipomfikia khuraym, hapo hapo alizikata nywele zake na kufika masikioni na akakinyanyua kikoi chake mpaka kikafika nusu ya muundi." Kisha akapita mara nyingine tena na Abu Dardaa' akamwambia: "Twambie neno ambalo litatufaa sisi wala halitakudhuru wewe." Akasema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika nyinyi munarudi kwa ndugu zenu, hivyo tengenezeni vipando vyenu na nguo zenu mpaka muwe katika hali ya ustahifu miongoni mwa watu. Hakika Allaah hapendi ujuvi wala uchakavu." [Abuu Daawuwd kwa Isnaad Hasan isipokuwa Qays bin Bishr, ambaye wametofautiana katika kumwamini na kumdhoofisha. Na hakika Muslim amepokea kutoka kwake].
Hadiyth – 10
وعن أَبي سعيد الخدريِّ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إزْرَةُ المُسْلِمِ إِلَى نِصْفِ السَّاقِ ، وَلاَ حَرَجَ – أَوْ لاَ جُنَاحَ – فِيمَا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الكَعْبَيْنِ ، فمَا كَانَ أسْفَلَ مِنَ الكَعْبَيْنِ فَهُوَ في النَّارِ ، وَمَنْ جَرَّ إزَارَهُ بَطَراً لَمْ يَنْظُرِ اللهُ إِلَيْهِ )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ صحيحٍ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iid Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kikoi cha Muislamu kinatakiwa kifike nusu muundi wala hapana tatizo lolote urefu wake ukiwa baina ya nusu muundi na nguyu zake mbili. Chochote kitakachokuwa chini ya nguyu mbili kitakuwa motoni. Allaah Hatamuangali kabisa mwenye kuburuza kikoi chake kwa kiburi." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Hasan]
Hadiyth – 11
وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : مررتُ عَلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم وفي إزَارِي استرخاءٌ ، فَقَالَ : (( يَا عَبدَ اللهِ ، ارْفَعْ إزَارَكَ )) فَرَفَعْتُهُ ثُمَّ قَالَ : (( زِدْ )) فَزِدْتُ ، فَمَا زِلْتُ أتَحَرَّاهَا بَعْدُ . فَقَالَ بَعْضُ القَوْم : إِلَى أينَ ؟ فَقَالَ : إِلَى أنْصَافِ السَّاقَيْنِ . رواه مسلم .
Amesema Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba: Nilipita mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kikoi changu kinaning'inia. Akasema: "Ee 'Abdallaah! Kipandishe Kikoi chako." Nami nikakipandisha. Kisha akasema: "Zidisha." Nami nikakipandisha tena na kuanzia wakati huo nikawa navaa kikiwa juu. Wakasema baadhi ya watu: "Juu mpaka wapi?" Akasema: "Mpaka nusu muundi." [Muslim]
Hadiyth – 12
وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ جَرَّ ثَوْبَهُ خُيَلاءَ لَمْ يَنْظُرِ اللهُ إِلَيْهِ يَوْمَ القِيَامَةِ )) فَقَالَتْ أُمُّ سَلَمَةَ : فَكَيْفَ تَصْنَعُ النِّسَاءُ بذُيُولِهِنَّ ؟ قَالَ : (( يُرْخِينَ شِبْراً )) قالت : إِذَاً تَنْكَشِفُ أقْدَامُهُنَّ . قَالَ : (( فَيرخِينَهُ ذِرَاعاً لاَ يَزِدْنَ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi, Allaah hatamuangalia siku ya Qiyaamah." Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) akauliza: "Hivyo watafanyaje wanawake kwa marinda (sketi) yao?" Akasema: "Waziteremshe shibiri." (Ummu Salamah) akauliza: "Hivyo, miguu yao itaonekana." Akasema: "Waziteremshe dhiraa na wala wasizidishe zaidi ya hapo." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب ترك الترفع في اللباس تواضعاً
04-Mlango Wa Kupendeza Kuacha Mavazi ya Kifahari kwa Sababu ya Unyenyekevu
Alhidaaya.com [4]
قَدْ سَبَقَ في بَابِ فَضْل الجُوعِ وَخشُونَةِ العَيْشِ جُمَلٌ تَتَعَلَّقُ بهذا الباب .
Tumetaja katika mlango wa fadhila za kuwa katika hali ya njaa na dhiki za kimaisha jumla ya Hadiythi zinazuhusiana na mlango huu.
وعن معاذ بن أنسٍ رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ تَرَكَ اللِّبَاس تَوَاضُعاً للهِ ، وَهُوَ يَقْدِرُ عَلَيْهِ ، دَعَاهُ اللهُ يَومَ القِيَامَةِ عَلَى رُؤوسِ الخَلائِقِ حَتَّى يُخَيِّرَهُ مِنْ أيِّ حُلَلِ الإيمَانِ شَاءَ يَلْبَسُهَا )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Mu'aadh bin Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuacha mavazi ya gharama japokuwa ana uwezo huo kwa unyenyekevu kwa ajili ya Allaah basi atatanguliza kuitwa na Allaah Siku wa Qiyaamah mbele ya viumbe vyote mpaka apatiwe fursa ya kuchagua vazi lolote la Imaani analolitaka." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب التوسط في اللباس وَلاَ يقتصر عَلَى مَا يزري بِهِ لغير حاجة وَلاَ مقصود شرعي
05-Mlango Wa Kupendeza Kuwa Kati na Kati Katika Mavazi na Kujiepusha na Mavazi Fulani Bila ya Haja Wala Makusudio ya Kisheria
Alhidaaya.com [4]
عن عمرو بن شعيب ، عن أبيهِ ، عن جَدِّهِ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ اللهَ يُحِبُّ أنْ يُرَى أثَرُ نِعْمَتِهِ عَلَى عَبْدِهِ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Amru bin Shu'ayb (Radhwiya Allaahu 'anhu) kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah anapenda kuona athari ya neema Yake kwa mja Wake." [At-Tirmidhiy, na akasema Hadiyth Hasan]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم لباس الحرير عَلَى الرجال ، وتحريم جلوسهم
عَلَيْهِ واستنادهم إِلَيْهِ وجواز لبسه للنساء
06-Mlango Wa Uharamu wa Kuvaa Hariri kwa Wanaume na Uharamu wa Kukaa Juu Yake na Kuegemea na Kujuzu Kuvaa kwa Wanawake
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن عمر بن الخَطَّابِ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَلْبَسُوا الحَرِيرَ ؛ فَإنَّ مَنْ لَبِسَهُ في الدُّنْيَا لَمْ يَلْبَسْهُ في الآخِرَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Khatwaab (Radhwiya Allaah 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Musivae hariri, hakika mwenye kuvaa duniani hatovaa Aakherah." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasai]
Hadiyth – 2
وعن عمر بن الخَطَّابِ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إنَّمَا يَلْبَسُ الحَرِيرَ مَنْ لاَ خَلاَقَ لَهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية للبخاري : (( مَنْ لاَ خَلاَقَ لَهُ في الآخِرَةِ )) .
Amesema 'Umar Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) akisema: "Hakika anayevaa hariri ni yule asiye na fungu (hatovaa) Aakherah." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasai]
Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy: "Ni asiye na fungu lake Aakherah."
Hadiyth – 3
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ لَبِسَ الحَرِيرَ في الدُّنْيَا لَمْ يَلْبَسْهُ في الآخِرَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuvaa hariri duniani hatovaa Aakherah." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن علي رضي الله عنه ، قَالَ : رأيتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم أخَذَ حَريراً ، فَجَعَلَهُ في يَمِينهِ ، وَذَهَبَاً فَجَعَلَهُ في شِمَالِهِ ، ثُمَّ قَالَ : (( إنَّ هذَيْنِ حَرَامٌ عَلَى ذُكُور أُمّتي )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ صحيحٍ .
Amesema 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akichukua hariri na kuiweka mkono wake wa kulia na dhahabu akaishika kwa mkono wake wa kushoto, kisha akasema: "Hakika hivi vitu viwili ni haramu kwa wanaume wa Ummah wangu." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Hasan]
Hadiyth – 5
وعن أَبي موسى الأشْعَري رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( حُرِّمَ لِبَاسُ الحَرِير وَالذَّهَبِ عَلَى ذُكُورِ أُمَّتِي ، وَأُحِلَّ لإنَاثِهِمْ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-'Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Imeharamishwa kuvaa hariri na dhahabu kwa wanaume wa Ummah wangu na ikahalalishwa kwa wanawake wao." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 6
وعن حُذَيْفَةَ رضي الله عنه ، قَالَ : نَهَانَا النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم أنْ نَشْرَبَ في آنِيَةِ الذَّهَبِ وَالفِضَّةِ ، وأنْ نَأْكُلَ فِيهَا ، وعَنْ لُبْس الحَريرِ وَالدِّيبَاج ، وأنْ نَجْلِسَ عَلَيْهِ . رواه البخاري .
Amesema Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Ametukataza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kunywa katika vyombo vya dhahabu na fedha na kula ndani yake na pia kuvaa hariri na dibaji na kukaa juu yake." [Al-Bukhaariy]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب جواز لبس الحرير لمن بِهِ حكة
07-Mlango Wa Ruhusa ya Kuvaa Hariri kwa Mwenye Ungonjwa wa Ngonzi
Alhidaaya.com [4]
عن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : رَخَّصَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم لِلزُّبَيْرِ وعَبْدِ الرَّحْمان بن عَوْفٍ رضي الله عنهما في لُبْس الحَريرِ لِحَكَّةٍ كَانَتْ بِهِما . متفقٌ عَلَيْهِ .
Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimruhusu Zubayr na 'Abdir-Rahmaan bin 'Awf (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuvaa nguo ya hariri, kutokana na ugonjwa wa ngozi waliokuwa nao." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن افتراش جلود النمور والركوب عَلَيْهَا
08-Mlango Wa Kukatazwa Kukaa na Kupanda Juu ya Ngozi ya Chui
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن معاوية رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَرْكَبُوا الخَزَّ وَلاَ النِّمَارَ )) حديث حسن ، رواه أَبُو داود وغيره بإسناد حسن .
Hadiyth – 2
وعن أَبي المليح ، عن أبيه رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم نَهَى عَنْ جُلُودِ السِّبَاعِ . رواه أَبُو داود والترمذيُّ والنسائيُّ بأسانِيد صِحَاحٍ .
وفي رواية للترمذي : نَهَى عَنْ جُلُودِ السِّبَاعِ أنْ تُفْتَرَشَ .
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب مَا يقول إِذَا لبس ثوباً جديداً أَوْ نعلاً أَوْ نحوه
09-Mlango Wa Anachosema Mtu Anapovaa Nguo Mpya
Alhidaaya.com [4]
عن أَبي سعيد الخدْريِّ رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم إِذَا اسْتَجَدَّ ثَوباً سَمَّاهُ باسْمِهِ – عِمَامَةً ، أَوْ قَميصاً ، أَوْ رِدَاءً – يقولُ : (( اللَّهُمَّ لَكَ الْحَمْدُ أنْتَ كَسَوْتَنِيهِ ، أسْأَلكَ خَيْرَهُ وَخَيْرَ مَا صُنِعَ لَهُ ، وَأَعوذُ بِكَ مِنْ شَرِّهِ وَشَرِّ مَا صُنِعَ لَهُ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب الابتداء باليمين في اللباس
10-Mlango Wa Kupendeza Kuanza Kuliani Katika Kuvaa Nguo
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يُعْجِبُهُ التَّيَمُّنُ في شَأنِهِ كُلِّهِ : في طُهُورِهِ ، وَتَرَجُّلِهِ ، وَتَنَعُّلِهِ . متفقٌ عَلَيْهِ .
'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anha) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapenda kuanza kuliani katika mambo yake yote: Katika kijitwahirisha kwake, kuchana nywele zake na kuvaa viatu vyake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَتْ يَدُ رسول الله صلى الله عليه وسلم اليُمْنَى لِطُهُورِهِ وَطَعَامِهِ ، وَكَانَتِ الْيُسْرَى لِخَلائِهِ وَمَا كَانَ مِنْ أذَىً . حديث صحيح ، رواه أَبُو داود وغيره بإسنادٍ صحيحٍ .
'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anha) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitumia mkono wake wa kuume kwa kujitwahirisha na kulia chakula. Na alikuwa anautumia mkono wake wa kushoto kujisafisha anapoingia haja (chooni) na mambo mengine kama hayo." [Hadiyth Swahiyh, Abu Daawuwd na wengineo kwa Isnaad iliyo Swahiyh].
Hadiyth – 3
وعن أم عطية رضي الله عنها : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ لهن في غَسْلِ ابْنَتِهِ زَيْنَبَ رضي الله عنها : (( ابْدَأنَ بِمَيَامِنِهَا ، وَمَوَاضِعِ الوُضُوءِ مِنْهَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ummu 'Atwiyyah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwaambia walipokuwa wanamuosha binti yake, Zaynab (Radhwiya Allaahu 'anhaa): "Anzeni kuliani kwake na sehemu za udhu wake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا انْتَعَلَ أحَدُكُمْ فَلْيَبْدَأْ بِالْيُمْنَى ، وَإِذَا نَزَعَ فَلْيَبْدأْ بِالشِّمَالِ . لِتَكُنْ اليُمْنَى أوَّلَهُمَا تُنْعَلُ ، وَآخِرُهُمَا تُنْزَعُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mmoja wenu anapovaa viatu aanze kwa mguu wa kulia na anapovua aanze kwa mguu wa kushoto. Hivyo, uwe mguu wa kulia wa mwanzo kuvaa nao viatu na wa mwisho kuvua viatu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 5
وعن حفصة رضي الله عنها : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يجعل يَمينَهُ لطَعَامِهِ وَشَرَابِهِ وَثِيَابِهِ ، وَيَجْعَلُ يَسَارَهُ لِمَا سِوَى ذَلِكَ . رواه أَبُو داود والترمذي وغيره .
Imepokewa kutoka kwa Hafswah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliujaalia mkono wake wa kulia ni wa kulia chakula, na kunywea kinywaji na kuvulia nguo. Na aliutumia mkono wake wa kushoto kwa mambo mengine yasiyokuwa hayo." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy na wengineo]
Hadiyth – 6
وعن أَبي هُريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا لَبِسْتُمْ ، وَإِذَا تَوَضَّأتُمْ ، فَابْدَأوا بأيَامِنِكُمْ )) حديث صحيح ، رواه أَبُو داود والترمذي بإسناد صحيح .
Imepokewa kutoka kwa Ahu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Alllahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anzeni kwa mkono wenu wa kulia mnapovaa nguo na mnapo tawadha." [Hadiyth Swahiyh, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy kwa Isnaad Swahiyh]
Hadiyth – 7
وعن أنس رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أتى مِنىً ، فَأتَى الْجَمْرَةَ فَرَمَاهَا ، ثُمَّ أتَى مَنْزِلَهُ بِمِنَىً ونحر ، ثُمَّ قَالَ لِلحَلاَّقِ : (( خُذْ )) وأشَارَ إِلَى جَانِبهِ الأَيْمَنِ ، ثُمَّ الأَيْسَرِ ، ثُمَّ جَعَلَ يُعْطِيهِ النَّاسَ . متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية : لما رمَى الجَمْرَةَ ، وَنَحَرَ نُسُكَهُ وَحَلَقَ ، نَاوَلَ الحَلاَّقَ شِقَّهُ الأَيْمَنَ فَحَلَقَهُ ، ثُمَّ دَعَا أَبَا طَلْحَةَ الأنْصَارِيَّ رضي الله عنه ، فَأعْطَاهُ إيَّاهُ ، ثُمَّ نَاوَلَهُ الشِّقَّ الأَيْسَرَ ، فَقَالَ : (( احْلِقْ )) ، فَحَلَقَهُ فَأعْطَاهُ أَبَا طَلْحَةَ ، فَقَالَ : (( اقْسِمْهُ بَيْنَ النَّاسِ )) .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifika Mina, akalielekea Jamarah na kutupa vijiwe. Baada ya hapo alirudi kwenye hema lake hapo Mina na kuchinja mnyama wake. Kisha alimwambia kinyozi: "Chukua (yaani amnyoe)." Akamuashiria upande wa kuliani (mwa kichwa chake) na kisha kushoto. Akawa anawapatia nywele zake watu (aliponyolewa). [Al-Bukhaariy, Muslim, abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Na katika riwaayah nyingine: Baada ya kurusha vijiwe kwenye Jamarah na kuchinja mnyama wake na akajitayarisha kunyolewa, alimuonyesha kinyozi upande wa kulia naye akamnyoa. Kisha alimuita abu Twalhah Al-Ansaariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) na akampatia hizo nywele. Baada ya hilo, alimuonyehsa kinyozi upande wa kushoto, na akanyolewa upande huo pia. akampatia Abu Twalhah nywele hizo na kumwambia: "Wagawanyie watu."
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/280
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10317&title=03-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20-%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%90%D8%A8%D9%8E%D8%A7%D8%B3%D9%90
[4] http://www.alhidaaya.com/
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11005&title=01-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kuvaa%20Nguo%20Nyeupe%20na%20Kujuzu%20Nyekundu%2C%20Kijani%2C%20Njano%2C%20Nyeusi%20na%20Kujuzu%20Nguo%20ya%20Pamba%2C%20Katani%2C%20Sufi%20na%20ya%20Manyoa%20na%20Nyinginezo%20Isipokuwa%20ya%20Hariri
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11006&title=02-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kuvaa%20Kamisi%20%28Kanzu%29
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11007&title=03-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Sifa%20ya%20Urefu%20wa%20Kanzu%2C%20Mikono%20Yake%2C%20Kikoi%20na%20Ncha%20ya%20Kilemba%20na%20Uharamu%20wa%20Kuburuza%20Chochote%20Katika%20Hizo%20Kwa%20Njia%20ya%20Kiburi%20na%20Karaha%20kwa%20Kufanya%20Hivyo%20Bila%20Kiburi
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11008&title=04-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kuacha%20Mavazi%20ya%20Kifahari%20kwa%20Sababu%20ya%20Unyenyekevu
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11009&title=05-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kuwa%20Kati%20na%20Kati%20Katika%20Mavazi%20na%20Kujiepusha%20na%20Mavazi%20Fulani%20Bila%20ya%20Haja%20Wala%20Makusudio%20ya%20Kisheria
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11010&title=06-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Uharamu%20wa%20Kuvaa%20Hariri%20kwa%20Wanaume%20na%20Uharamu%20wa%20Kukaa%20Juu%20Yake%20na%20Kuegemea%20na%20Kujuzu%20Kuvaa%20kwa%20Wanawake
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11011&title=07-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Ruhusa%20ya%20Kuvaa%20Hariri%20kwa%20Mwenye%20Ungonjwa%20wa%20Ngonzi
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11012&title=08-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kukatazwa%20Kukaa%20na%20Kupanda%20Juu%20ya%20Ngozi%20ya%20Chui
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11013&title=09-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Anachosema%20Mtu%20Anapovaa%20Nguo%20Mpya
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11014&title=10-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kuanza%20Kuliani%20Katika%20Kuvaa%20Nguo