أَحاديثُ عَنْ فَضْلِ الْعِلْم وَالْعُلَمَاء
Hadiyth Kuhusu
Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa
Alhidaaya.com [2]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 01
Kutafuta ‘Ilmu Ni Fardhi Kwa Kila Muislaam
Alhidaaya.com [4]
عن أنس بْنِ مَالِكٍ قَالَ :عن النبيِّ صلَّى اللهُ عليهِ وسلَّم أنه قالَ : (طَلَبُ العِلْمِ فَرِيْضَةٌ عَلَىْ كُلِّ مُسْلِمٍ ) . رواه ابن ماجه
Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kutafuta ‘Ilmu ni faradhi juu ya kila Muislaam.” [Ibn Maajah (224), ameisahihisha Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (Uk 184)].
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 02
Allaah Atamsahilishia Mwenye Kutafuta ‘Ilmu Njia Ya Kuingia Jannah
Alhidaaya.com [4]
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم "((مَنْ سَلَكَ طَرِيقًا يَلْتَمِسُ فِيهِ عِلْمًا سَهَّلَ اللَّهُ لَهُ بِهِ طَرِيقًا إِلَى الْجَنَّةِ)) مسلم
Abu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Yeyote anayetoka katika njia akiitafuta kutokana nayo (njia hiyo) ‘Ilmu, Allaah Humfanyia sahali njia ya kuingia Jannah (Pepon).” [Muslim]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 03
Allaah Akimtakia Mja Wake Kheri Humjaali Ufaqahi Wa Dini
Alhidaaya.com [4]
وَعَنْ مُعَاوِيَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ يُرِدِ اَللَّهُ بِهِ خَيْرًا، يُفَقِّهْهُ فِي اَلدِّينِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Mu’aawiyah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah Akimtakia mja Wake kheri Humjaalia ufaqihi (‘ilmu ya kina) katika Dini.” [Bukhaariy, Muslim]
Faida:
Elimu ya halaal na haraam katika Shariy’ah inaitwa Fiqh. Maelezo haya yanaonesha utukufu na ukubwa wa somo hili muhimu. Kilichoelezwa hapa ni elimu ya Qur-aan na Sunnah ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 04
Anayeongoza Katika Kheri Atapata Ujira Wa Mwenye Kutekeleza Kheri Hiyo
Alhidaaya.com [4]
وَعَنْ أَبِي مَسْعُودٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ دَلَّ عَلَى خَيْرٍ، فَلَهُ مِثْلُ أَجْرِ فَاعِلِهِ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kujulisha kheri atapata mfano wa ujira (malipo) wa mwenye kuifanya.” [Muslim]
Na pia,
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: (( مَنْ دَعَا إِلَى هُدًى كَانَ لَهُ مِنَ الأَجْرِ مِثْلُ أُجُورِ مَنْ تَبِعَهُ لاَ يَنْقُصُ ذَلِكَ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْئًا)) مسلم
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Yeyote anayelingania katika uongofu, atakuwa na ujira mfano ujira wa anayemfuata, hatapunguziwa kutokana ujira huo chochote)) [Muslim]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 05
Vikao Vya ‘Ilmu Huteremkiwa Utulivu, Hufunikwa Rahma,
Malaika Huwazunguka Na Allaah Huwataja
Alhidaaya.com [4]
عن أبي هُرَيْرَة رضي اللهُ عنه، عن النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قال مَا اجتَمَعَ قَوْمٌ في بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللهِ يَتْلُونَ كِتَابَ اللهِ ويَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ، إلا نَزَلَتْ عليهمُ السَّكِينَةُ، وغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ، وحَفَّتهُمُ المَلائِكَةُ، وذَكَرَهُمُ اللهُ فيمَنْ عِنْدَه)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Hawajumuiki watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah wakisoma Kitabu cha Allaah na wakasomeshana baina yao ila watateremkiwa na utulivu na itawafunika rehma, na Malaika watawazunguka, na Allaah Atawataja kwa walio Naye. [Muslim]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 06
‘Ilmu Ni Kama Mfano Wa Ardhi Yenye Rutuba Inayonufaisha Watu
Alhidaaya.com [4]
عَنْ أَبِي مُوسَى، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " مَثَلُ مَا بَعَثَنِي اللَّهُ بِهِ مِنَ الْهُدَى وَالْعِلْمِ كَمَثَلِ الْغَيْثِ الْكَثِيرِ أَصَابَ أَرْضًا، فَكَانَ مِنْهَا نَقِيَّةٌ قَبِلَتِ الْمَاءَ، فَأَنْبَتَتِ الْكَلأَ وَالْعُشْبَ الْكَثِيرَ، وَكَانَتْ مِنْهَا أَجَادِبُ أَمْسَكَتِ الْمَاءَ، فَنَفَعَ اللَّهُ بِهَا النَّاسَ، فَشَرِبُوا وَسَقَوْا وَزَرَعُوا، وَأَصَابَتْ مِنْهَا طَائِفَةً أُخْرَى، إِنَّمَا هِيَ قِيعَانٌ لاَ تُمْسِكُ مَاءً، وَلاَ تُنْبِتُ كَلأً، فَذَلِكَ مَثَلُ مَنْ فَقِهَ فِي دِينِ اللَّهِ وَنَفَعَهُ مَا بَعَثَنِي اللَّهُ بِهِ، فَعَلِمَ وَعَلَّمَ، وَمَثَلُ مَنْ لَمْ يَرْفَعْ بِذَلِكَ رَأْسًا، وَلَمْ يَقْبَلْ هُدَى اللَّهِ الَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ ". قَالَ أَبُو عَبْدِ اللَّهِ قَالَ إِسْحَاقُ وَكَانَ مِنْهَا طَائِفَةٌ قَيَّلَتِ الْمَاءَ. قَاعٌ يَعْلُوهُ الْمَاءُ، وَالصَّفْصَفُ الْمُسْتَوِي مِنَ الأَرْضِ.
Abu Muwsaa Al-Ash’ariyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mfano wa mwongozo na ‘Ilmu Aliyonituma nayo Allaah ni kama mvua nyingi iliyonyesha juu ya ardhi, kukawa katika hiyo ni ardhi safi ilisharaba maji (ilinyonya mvua) na kuotesha mimea na nyasi nyingi. Na sehemu nyingine ilikuwa ngumu ikazuia maji, na Allaah Akawafaidisha nayo watu, na wakayanywa, wakanywesha (wanyama wao) na wakamwagilia mashamba. (Na) mvua ikanyeshea sehemu nyingine iliokuwa jangwa ambao hakuweza kubeba maji wala kuotesha majani. Huo ni mfano wa mtu aliyefahamu Dini ya Allaah na akapata manufaa (kutokana na ‘Ilmu) ambayo Allaah Amenituma nayo, kwa hiyo akajua na kuwafundisha wengine. Na Mfano wa yule ambae hakuinua kichwa chake kwa ajili ya hilo (mwongozo wa Allaah) na wala hakukubali mwongozo wa Allaah ambao nimetumwa nayo.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 07
Mtu Mmoja Akiongoka Ni Bora Kuliko Kupata Ngamia Mwekundu
Alhidaaya.com [4]
عَنْ سَهْلِ بن سعدٍ، t، أنَّ النَّبيَّ ﷺ قَالَ لِعَليًّ، : فو اللَّهِ لأنْ يهْدِيَ اللَّه بِكَ رجُلًا واحِدًا خَيْرٌ لكَ من حُمْرِ النَّعم متفقٌ عليهِ.
Sahl bin Sa’iyd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimwambia ‘Aliy bin Abi Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “Naapa kwa Allaah kwamba Akimuongoa Allaah mtu mmoja kupitia kwako ni bora kwako kuliko ngamia mwekundu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 08
Balighisheni Japo Aayah Moja Tahadharini Kumzulia Uongo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)
Alhidaaya.com [4]
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو العَاص (رضي الله عنهما) أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((بَلِّغُوا عَنِّي وَلَوْ آيَةً، وَحَدِّثُوا عَنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلاَ حَرَجَ، وَمَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ)) البخاري
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr Al-‘Aasw (رضي الله عنهما) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Balighisheni (fikisheni) kutoka kwangu japo Aayah moja. Na simulieni kuhusu habari za Wana wa Israaiyl wala hakuna dhambi [ubaya]. Na mwenye kunizulia uongo kwa makusudi, basi ajiandalie makazi yake motoni)). [Al-Bukhaariy]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 09
‘Ilmu Inayonufaisha Inaendelea Kumpatia Ujira Mtu Baada Ya Kufariki
Alhidaaya.com [4]
عَنْ أَبِي هُرَيْرَة (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِذَا مَاتَ ابْنُ آدَم انْقَطَعَ عَمَلُهُ إلاَّ مِنْ ثَلاَث: صَدَقَةٍ جَارِيَةٍ أَوْ عِلْمٍ يُنْتَفَعُ بِهِ أَوْ وَلَدٍ صَالِحٍ يَدْعُو لَهُ)) مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Bin Aadam akifa, ‘amali zake hukatika isipokuwa mambo matatu: Swadaqah inayoendelea, au elimu inayonufaisha, au mtoto mwema anayemuombea du’aa)). [Muslim]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 10
Dunia Imelaaniwa Isipokuwa Matatu Dhikru-Allaah ‘Aalim Na Mwanafunzi Wa Dini
Alhidaaya.com [4]
عن أبي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: (( أَلاَ إِنَّ الدُّنْيَا مَلْعُونَةٌ مَلْعُونٌ مَا فِيهَا إِلاَّ ذِكْرُ اللَّهِ ، وَمَا وَالاَهُ ، وَعَالِمٌ أَوْ مُتَعَلِّمٌ)) الترمذي وقال: حَدِيثٌ حَسَنٌ
Imepokelewa toka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: ((Zindukeni! Dunia imelaaniwa, kimelaaniwa kilichomo humo isipokuwa kumtaja Allaah na jambo linalokaribiana na hilo (la kumtii Allaah), ‘Aalim na anayejifunza [Dini])) [At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Hasan]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 11
Allaah Amneemeshe Mtu Anayebalighisha Risala Kama Alivyosikia
Alhidaaya.com [4]
عن إبْنِ مَسْعُودٍ (رضي الله عنه) ِ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولُ الله صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: (( نَضَّرَ اللَّهُ امْرَأً سَمِعَ مِنَّا شَيْئًا فَبَلَّغَهُ كَمَا سَمِعَه، فَرُبَّ مُبَلِّغٍ أَوْعَى مِنْ سَامِعٍ)) وراوه الترمذي وقَالَ : حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ
Imepokelewa toka kwa ibn Mas’uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) ambaye amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: ((Allaah Amneemeshe mtu aliyesikia kitu kutoka kwetu naye akakifikisha kama alivyosikia. Huenda anayefikishiwa akawa mwenye kufahamu zaidi kuliko aliyesikia)) [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 12
Aliyekuwa Umahiri Wa Qur-aan Yupamoja Na Malaika,
Ama Anayejifunza Ana Thawabu Mara Mbili
Alhidaaya.com [4]
عَنْ عَائِشَةَ قَالَتْ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((الْمَاهِرُ بِالْقُرْآنِ مَعَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ وَالَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَيَتَتَعْتَعُ فِيهِ وَهُوَ عَلَيْهِ شَاقٌّ لَهُ أَجْرَانِ))
'Aaishah (رضي الله عنها) amesimulia: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Yule aliyekuwa mahiri (mwenye ujuzi) wa kusoma Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika Waandishi wa Allaah watukufu, na yule ambaye anaisoma Qur-aan kwa mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa atapata ujira mara mbili)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 13
Ubora Wa ‘Aalim - Allaah Na Viumbe Wote Wanamuombea (Maghfirah Na Kila Khayr)
Mwenye Kufundisha Watu Mambo Ya Khayr (Ya Dini Ya Kiislaam)
Alhidaaya.com [4]
عَنْ أَبِي أُمَامَةَ (رضي الله عنه) أنَّ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قال: ((فضْلُ الْعَالِمِ عَلَى الْعَابِدِ كَفَضْلِي عَلَى أَدْنَاكُم)) ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ وَمَلاَئِكَتَهُ وَأَهْلَ السَّمَوَاتِ وَالأَرَض حَتَّى النَّمْلَةَ فِي جُحْرِهَا وَحَتَّى الْحُوتَ لَيُصَلُّونَ عَلَى مُعَلِّمِي النَّاسِ الْخَيْرَ)) رواه الترمذي وقَالَ حَدِيثٌ حَسَنٌ.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Umaamah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم ) amesema: “Ubora wa ‘Aalim (Mwanazuoni) juu ya mfanya ‘Ibaadah, ni kama ubora wangu juu ya mwenye daraja ya chini miongoni mwenu.” Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hakika Allaah na Malaika Wake, na walio mbinguni, hata wadudu chungu waliomo katika mashimo yao, na hata samaki, wanawaombea (maghfirah na khayr) wanaowafundisha watu kheri.” [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 14
Anayejifunza Au Kufundisha ‘Ilmu Msikitini
Yuko Katika Daraja La Mujaahid Fiy SabiliLLaah
Alhidaaya.com [4]
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ : سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ : (مَنْ جَاءَ مَسْجِدِي هَذَا لَمْ يَأْتِهِ إِلَّا لِخَيْرٍ يَتَعَلَّمُهُ أَوْ يُعَلِّمُهُ فَهُوَ بِمَنْزِلَةِ الْمُجَاهِدِ فِي سَبِيلِ اللَّهِ ، وَمَنْ جَاءَ لِغَيْرِ ذَلِكَ فَهُوَ بِمَنْزِلَةِ الرَّجُلِ يَنْظُرُ إِلَى مَتَاعِ غَيْرِهِ)
Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: "Yeyote anayekuja kwenye Msikiti wangu huu, na anakuja tu kwa kusudio zuri, kama vile kujifunza au kufundisha, daraja lake ni kama ya yule Mujaahid fiy SabiliLLaah. Yeyote anayekuja kwa sababu nyingine yoyote, daraja lake ni ya mtu ambaye analinda mali ya watu wengine.” [Ahmad (14/257), Ibn Maajah (223), ameisahihisha Al-Albaaniy: Swahiyh Ibn Maajah (187)]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 15
Husda Imeruhusika Kwa Aliyejaaliwa ‘Ilmu Akaifanyia Kazi Na Kuifundisha
Alhidaaya.com [4]
عَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ رضى الله عنه قَالَ سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ " لاَ حَسَدَ إِلاَّ فِي اثْنَتَيْنِ رَجُلٌ آتَاهُ اللَّهُ مَالاً فَسَلَّطَهُ عَلَى هَلَكَتِهِ فِي الْحَقِّ، وَرَجُلٌ آتَاهُ اللَّهُ حِكْمَةً فَهْوَ يَقْضِي بِهَا وَيُعَلِّمُهَا ".
Kutoka kwa Ibn Mas’uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nilimsikia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) "Hakuna husda isipokuwa kwa wawili: Mtu ambaye Allaah amempa mali na anaitumia katika njia sahihi, na mtu ambaye Allaah Amempa hekima (yaani, elimu ya Qur-aan na Sunnah) na anafanya maamuzi yake kufuatana nayo na anawafundisha wengine." [Al-Bukhaariy, Muslim]
Faida:
Katika lugha ya kiarabu ‘Hasad’ (husuda na wivu) hurejea kwa mtu anayemuonea wivu mwenzake na kuhusudu alichokuwa nacho na kutamani neema ile imuondokee na ije kwake. Jambo hili limekatazwa. Ikiwa mtu anatamani apate kitu fulani lakini hataki vile vile kimuondokee mwenzake, jambo hili linaitwa ‘Hiqd’. Hisia hii inahitajika katika mambo ya kidini. Kwa hiyo Hadiyth hii imekusudiwa husda ya kutamani mtu awe kama hao watu wa aina mbili, na sio hiqd ambayo inamaanisha kutamani mtu neema za hao watu wawili ziwaondokee.
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 16
Fadhila Za ‘Aalim Na ‘Ulamaa Ni Warithi Wa Manabii
Alhidaaya.com [4]
عن أبي الدرداء رضي الله عنه قال : سمعتُ رسولَ الله صلَّى الله عليه وسلَّم يقول: «مَنْ سَلَكَ طَرِيقًا يَطْلُبُ فِيهِ عِلْمًا سَلَكَ اللهُ بِهِ طَرِيقًا مِنْ طُرُقِ الجَنَّةِ، وَإِنَّ المَلَائِكَةَ لَتَضَعُ أَجْنِحَتَهَا رِضًا لِطَالِبِ العِلْمِ، وَإِنَّ العَالِمَ لَيَسْتَغْفِرُ لَهُ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَمَنْ فِي الأَرْضِ وَالحِيتَانُ فِي جَوْفِ المَاءِ، وَإِنَّ فَضْلَ العَالِمِ عَلَى العَابِدِ كَفَضْلِ القَمَرِ لَيْلَةَ البَدْرِ عَلَى سَائِرِ الكَوَاكِبِ، وَإِنَّ العُلَمَاءَ وَرَثَةُ الأَنْبِيَاءِ، وَإِنَّ الأَنْبِيَاءَ لَمْ يُوَرِّثُوا دِينَارًا وَلَا دِرْهَمًا، إِنَّمَا وَرَّثُوا العِلْمَ، فَمَنْ أَخَذَهُ أَخَذَ بِحَظٍّ وَافِرٍ» [رواه أبو داود (٣٦٤١)، والترمذي (٢٦٨٢)، وصحَّحه الألباني في «صحيح أبي داود» (٣٦٤١)].
Abu Dardaai (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Mwenye kuifuata njia ya kuitafua ‘Ilmu, Allaah Humfanyia wepesi njia ya Jannah, na hakika ya Malaika wanagubika mbawa zao kwa mwenye kutafuta ‘Ilmu, wapo radhi kwa anayoyafanya, na hakika ‘Aalim (Mwanazuoni) anaombewa maghfira kwa aliyepo katika mbingu na ardhi hata samaki baharini, na fadhila za ‘Aalim juu ya mwenye kufanya ‘ibaadah ni kama fadhila za mwezi juu ya nyota nyengine, na hakika ya ‘Ulamaa ni warithi wa Manabii, na hakika Manabii hawarithishi dinari wala dirham, na hakika (wao) wanarithisha ‘Ilmu. Basi yeyote atakayechukua (‘Ilmu hiyo), amechukua kitu bora.)) [Imepokewa na Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd (3641)]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 17
Anayejifunza ‘Ilmu Ya Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) Kwa Ajili Ya Cheo Pekee Hatopata Harufu Ya Jannah
Alhidaaya.com [4]
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " مَنْ تَعَلَّمَ عِلْمًا مِمَّا يُبْتَغَى بِهِ وَجْهُ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ لاَ يَتَعَلَّمُهُ إِلاَّ لِيُصِيبَ بِهِ عَرَضًا مِنَ الدُّنْيَا لَمْ يَجِدْ عَرْفَ الْجَنَّةِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ " . يَعْنِي رِيحَهَا .
Abuu Huraryah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kujifunza ‘Ilmu za Allaah (عَزَّ وَجَلَّ), hajifunzi isipokuwa kupata cheo ndani ya dunia, hatoipata (hata) harufu ya Jannah (Pepo) Siku Ya Qiyaamah.” [Abuu Daawuwd]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 18
Allaah Huichukua ‘Ilmu Kwa Kufariki ‘Ulamaa
Kisha Viongozi Wajinga Watatoa Fatwa Bila ‘Ilmu
Alhidaaya.com [4]
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ، قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ " إِنَّ اللَّهَ لاَ يَقْبِضُ الْعِلْمَ انْتِزَاعًا، يَنْتَزِعُهُ مِنَ الْعِبَادِ، وَلَكِنْ يَقْبِضُ الْعِلْمَ بِقَبْضِ الْعُلَمَاءِ، حَتَّى إِذَا لَمْ يُبْقِ عَالِمًا، اتَّخَذَ النَّاسُ رُءُوسًا جُهَّالاً فَسُئِلُوا، فَأَفْتَوْا بِغَيْرِ عِلْمٍ، فَضَلُّوا وَأَضَلُّوا ".
Abdallaaah bin Amr bin Al-Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Allaah Haiondoshi ‘Ilmu kwa kuichukua kutoka kwa (mioyo ya) watu, lakini Huichukua kwa kufariki ‘Ulamaa mpaka watakapokwisha (‘Ulamaa) wote, watu watachukua kama wao viongozi wajinga ambao wataulizwa na watatoa Fatwa bila ‘Ilmu. Kwa hiyo watapotoka na watapotosha (Ummah). [Al-Bukhaariy, Muslim]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 19
Malaika Huwateremshia Mbao Zao Mtafutaji ‘Ilmu Na Wanaridhia Naye
Alhidaaya.com [4]
عَنْ زِرِّ بْنِ حُبَيْشٍ، قَالَ أَتَيْتُ صَفْوَانَ بْنَ عَسَّالٍ الْمُرَادِيَّ فَقَالَ مَا جَاءَ بِكَ قُلْتُ أُنْبِطُ الْعِلْمَ . قَالَ فَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ ـ صلى الله عليه وسلم ـ يَقُولُ " مَا مِنْ خَارِجٍ خَرَجَ مِنْ بَيْتِهِ فِي طَلَبِ الْعِلْمِ إِلاَّ وَضَعَتْ لَهُ الْمَلاَئِكَةُ أَجْنِحَتَهَا رِضًا بِمَا يَصْنَعُ " .
Zirr bin Hubaysh (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nilimwendea Swafwaan bin ‘Assaal Al-Muraadiyy akasema: Nini kilichokuleta? Nikasema: Kutafuta ‘Ilmu. Akasema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Hakuna yeyote atokaye kutoka nyumbani kwake kwa ajili ya kutafuta ‘Ilmu isipokuwa Malaika huteremsha mbawa zao wakiridhia analolifanya. “ [Ibn Maajah na ameisahihisha Imaam Al-Abaaniy: Swahiyh Ibn Maajah (186), Swahih Al-Jaami’ (5702)]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 20
Mwenye ‘Ilmu Asifiche ‘Ilmu Yake Ili Aepukane Na Lijamu La Moto
Alhidaaya.com [4]
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " مَنْ سُئِلَ عَنْ عِلْمٍ فَكَتَمَهُ أَلْجَمَهُ اللَّهُ بِلِجَامٍ مِنْ نَارٍ يَوْمَ الْقِيَامَةِ " .
Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Atakayeulizwa jambo la kuhusiana na ‘ilmu (ya Dini) lakini alifiche, atafungwa lijamu la moto Siku ya Qiyaamah.” [At-Tirmidhy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Swahiyh At-Targhiyb (120)].
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 21
Aliye Mbora Kabisa Ni Mwenye Kujifunza Na Kufundisha Qur-aan
Alhidaaya.com [4]
عن عثمانَ بن عفانَ رضي الله عنه أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلّم قالَ: ((خَيرُكُم مَنْ تعَلَّمَ القُرآنَ وعَلَّمَه)) صحيح البخاريِّ
Imepokelewa kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kwamba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mbora wenu ni yule mwenye kujifunza Qur-aan kisha akaifundisha.” [Al-Bukhaariy]
Fadhila nyenginezo tele za kujifunza na kufundisha Qur-aan zinapatikana katika viungo vifuatavyo:
Aayaat Kuhusu Fadhila Za Qur-aan Na Umuhimu Wake [25]
Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan Katika Hadiyth Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) [26]
Maamrisho Ya Kuisoma Qur-aan Na Kuifanyia Kazi [27]
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 22
Du’aa Za Kuomba Kuhusu ‘Ilmu
Alhidaaya.com [4]
عَنْ جَابِرٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ـ صلى الله عليه وسلم " سَلُوا اللَّهَ عِلْمًا نَافِعًا وَتَعَوَّذُوا بِاللَّهِ مِنْ عِلْمٍ لاَ يَنْفَعُ "
Amesimulia Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Muombeni Allaah ‘Ilmu ya kunufaisha na ombeni kinga kwa Allaah dhidi ya ‘Ilmu isiyonufaisha.” [Ibn Maajah, ameisahihisha Imaam Al-Albaaniy: Swahiyh Ibn Maajah (3114)]
Du’aa za Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Kuhusu ‘Ilmu:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ قَلْبٍ لاَ يَخْشَعُ وَمِنْ دُعَاءٍ لاَ يُسْمَعُ وَمِنْ نَفْسٍ لاَ تَشْبَعُ وَمِنْ عِلْمٍ لاَ يَنْفَعُ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَؤُلآءِ الأَرْبَعِ
Allaahumma inniy a’uwdhu bika min-qalbin-laa yakh-sha’u, wamin du’aain-laa yasma’u, wamin nafsin-laa tashba’u, wamin ilmin-laa yanfa’u, a’uwdhu bika min haaulail-arba’i
Ee Allaah, hakika mimi najikinga moyo usionyenyekea na du’aa isiyosikizwa na nafsi isiyoshiba na elimu isiyonufaisha, najikinga Kwako dhidi ya haya manne.
[Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Swahiyh An-Nasaaiy, Swahiyh Al-Jaami’ (1297)]
(الَّلهُمَّ انْفَعْنِي بِمَا عَلَّمْتَنِي وَعَلِّمْنِي مَا يَنْفَعُنِي وَزِدْنِي عِلْمًا))
Allaahumma Anfa’niy bimaa ‘Allamtaniy, wa ‘Allimniy maa yanfa’uniy wa-Zidniy ‘ilmaa.
((Ee Allaah, Ninufaishe kwa Unayonifunza, na nielimishe yatakayoninufaisha na nizidishie elimu)) [Swahiyh Ibn Maajah]
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْعَجْزِ وَالْكَسَلِ، وَالْجُبْنِ وَالْبُخْلِ، وَالْهَرَمِ وَعَذَابِ الْقَبْرِ. اللَّهُمَّ آتِ نَفْسِي تَقْوَاهَا، وَزَكِّهَا أَنْتَ خَيْرُ مَنْ زَكَّاهَا، أَنْتَ وَلِيُّهَا وَمَوْلاَهَا. اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عِلْمٍ لاَ يَنْفَعُ، وَمِنْ قَلْبٍ لاَ يَخْشَعُ، وَمِنْ نَفْسٍ لاَ تَشْبَعُ، وَمِنْ دَعْوَةٍ لاَ يُسْتَجَابُ لَهَا
Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-‘ajzi wal-kasali, wal-jubni wal-bukhli, wal-harami, wa ‘adhaabil-qabri, Allaahumma aati nafsiy taqwaahaa, wa zakkihaa Anta khayru man zakkaahaa, Anta Waliyyuhaa wa Mawlaaha. Allaahumma inniy a’uwdhu bika min ’ilmin-laa yanfa’u, wamin qalbin-laa yakhsha’u, wamin-nafsil-laa tashba’u, wamin da’-watin-laa yustajaabu lahaa
Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kushindwa hila, na uvivu, na uoga, na ubakhili, na kudhoofika [kutokana na uzee] na adhabu za kaburi. Ee Allaah, Ipe nafsi yangu taqwa yake, na Itakase kwani Wewe ni Mbora wa kuitakasa, Wewe ni Waliyyu wake na Mawlaa wake. Ee Allaah, hakika najikinga Kwako elimu isiyonufaisha, na moyo usionyeyekea na nafsi isiyoshiba, na du’aa isiyoitikiwa.
[Muslim, An-Nasaaiy , Ahmad]
عن أمِّ المؤمنين أمِّ سلمة رَضِيَ اللهُ عَنْهَا زوج النّبيّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ :"أنَّه كان يقولُ إذا صَلَّى الصُّبحَ حين يُسلِّمُ"،: "اللَّهُمَّ إنِّي أسأَلُك عِلْمًا نافعًا وَرِزْقًا طَيِّبًا ، وَعَمَلًا مُتَقَبَّلًا
Amesimulia Ummul-Muuminiyn Umm Salamah (رَضِيَ الْلَّهُ عَنْهَا) mke wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): Alikuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Anasema pindi anapomaliza kuswali asubuhi:
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ عِلْمـاً نافِعـاً وَرِزْقـاً طَيِّـباً، وَعَمَـلاً مُتَقَـبَّلاً
Allaahumma inniy as-aluka ‘ilman naafi’an warizqan twayyiban wa ‘amalam mutaqabbalan.
Ee Allaah, hakika nakuomba elimu yenye kunufaisha na rizki njema na amali zenye kutakabaliwa [Ibn Maajah [925], Taz Swahiyh Ibn Maajah (1/152)].
Pindi hali inapokuwa ngumu:
اللّهُـمَّ لا سَـهْلَ إِلاّ ما جَعَلـتَهُ سَهـلاً، وَأَنْتَ تَجْـعَلُ الْحَـزَنَ إِذا شِـئْتَ سَهـْلاً
Allaahumma laa sahla illaa maa Ja’altahu sahlan wa Anta Taj-’alul-hazna idhaa shi-ita sahlaa
Ee Allaah hakuna jepesi ila Ulilolifanya jepesi, Nawe Unalifanya (lilokuwa) gumu (liwe) jepesi Ukitaka [Hadiyth ya Anas bin Maalik (رضي الله عنه) - Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake [2427]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/279
[2] http://www.alhidaaya.com
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10882&title=Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%20-%20%20%D8%A3%D9%8E%D8%AD%D8%A7%D8%AF%D9%8A%D8%AB%D9%8F%20%D8%B9%D9%8E%D9%86%D9%92%20%D9%81%D9%8E%D8%B6%D9%92%D9%84%D9%90%20%D8%A7%D9%84%D9%92%D8%B9%D9%90%D9%84%D9%92%D9%85%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%84%D9%92%D8%B9%D9%8F%D9%84%D9%8E%D9%85%D9%8E%D8%A7%D8%A1
[4] http://www.alhidaaya.com/sw/
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10883&title=01-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Kutafuta%20%27Ilmu%20Ni%20Fardhi%20Kwa%20Kila%20Muislaam
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10884&title=02-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Allaah%20Atamsahilishia%20Mwenye%20Kutafuta%20%27Ilmu%20Njia%20Ya%20Kuingia%20Jannah
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10885&title=03-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Allaah%20Akimtakia%20Mja%20Wake%20Kheri%20Humjaali%20Ufaqahi%20Wa%20Dini
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10886&title=04-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Anayeongoza%20Katika%20Kheri%20Atapata%20Ujira%20Wa%20Mwenye%20Kutekeleza%20Kheri%20Hiyo
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10887&title=05-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Vikao%20Vya%20%E2%80%98Ilmu%20Huteremkiwa%20Utulivu%2C%20Hufunikwa%20Rahma%2C%20Malaika%20Huwazunguka%20Na%20Allaah%20Huwataja
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10888&title=06-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20%E2%80%98Ilmu%20Ni%20Kama%20Mfano%20Wa%20Ardhi%20Yenye%20Rutuba%20Inayonufaisha%20Watu
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10889&title=07-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Mtu%20Mmoja%20Akiongoka%20Ni%20Bora%20Kuliko%20Kupata%20Ngamia%20Mwekundu
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10890&title=08-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Balighisheni%20Japo%20Aayah%20Moja%20%20
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10891&title=09-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20%E2%80%98Ilmu%20Inayonufaisha%20Inaendelea%20Kumpatia%20Thawabu%20Mtu%20Baada%20Ya%20Kufariki
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10892&title=10-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Dunia%20Imelaaniwa%20Isipokuwa%20Matatu%20Dhikru-Allaah%20%E2%80%98Aalim%20Na%20Mwanafunzi
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10893&title=11-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Allaah%20Amneemeshe%20Mtu%20Anayebalighisha%20Risala%20Kama%20Alivyosikia
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10894&title=12-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Aliyekuwa%20Umahiri%20Wa%20Qur-aan%20Yupamoja%20Na%20Malaika%20Anayejifunza%20Ana%20Thawabu%20Mara%20Mbili
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10895&title=13-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Ubora%20Wa%20%E2%80%98Aalim-%20Allaah%20Na%20Viumbe%20Wote%20Wanamuombea%20Mwenye%20Kufundisha%20Khayr
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10896&title=14-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Anayejifunza%20Au%20Kufundisha%20%E2%80%98Ilmu%20Msikitini%20Yuko%20Katika%20Daraja%20La%20Mujaahid%20Fiy%20SabiliLLaah
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10897&title=15-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Husda%20Imeruhusika%20Kwa%20Aliyejaaliwa%20%E2%80%98Ilmu%20Akaifanyia%20Kazi%20Na%20Kuifundisha
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10898&title=16-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Fadhila%20Za%20%E2%80%98Aalim%20Na%20%E2%80%98Ulamaa%20Ni%20Warithi%20Wa%20Manabii
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10899&title=17-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Anayejifunza%20%E2%80%98Ilmu%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Cheo%20Pekee%20Hatopata%20Harufu%20Ya%20Jannah
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10900&title=18-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Allaah%20Huichukua%20%E2%80%98Ilmu%20Kwa%20Kufariki%20%E2%80%98Ulamaa%20Kisha%20Viongozi%20Wajinga%20Watatoa%20Fatwa%20Bila%20%E2%80%98Ilmu
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10903&title=19-Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Malaika%20Huwateremshia%20Mbao%20Zao%20Mtafutaji%20%E2%80%98Ilmu%20Na%20Wanaridhia%20Naye
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10904&title=20-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Mwenye%20%E2%80%98Ilmu%20Asifiche%20%E2%80%98Ilmu%20Yake%20Ili%20Aepukane%20Na%20Lijamu%20La%20Moto
[25] http://www.alhidaaya.com/sw/node/9572
[26] http://www.alhidaaya.com/sw/node/50
[27] http://www.alhidaaya.com/sw/node/9573
[28] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10905&title=21-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Aliye%20Mbora%20Kabisa%20Ni%20Mwenye%20Kujifunza%20Na%20Kufundisha%20Qur-aan
[29] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10906&title=22-Hadiyth%3A%20Fadhila%20Za%20%27Ilmu%20Na%20%27Ulamaa%3A%20Du%E2%80%99aa%20Za%20Kuomba%20Kuhusu%20%E2%80%98Ilmu