Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
01-Miujiza Yake: Ni Mingi Muujiza Mkubwa Kabisa Ni Qur-aan
Alhidaaya.com [4]
Miujiza ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika Siyrah yake ni mingi mno kama itakavyobainishwa katika makala zijazo na Muujiza mkubwa kabisa ni Qur-aan ambayo Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) Anasema:
وَإِنَّهُ لَكِتَابٌ عَزِيزٌ﴿٤١﴾ لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ ۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ﴿٤٢﴾
Na hakika hicho ni Kitabu chenye utukufu na udhibiti. Hakitokifikia ubatili mbele yake, na wala nyuma yake; ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hikmah wa yote, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote. [Fusw-Swilat: 41 – 42]
Na katika Hadiyth amethibitisha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ):
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " مَا مِنَ الأَنْبِيَاءِ نَبِيٌّ إِلاَّ أُعْطِيَ مَا مِثْلُهُ آمَنَ عَلَيْهِ الْبَشَرُ، وَإِنَّمَا كَانَ الَّذِي أُوتِيتُ وَحْيًا أَوْحَاهُ اللَّهُ إِلَىَّ فَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَكْثَرَهُمْ تَابِعًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ".
AmesimuliaAbuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna Nabiy katika Manabii ila alipewa miujiza ambayo watu wanaiamini. Kwa hakika nilichopewa mimi ni Wahyi aliouleta Allaah kwangu. Kwa hiyo, ninataraji nitawapiku kwa wingi wa wafuasi Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Bila shaka Qur-aan Tukufu ni muujiza mkubwa kabisa ambao wana-Aadam ulimwenguni wameujua kwani ndio muujiza pekee uliobakia na utaendelea kubakia hadi Siku ya Qiyaamah kwa sababu Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ndiye Nabiy wa mwisho na Risala yake ni Risala ya mwisho na ya kudumu hadi Siku ya Qiyaamah wala hakuna atakayeweza kudai anayo mfano wa Qur-aan, wala hata kuleta Aayah au kidogo tu kulikoni Aayah, Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) Anahakikisha hivyo pindi Anavosema:
قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا ﴿٨٨﴾
Sema: Ikiwa watajumuika wana Aadam na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan; hawatoweza kuleta mfano wake na japokuwa watasaidiana wao kwa wao. [Al-Israa: 88]
Bali Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) Anatoa changamoto ya mustahili ambayo kuanzia mwanzo wake hadi Siku ya Qiyaamah hakuna atakayeweza kuleta Suwrah moja au zaidi yake; Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٣﴾
Na ikiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya mja Wetu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi leteni Suwrah mfano wake, na waiteni mashahidi wenu pasipo na Allaah mkiwa ni wakweli. [Al-Baqarah: 23]
Na pia Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِعَشْرِ سُوَرٍ مِّثْلِهِ مُفْتَرَيَاتٍ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿١٣﴾
Je, wanasema Ameitunga (hii Qur-aan)? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Leteni Suwrah kumi mfano wake zilizotungwa, na iteni muwawezao (wakusaidieni) pasina Allaah mkiwa ni wakweli. [Huwd: 13]
Na pia Kauli Yake Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
أَمْ يَقُولُونَ تَقَوَّلَهُ ۚ بَل لَّا يُؤْمِنُونَ ﴿٣٣﴾ فَلْيَأْتُوا بِحَدِيثٍ مِّثْلِهِ إِن كَانُوا صَادِقِينَ ﴿٣٤﴾
Au wanasema ameibuni (Qur-aan)? Bali hawaamini. Basi walete kauli mfano wake wakiwa ni wakweli. [Atw-Twuwr: 33 – 34]
Kwanini Qur-aan Ni Muujiza Mkubwa:
Basi makafiri wangapi wameingia Uislamu kwa kutambua miujiza iliyomo ndani ya Qur-aan na itaendelea Qur-aan kuwashangaza wana-Aadam na kuwabainikia wenye kutaka kuongoka hadi Siku ya Qiyaamah mijuza ya Aayaat za Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) kama Anavyosema Mwenyewe Allaah (عَزَّ وَجَلَّ):
سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الْآفَاقِ وَفِي أَنفُسِهِمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ الْحَقُّ ۗ أَوَلَمْ يَكْفِ بِرَبِّكَ أَنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ﴿٥٣﴾
Tutawaonyesha Aayaat (ishara, dalili) Zetu katika peo za mbali na katika nafsi zao, mpaka iwabainikie kwamba hiyo ni haki! Je, haitoshelezi Rabb wako kuwa Yeye ni Shahidi juu ya kila kitu? [Fusw-Swilat: 53]
Miujiza ndani ya Qu-raan pekee inaweza kupindukia maelfu na inahitaji mijalada na mijalada ya Vitabu kuitaja na kuibainisha miujiza hiyo iliyomo ndani ya Muujiza huo mkubwa wa Qur-aan.
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
02-Miujiza Yake: Muujiza Wa Al-Israa Wal-Mi’raaj
Alhidaaya.com [4]
Muujiza wa Al-Israa wal Mi’raaj ni muujiza mwengineo mkubwa katika miujiza ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم). Tukio la Israa wal Mi’raaj halikuwa ni tukio la kawaida bali lilikuwa ni tukio la muujiza adhimu ambao umedhihirisha Utukufu usio na mithali, na Uwezo mkubwa wa Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى). Alimwongoza Rasuli Wake (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na Akadhihirisha dalili mojawapo ya Unabiy wake kwa watu khasa washirikina wa Makkah ambao hawakumwamini bali walimkanusha na kumtesa na kumdhikisha kutokana na Risala yake aliyotakiwa na Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) Aibalighishe kwao.
Ni muujiza mashuhuri unaotambulikana na walimwengu kutokana na ajabu ya muujiza huu wa kuweza kusafirishwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) katika safari ya usiku mmoja kutoka Makkah kupita Baytul-Maqdis (Jerusalem), kisha kufikia mbingu ya saba na kurudi Makkah siku hiyo hiyo.
Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١﴾
Utakasifu ni wa Ambaye Amemsafirisha usiku mja Wake kutoka Al-Masjid Al-Haraam mpaka Al-Masjid Al-Aqswaa ambao Tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake; ili Tumuonyeshe baadhi ya Aayaat (miujiza, ishara, dalili) Zetu. Hakika Yeye (Allaah) ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. [Al-Israa: 1]
Al-Israa wal Mi’raaj ni tukio ambalo limempatia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) hadhi kubwa ulimwenguni, hadhi ya kumfikisha mahali ambako hakuna mwana-Aadam aliyewahi kufikia nako ni Sidrat Al-Muntahaa huko mbingu ya saba.
Al-Israa wal Mi’raaj ni muujiza ambao wana-Aadam wamestaabishwa na wengine kuduwaa kwa kutafakari jinsi gani inawezekana safari ya mtu kwa usiku mmoja kusafiri mji hadi mji, kisha mpaka kupanda mbinguni na kufikia mbingu ya saba na kuongea na Rabb wake. Wanaoitilia shaka ni makafiri, ama Waumini hawana shaka nayo safari hiyo kwa sababu Iymaan zao zimethibiti katika kila jambo alokuja nalo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم). Juu ya hivyo imetajwa na Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) Ambaye ni Al-Qaadir (Mweza wa kila kitu) katika Qur-aan Anaposema:
وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ ﴿١٣﴾ عِندَ سِدْرَةِ الْمُنتَهَىٰ ﴿١٤﴾ عِندَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَىٰ ﴿١٥﴾ إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ ﴿١٦﴾ مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ ﴿١٧﴾ لَقَدْ رَأَىٰ مِنْ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَىٰ ﴿١٨﴾
Na kwa yakini amemuona (Jibriyl) katika uteremko mwingine. Kwenye mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa. Karibu yake kuna Jannah ya Al-Ma-waa. Ulipoufunika mkunazi huo unachokifunika. Jicho lake halikukengeuka wala halikupinduka mipaka. Kwa yakini aliona miongoni mwa Aayaat (ishara, dalili) za Rabb wake kubwa kabisa. [An-Najm: 13- 18]
Matukio yafuatayo kwa kifupi yalitokea katika safari hiyo kuu ya Israa wal Mi’raaj:
1-Safari ya usiku mmoja kuanzika Masjid Al-Haram Makkah kupitia Baytul-Maqdis Jerusalem, kupanda mbinguni hadi mbingu ya saba na kuongea na Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى).
2-Kuwasalisha Manabii wote pindi alipofika Baytul-Maqdis.
3-Katika kila mbingu alionana na Manabii; Aadam, ‘Iysaa na Yahyaa, Yuwsuf, Idriys, Haaruwn, Muwsaa, (عَلَيْهِم السَّلام) hadi kumfikia Nabiy Ibraahiym (عَلَيْهِ السَّلام) ambaye alikuwa mbingu ya saba.
3-Alipokutana na Nabiy Muwsaa (عَلَيْهِ السَّلام) mbingu ya sita alimnasihi arudi kwa Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) ili amuombe Ampunguzie idadi za Swalaah aliyofaridhishwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na Ummah wake kuanzia khamsini kwa siku hadi kufikia tano kwa siku.
4-Jibriyl alipofikia Sidrat Al-Muntahaa huko mbingu ya saba, alimwacha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) aendelee akaongea na Allaah (عَزَّ وَجَلَّ), ilhali yeye Jibriyl (عَلَيْهِ السَّلام) alibakia nyuma.
4-Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) Alifaridhisha nguzo ya Kiislaam ambayo ni Swalaah tano kwa siku.
5-Neema za Jannah (Pepo) alizoziona Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akanusa harufu yake.
6-Kuona kwake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) Moto wa Jahannam na matukio mbalimbali aliyoyaona, yaliyothibiti katika Hadiyth za Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم), yakiwemo adhabu za watu wa matendo mbali mbali ya madhambi kama kula ribaa, ghiybah (kusengenya), wazinifu n.k.
7-Baada ya kurudi Makkah, washirikina wa Makkah kutokumwamini Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم).
8-Abu Bakr Asw-Swiddiyq alimwamini mojamoja kwa moja na ndipo alipopata laqab yake hiyo ya Asw-Swiddiyq (mkweli).
Kwa faida nyenginezo bonyeza viungo vifuatavyo:
Tukio la Israa Na Mi'iraaj [6]
Muujiza Wa Al-Israa Wal-Mi'raaj Na Mafunzo Yake [7]
Israa Na Mi'iraaj: Kisa Cha Abu Bakr Asw-Swiddiyq (رضي الله عنه) [8]
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
03-Miujiza Yake: Kupasuka Mwezi
Alhidaaya.com [4]
Quraysh wa Makkah katika inadi zao walimtaka Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) awaonyeshe muujiza, basi Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) Akaleta muujiza wa kupasuka mwezi mbele ya macho yao, lakini kama kawaida yao waliendelea kumfanyia inadi na istihzai. Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿١﴾ وَإِن يَرَوْا آيَةً يُعْرِضُوا وَيَقُولُوا سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ ﴿٢﴾
Saa imekaribia na mwezi umepasuka. Na wanapoona Aayah (ishara, dalili) hukengeuka na husema: Sihiri inayoendelea [Al-Qamar: 1-2]
Na Hadiyth zifuatazo pia zinaelezea tukio hilo la muujiza wa kupasuka mwezi:
عَنْ أَنَسٍ، قَالَ سَأَلَ أَهْلُ مَكَّةَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم آيَةً فَانْشَقَّ الْقَمَرُ بِمَكَّةَ مَرَّتَيْنِ فَنَزَلَت: ((اقتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانْشَقَّ الْقَمَرُ)) إِلَى قَوْلِهِ : ((سحْرٌ مُسْتَمِرٌّ)) يَقُولُ ذَاهِبٌ . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ .
Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) kwamba watu wa Makkah walimuomba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) awaletee Aayah (Ishara, muujiza), basi mwezi ukapasuka Makkah mara mbili (Yaani sehemu mbili), kisha ikateremka:
اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿١﴾
Saa imekaribia na mwezi umepasuka
Mpaka kauli Yake:
سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ
Na pia,
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ انْشَقَّ الْقَمَرُ وَنَحْنُ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم بِمِنًى فَقَالَ " اشْهَدُوا ". وَذَهَبَتْ فِرْقَةٌ نَحْوَ الْجَبَلِ
Amesimulia ‘Abdallaah bin Mas‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Mwezi ulipasuka (na kuwa vipande viwili) wakati tukiwa pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) huko Minaa. Akasema, "Shuhudieni." Kisha kipande cha mwezi kikaelekea upande wa mlima. [Al-Bukhaariy]
Na pia,
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ انْشَقَّ الْقَمَرُ وَنَحْنُ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَصَارَ فِرْقَتَيْنِ، فَقَالَ لَنَا " اشْهَدُوا، اشْهَدُوا ".
Amesimulia ‘Abdallaah bin Mas‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Ulipasuka mwezi wakati wa uhai wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) vipande viwili akatuambia: “Shuhudieni! Shuhudieni! [Al-Bukhaariy]
Na pia,
عَنْ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ، قَالَ: انْشَقَّ الْقَمَرُ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللَّهِ ﷺ فَصَارَ فِرْقَتَيْنِ: فِرْقَةٌ عَلَى هَذَا الْجَبَلِ، وَفِرْقَةٌ عَلَى هَذَا الْجَبَلِ، فَقَالُوا: سَحَرَنَا مُحَمَّدٌ. فَقَالُوا: إِنْ كَانَ سَحَرَنَا فَإِنَّهُ لَا يَسْتَطِيعُ أَنْ يَسْحَرَ النَّاسَ كُلَّهُمْ.
Jubayr bin Mutw'im (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alisema: "Mwezi ulipasuka vipande viwili zama za Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na sehemu ya mwezi ulikuwa juu ya mlima na sehemu nyingine kwenye mlima mwingine. Wakasema (makafiri) "Muhammad ametufanyia sihri (uchawi)". Kisha wakasema: "Angeliweza kututeka kwa sihri asingeliweza kufanya kwa watu wote" [Imaam Ahmad]
Na Riwaayah nyenginezo kama hizo zimethibiti pia.
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
04-Miujiza Yake: Wanyama Kuzungumza Na Swahaba
Alhidaaya.com [4]
Miongoni mwa miujiza yake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) ni kwamba baadhi ya Wanyama walizungumza na wana-Aadam; mmojawapo ni mbwa mwitu aliyezungumza na Swahaba karibu na mji wa Madiynah kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنَا يَزِيدُ، أَخْبَرَنَا الْقَاسِمُ بْنُ الْفَضْلِ الْحُدَّانِيُّ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ قَالَ: عَدَا الذِّئْبُ عَلَى شَاةٍ فَأَخَذَهَا، فَطَلَبَهُ الرَّاعِي، فَانْتَزَعَهَا مِنْهُ فَأَقْعَى الذِّئْبُ عَلَى ذَنَبِهِ قَالَ: أَلَا تَتَّقِي اللَّهَ تَنْزِعُ مِنِّي رِزْقًا سَاقَهُ اللَّهُ إِلَيَّ. فَقَالَ: يَا عَجَبِي ذِئْبٌ مُقْعٍ عَلَى ذَنَبِهِ يُكَلِّمُنِي كَلَامَ الْإِنْسِ. فَقَالَ الذِّئْبُ: أَلَا أُخْبِرُكَ بِأَعْجَبَ مِنْ ذَلِكَ، مُحَمَّدٌ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِيَثْرِبَ، يُخْبِرُ النَّاسَ بِأَنْبَاءِ مَا قَدْ سَبَقَ. قَالَ: فَأَقْبَلَ الرَّاعِي يَسُوقُ غَنَمَهُ حَتَّى دَخَلَ الْمَدِينَةَ، فَزَوَاهَا إِلَى زَاوِيَةٍ مِنْ زَوَايَاهَا، ثُمَّ أَتَى رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَخْبَرَهُ فَأَمَرَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَنُودِيَ: الصَّلَاةُ جَامِعَةٌ، ثُمَّ خَرَجَ فَقَالَ لِلرَّاعِي: أَخْبِرْهُمْ فَأَخْبَرَهُمْ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: صَدَقَ وَالَّذِي نَفْسِي، بِيَدِهِ لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يُكَلِّمَ السِّبَاعُ الْإِنْسَ، وَيُكَلِّمَ الرَّجُلَ عَذَبَةُ سَوْطِهِ، وَشِرَاكُ نَعْلِهِ، وَيُخْبِرَهُ فَخِذُهُ بِمَا أَحْدَثَ أَهْلُهُ بَعْدَهُ. روى الإمام أحمد في مسنده (3/ 83 - 84
Amesimulia Abu Sa'iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kwamba: Mchunga kondoo alipokuwa na kondoo zake, mara mbwa mwitu alimshambulia kondoo na kuondoka naye, mchunga kondoo akamkimbiza mbwa mwitu na akamrejesha kondoo, mbwa mwitu akakalia mkia wake na akamwambia mchunga kondoo: "Mche Allaah! Umechukua rizqi yangu Alonijaalia Allaah!” Mchunga kondoo akasema: "Ajabu! Mbwa mwitu anakalia mkia wake na kuzungumza na mimi kwa lugha ya kibin-Aadam." Mbwa mwitu akasema: "Je nikuambie jambo la ajabu zaidi kuliko hilo? Yupo Muhammad (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) huko Yathrib (Al-Madiynah) akiwajulisha watu kuhusu khabari za kale." Basi mchunga kondoo akaenda (upande wa Al-Madiynah) huku akiwaswaga kondoo wake mpaka akafika Al-Madiynah, akawazuia kondoo wake mahali, na akaja kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na kusimulia kisa chote. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akaamuru iadhiniwe Adhaan ya Swalaah ya Jamaa, kisha akatoka na kumwomba mchunga kondoo awaambie watu na akawaambia. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akasema: "Amesema kweli. Naapa kwa Ambaye Mikononi Mwake ipo nafsi yangu, Siku ya Qiyaamah haitasimama isipokuwa mpaka wanyama wawindao wazungumze na wana-Aadam, na fimbo na kamba za viatu za mtu zizungumze naye na paja lake kumjulisha kuhusu familia yake yaliyowatokea nyuma yake. [Musnad Imaam Ahmad (3: 83 - 84)].
Na pia ng’ombe alizungumza kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنَا أَبُو الْيَمَانِ، أَخْبَرَنَا شُعَيْبٌ، عَنِ الزُّهْرِيِّ، قَالَ أَخْبَرَنِي أَبُو سَلَمَةَ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، أَنَّ أَبَا هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ " بَيْنَمَا رَاعٍ فِي غَنَمِهِ عَدَا عَلَيْهِ الذِّئْبُ، فَأَخَذَ مِنْهَا شَاةً، فَطَلَبَهُ الرَّاعِي، فَالْتَفَتَ إِلَيْهِ الذِّئْبُ فَقَالَ مَنْ لَهَا يَوْمَ السَّبُعِ، يَوْمَ لَيْسَ لَهَا رَاعٍ غَيْرِي، وَبَيْنَا رَجُلٌ يَسُوقُ بَقَرَةً قَدْ حَمَلَ عَلَيْهَا، فَالْتَفَتَتْ إِلَيْهِ فَكَلَّمَتْهُ فَقَالَتْ إِنِّي لَمْ أُخْلَقْ لِهَذَا، وَلَكِنِّي خُلِقْتُ لِلْحَرْثِ ". قَالَ النَّاسُ سُبْحَانَ اللَّهِ. قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " فَإِنِّي أُومِنُ بِذَلِكَ وَأَبُو بَكْرٍ وَعُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ رضى الله عنهما ".
Amesimulia Abu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akisema, "Mchunga kondoo alipokuwa na kondoo zake, mbwa mwitu alimvamia na kumchukua kondoo mmoja. Mchunga kondoo alipomkimbiza mbwa mwitu, mbwa mwitu alimgeukia na kumwambia, ‘Nani atakayewalinda katika siku ya wanyama mwitu ambapo hakutakuwa na mchungaji isipokuwa mimi’. Na wakati mtu mmoja alipokuwa akimswaga ng’ombe huku akiwa amembebesha mzigo, alimgeukia na kuzungumza naye akisema, ‘Sikuumbwa kwa ajili hii (yaani, kubeba mzigo), bali kwa ajili ya kulima.’" Watu wakasema, "Subhaana Allaah." Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akasema, "Hakika Ninaapa yaamini hayo na pia Abu Bakr na ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا)” [Al-Bukhaariy]
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
05-Miujiza Yake: Kuteremshwa Mvua Tele Kwa Du’aa Yake
Alhidaaya.com [4]
Miongoni mwa miujiza aliyojaaliwa nayo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na Rabb wake ni du’aa zake, kwani alikuwa pindi alipoomba jambo basi halirudi bali hutaqabaliwa na hutaqabaliwa kwa miujiza ya kutoka mbinguni. Watu walipolalamika kuwa kuna ukame wakaomba mvua, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) aliomba du’aa kwa Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) Ateremshe mvua, basi naam! Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) Aliteremsha na hali ilikuwa kama inavoelezewa katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّ رَجُلاً، دَخَلَ الْمَسْجِدَ يَوْمَ جُمُعَةٍ مِنْ بَابٍ كَانَ نَحْوَ دَارِ الْقَضَاءِ، وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَائِمٌ يَخْطُبُ، فَاسْتَقْبَلَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَائِمًا ثُمَّ قَالَ: "يَا رَسُولَ اللَّهِ هَلَكَتِ الأَمْوَالُ وَانْقَطَعَتِ السُّبُلُ، فَادْعُ اللَّهَ يُغِيثُنَا" فَرَفَعَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَدَيْهِ ثُمَّ قَالَ: ((اللَّهُمَّ أَغِثْنَا، اللَّهُمَّ أَغِثْنَا، اللَّهُمَّ أَغِثْنَا)). قَالَ أَنَسٌ: وَلاَ وَاللَّهِ مَا نَرَى فِي السَّمَاءِ مِنْ سَحَابٍ، وَلاَ قَزَعَةً، وَمَا بَيْنَنَا وَبَيْنَ سَلْعٍ مِنْ بَيْتٍ وَلاَ دَارٍ. قَالَ فَطَلَعَتْ مِنْ وَرَائِهِ سَحَابَةٌ مِثْلُالتُّرْسِ، فَلَمَّا تَوَسَّطَتِ السَّمَاءَ انْتَشَرَتْ ثُمَّ أَمْطَرَتْ، فَلاَ وَاللَّهِ مَا رَأَيْنَا الشَّمْسَ سِتًّا، ثُمَّ دَخَلَ رَجُلٌ مِنْ ذَلِكَ الْبَابِ فِي الْجُمُعَةِ وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَائِمٌ يَخْطُبُ، فَاسْتَقْبَلَهُ قَائِمًا فَقَالَ: "يَا رَسُولَ اللَّهِ هَلَكَتِ الأَمْوَالُ وَانْقَطَعَتِ السُّبُلُ، فَادْعُ اللَّهَ يُمْسِكْهَا عَنَّا". قَالَ: فَرَفَعَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَدَيْهِ ثُمَّ قَالَ: ((اللَّهُمَّ حَوَالَيْنَا وَلاَ عَلَيْنَا، اللَّهُمَّ عَلَى الآكَامِ وَالظِّرَابِ وَبُطُونِ الأَوْدِيَةِ وَمَنَابِتِ الشَّجَرِ)) قَالَ: فَأَقْلَعَتْ وَخَرَجْنَا نَمْشِي فِي الشَّمْسِ. قَالَ شَرِيكٌ: سَأَلْتُ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ أَهُوَ الرَّجُلُ الأَوَّلُ فَقَالَ مَا أَدْرِي.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kwamba mtu mmoja aliingia Masjid siku ya Ijumaa kupitia mlango ulioelekea Daar Al-Qadhwaa na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alikuwa amesimama akikhutubia. Akasimama mbele ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) kisha akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Wanyama wameteketea na njia zimekatika, basi muombe Allaah Atuteremshie mvua.” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akanyanyua mikono akaomba:
اللَّهُمَّ أَغِثْنَا، اللَّهُمَّ أَغِثْنَا، اللَّهُمَّ أَغِثْنَا
Allaahumma Aghithnaa, Allaahumma Aghithnaa, Allaahumma Aghithnaa
Ee Allaah tubarikie kwa mvua
Anas amesema: Wa-Allaahi hakukuwa na mawingu mbinguni na hakukuwa na nyumba au jengo baina yetu na baina ya mlima wa Sal’i. Basi wingu kubwa kama ngao lilitokea nyuma yake. Lilipofika katikati lilienea kisha ikanyesha mvua. Basi wa-Allaahi, hatukuona jua siku sita. Kisha Ijumaa iliyofuatia aliingia mtu kupitia mlango huo huo na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alikuwa akikhutubia khutbah ya Ijumaa, akasimama mbele yake akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Mifugo ya nyama inateketea na njia zimekatika, muombe Allaah Atuzuilie mvua!” Anas akasema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akanyanyua mikono yake akaomba:
اللَّهُمَّ حَوَالَيْنَا وَلاَ عَلَيْنَا
Allaahumma hawaalaynaa walaa ‘alaynaa.”
Ee Allaah! Pembezoni mwetu na si juu yetu.
Eee Allaah juu ya majabali, na vilimani, na ndani ya mabonde na juu ya sehemu zinazoota miti.”
Anas akasema: Mvua ikasita na tukatoka tukitembea katika jua. Shariyk alimuuliza Anas kama huyo mtu alikuwa ni yule yule wa kwanza? Akajibu kuwa hajui. [Al-Bukhaariy, Kitaab Al-Istisqaa]
Na ndio maana Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akatunfundisha du’aa zifuatazo zinazohusiana na kuomba mvua hadi inaponyesha.
063-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Istisqaa (Kuomba Mvua) [12]
064-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Mvua Inaponyesha [13]
064-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Mvua Inaponyesha [13]
066-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kutaka Mvua Iondoke (Wakati Itakapoleta Madhara) [14]
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
06-Miujiza Yake: Vidole Vyake Kutoa Maji Tele
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth kadhaa zimethibiti kuhusu muujiza wa kutoka maji tele katika vidole vya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم); miongoni mwazo ni zifuatazo:
Hadiyth Ya 1:
حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي عَدِيٍّ، عَنْ سَعِيدٍ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَنَسٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ أُتِيَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بِإِنَاءٍ وَهْوَ بِالزَّوْرَاءِ، فَوَضَعَ يَدَهُ فِي الإِنَاءِ، فَجَعَلَ الْمَاءُ يَنْبُعُ مِنْ بَيْنِ أَصَابِعِهِ، فَتَوَضَّأَ الْقَوْمُ. قَالَ قَتَادَةُ قُلْتُ لأَنَسٍ كَمْ كُنْتُمْ قَالَ ثَلاَثَمِائَةٍ، أَوْ زُهَاءَ ثَلاَثِمِائَةٍ.
Amesimulia Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Bakuli la maji ililetwa kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alipokuwa Az-Zawraai. Alitia mkono wake ndani yake, maji yakaanza kutoka vidoleni mwake. Watu wote walitawadha (na maji hayo). Qataadah alimuuliza Anas: “Mlipokuwa wangapi?” Akasema: “Mia tatu au karibu na mia tatu”. [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Fadhila Za Nabiy Na Ubora Wa Swahaba]
Hadiyth Ya 2:
حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ الْمُثَنَّى، حَدَّثَنَا أَبُو أَحْمَدَ الزُّبَيْرِيُّ، حَدَّثَنَا إِسْرَائِيلُ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ كُنَّا نَعُدُّ الآيَاتِ بَرَكَةً وَأَنْتُمْ تَعُدُّونَهَا تَخْوِيفًا، كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي سَفَرٍ فَقَلَّ الْمَاءُ فَقَالَ " اطْلُبُوا فَضْلَةً مِنْ مَاءٍ ". فَجَاءُوا بِإِنَاءٍ فِيهِ مَاءٌ قَلِيلٌ، فَأَدْخَلَ يَدَهُ فِي الإِنَاءِ، ثُمَّ قَالَ " حَىَّ عَلَى الطَّهُورِ الْمُبَارَكِ، وَالْبَرَكَةُ مِنَ اللَّهِ " فَلَقَدْ رَأَيْتُ الْمَاءَ يَنْبُعُ مِنْ بَيْنِ أَصَابِعِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم، وَلَقَدْ كُنَّا نَسْمَعُ تَسْبِيحَ الطَّعَامِ وَهْوَ يُؤْكَلُ.
Amesimulia ‘Abdullaah (رضي الله عنه): Tulikuwa tukichukulia miujiza kuwa ni Baraka ya Allaah, lakini nyinyi mnachukulia kuwa ni onyo na tahadhari. Wakati mmoja tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) safarini, nasi tukapungukiwa na maji. Akasema: “Nileteeni maji mliyo nayo.” Watu walileta chombo kilichokuwa na maji kidogo. Alitia mkono wake ndani yake, akasema: “Njooni kwenye maji ya Baraka na Baraka inatoka kwa Allaah.” Niliyaona maji yakitoka kutoka kwenye vidole vya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Na kwa hakika tulikuwa tunasikia chakula kikileta Tasbiyh (Subhaana Allaah) kilipokuwa kinaliwa na yeye. [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Fadhila Za Nabiy Na Ubora Wa Swahaba]
Hadiyth Ya 3:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، قَالَ أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنْ إِسْحَاقَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي طَلْحَةَ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّهُ قَالَ رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَحَانَتْ صَلاَةُ الْعَصْرِ، فَالْتَمَسَ النَّاسُ الْوَضُوءَ فَلَمْ يَجِدُوهُ، فَأُتِيَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِوَضُوءٍ، فَوَضَعَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي ذَلِكَ الإِنَاءِ يَدَهُ، وَأَمَرَ النَّاسَ أَنْ يَتَوَضَّئُوا مِنْهُ. قَالَ فَرَأَيْتُ الْمَاءَ يَنْبُعُ مِنْ تَحْتِ أَصَابِعِهِ حَتَّى تَوَضَّئُوا مِنْ عِنْدِ آخِرِهِمْ
Amesimulia Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Nilimuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) wakati ambapo Swalaah ya Alasiri ilikuwa imekaribia. Watu wakawa wanatafuta maji kwa ajili ya kushika wudhu lakini hawakuweza kupata (maji). Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) aliletewa maji, naye Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akatia mkono wake katika chombo hicho cha maji, kisha akawaamuru watu washike wudhu kwa maji hayo. Niliona maji yakitoka chini ya vidole vyake na watu wakaanza kuchukua wudhu mpaka wote wakamaliza kushika wudhu. [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Fadhila Za Nabiy Na Ubora Wa Swahaba]
Hadiyth Ya 4:
حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ إِسْمَاعِيلَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ مُسْلِمٍ، حَدَّثَنَا حُصَيْنٌ، عَنْ سَالِمِ بْنِ أَبِي الْجَعْدِ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ ـ رضى الله عنهما ـ قَالَ عَطِشَ النَّاسُ يَوْمَ الْحُدَيْبِيَةِ، وَالنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بَيْنَ يَدَيْهِ رَكْوَةٌ فَتَوَضَّأَ فَجَهَشَ النَّاسُ نَحْوَهُ، فَقَالَ " مَا لَكُمْ ". قَالُوا لَيْسَ عِنْدَنَا مَاءٌ نَتَوَضَّأُ وَلاَ نَشْرَبُ إِلاَّ مَا بَيْنَ يَدَيْكَ، فَوَضَعَ يَدَهُ فِي الرَّكْوَةِ فَجَعَلَ الْمَاءُ يَثُورُ بَيْنَ أَصَابِعِهِ كَأَمْثَالِ الْعُيُونِ، فَشَرِبْنَا وَتَوَضَّأْنَا. قُلْتُ كَمْ كُنْتُمْ قَالَ لَوْ كُنَّا مِائَةَ أَلْفٍ لَكَفَانَا، كُنَّا خَمْسَ عَشْرَةَ مِائَةً.
Amesimulia Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “Watu walishikwa na kiu siku ya Hudaybiyah. Chombo kidogo kilichokuwa na maji kidogo kilikuwa mbele ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na alipomaliza kutawadha, watu walikimbilia kwake. Akauliza: “Mna nini?” Wakasema: “Sisi hatuna maji ya kutawadhia au ya kunywa isipokuwa yaliyo mbele yako.” Basi alitia mkono wake kwenye chombo hicho, maji yakaanza kutoka kwenye vidole vyake kama mfano wa kijito. Sote tulikunywa na kutawadha (kwa maji hayo). Nikamuuliza Jaabir, “Je, mlikuwa wangapi?” Akajibu: “Hata kama tungelikuwa laki moja (elfu mia moja – 100,000) ingewatosha, lakini tulikuwa elfu moja na mia tano.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Fadhila Za Nabiy Na Ubora Wa Swahaba]
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
07-Miujiza Yake: Kuzidi Chakula
Alhidaaya.com [4]
Miujiza yake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) ya kuongezeka chakula na vinywaji imetokea mara kadhaa na katika hali na sehemu tofauti. Kati ya miujiza ya kuongezeka chakula ni kama ilivyothibiti katika Hadiyth zifuatazo:
Hadiyth Ya 1:
حَدَّثَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، قَالَ حَدَّثَنَا مُعْتَمِرُ بْنُ سُلَيْمَانَ، قَالَ حَدَّثَنَا أَبِي، حَدَّثَنَا أَبُو عُثْمَانَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي بَكْرٍ، أَنَّ أَصْحَابَ الصُّفَّةِ، كَانُوا أُنَاسًا فُقَرَاءَ، وَأَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " مَنْ كَانَ عِنْدَهُ طَعَامُ اثْنَيْنِ فَلْيَذْهَبْ بِثَالِثٍ، وَإِنْ أَرْبَعٌ فَخَامِسٌ أَوْ سَادِسٌ ". وَأَنَّ أَبَا بَكْرٍ جَاءَ بِثَلاَثَةٍ فَانْطَلَقَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بِعَشَرَةٍ، قَالَ فَهْوَ أَنَا وَأَبِي وَأُمِّي، فَلاَ أَدْرِي قَالَ وَامْرَأَتِي وَخَادِمٌ بَيْنَنَا وَبَيْنَ بَيْتِ أَبِي بَكْرٍ. وَإِنَّ أَبَا بَكْرٍ تَعَشَّى عِنْدَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ لَبِثَ حَيْثُ صُلِّيَتِ الْعِشَاءُ، ثُمَّ رَجَعَ فَلَبِثَ حَتَّى تَعَشَّى النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَجَاءَ بَعْدَ مَا مَضَى مِنَ اللَّيْلِ مَا شَاءَ اللَّهُ، قَالَتْ لَهُ امْرَأَتُهُ وَمَا حَبَسَكَ عَنْ أَضْيَافِكَ ـ أَوْ قَالَتْ ضَيْفِكَ ـ قَالَ أَوَمَا عَشَّيْتِيهِمْ قَالَتْ أَبَوْا حَتَّى تَجِيءَ، قَدْ عُرِضُوا فَأَبَوْا. قَالَ فَذَهَبْتُ أَنَا فَاخْتَبَأْتُ فَقَالَ يَا غُنْثَرُ، فَجَدَّعَ وَسَبَّ، وَقَالَ كُلُوا لاَ هَنِيئًا. فَقَالَ وَاللَّهِ لاَ أَطْعَمُهُ أَبَدًا، وَايْمُ اللَّهِ مَا كُنَّا نَأْخُذُ مِنْ لُقْمَةٍ إِلاَّ رَبَا مِنْ أَسْفَلِهَا أَكْثَرُ مِنْهَا. قَالَ يَعْنِي حَتَّى شَبِعُوا وَصَارَتْ أَكْثَرَ مِمَّا كَانَتْ قَبْلَ ذَلِكَ، فَنَظَرَ إِلَيْهَا أَبُو بَكْرٍ فَإِذَا هِيَ كَمَا هِيَ أَوْ أَكْثَرُ مِنْهَا. فَقَالَ لاِمْرَأَتِهِ يَا أُخْتَ بَنِي فِرَاسٍ مَا هَذَا قَالَتْ لاَ وَقُرَّةِ عَيْنِي لَهِيَ الآنَ أَكْثَرُ مِنْهَا قَبْلَ ذَلِكَ بِثَلاَثِ مَرَّاتٍ. فَأَكَلَ مِنْهَا أَبُو بَكْرٍ وَقَالَ إِنَّمَا كَانَ ذَلِكَ مِنَ الشَّيْطَانِ ـ يَعْنِي يَمِينَهُ ـ ثُمَّ أَكَلَ مِنْهَا لُقْمَةً، ثُمَّ حَمَلَهَا إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَأَصْبَحَتْ عِنْدَهُ، وَكَانَ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمٍ عَقْدٌ، فَمَضَى الأَجَلُ، فَفَرَّقَنَا اثْنَا عَشَرَ رَجُلاً، مَعَ كُلِّ رَجُلٍ مِنْهُمْ أُنَاسٌ، اللَّهُ أَعْلَمُ كَمْ مَعَ كُلِّ رَجُلٍ فَأَكَلُوا مِنْهَا أَجْمَعُونَ، أَوْ كَمَا قَالَ.
Amesimulia ‘Abdur-Rahman bin Abiy Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) : Hakika watu wa Swuffah walikuwa mafakiri. Na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) mara moja alisema: “Mwenye chakula cha watu wawili, amchuke wa tatu (yaani amchukue mtu mmoja miongoni mwao), na yeyote mwenye chakula cha kuwatosha watu wane, achukue wa tano au wa sita (au alisema mfano wake).” Abu Bakr alichukua watu watatu ilhali Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alichukua kumi. Na Abu Bakr pamoja na watu wake watatu wa familia ambao ni mimi, babangu na mamangu. Mpokezi akawa ana shaka kama ‘Abdur-Rahman amesema: “Mke wangu na mtumishi, ambaye alikuwa ni huyo huyo nyumbani kwangu na nyumba ya Abu Bakr.” Abu Bakr alikula chakula cha usiku pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na akabaki huko mpaka akaswali Swalaah ya ‘Ishaa. Alirudi na kubaki na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) mpaka akala chakula chake cha usiku. Baada ya kupita sehemu fulani ya usiku, alirudi nyumbani kwake. Mkewe akamwambia: “Ni kitu kilichokuzuia na wageni wako?” Akasema: “Je, mmewapatia chakula cha usiku?” Akasema: “Wamekataa kula mpaka uje. Wao (yaani baadhi ya watu wa nyumbani) waliwapelekea chakula lakini walikataa (kula)”. Nilikwenda kujificha, akasema: “Ee Ghunthar!” Akamuomba Allaah Ayafanye masikio yangu kukatwa, naye akanikaripia. Akasema: “Kuleni!” Na akaongeza: “Mimi sitokula chakula”. Akasema: “Naapa kwa Allaah! Kila tulipokuwa tunachukua tonge ya chakula, chakula kilikuwa kikijaa kutoka chini zaidi kuliko tonge hilo mpaka kila mmoja akala na kushiba. Hata ivyo, chakula kilichobakia kilikuwa kingi kuliko kile cha awali. Abu Bakr akakiona chakula kilikuwa zaidi kuliko kile cha mwanzo”. Alimuita mkewe, “Ee dada wa Bani Firaas!” Akajibu, “Ee pozo la macho yangu. Chakula hiki kimeongezeka mara tatu zaidi.” Abu Bakr, alianza kula chakula hicho, na huku anasema: “Hakika hicho (yaani kiapo cha kutokula) ni kwa sababu ya shaytwaan.” Kisha akala tonge kwayo, na kumpelekea chengine Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم). Chakula hicho kikawa kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم). Kulikuwa na sulhu baina yetu na watu fulani, na muda wa sulhu ulipomalizika, alitugawa makundi kumi na mbili, kila kimoja kikiongozwa na mtu. Allaah Ndiye Ajuaye watu wangapi walikuwa chini ya amiri wa kila kikundi. Hata hivyo, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alituma amiri kwa kila kikundi. Kisha wote wakala chakula hicho. [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Manaaqib]
Hadiyth Ya 2:
حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ النَّضْرِ بْنِ أَبِي النَّضْرِ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبُو النَّضْرِ، هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ الأَشْجَعِيُّ، عَنْ مَالِكِ بْنِ مِغْوَلٍ، عَنْ طَلْحَةَ بْنِ مُصَرِّفٍ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي مَسِيرٍ - قَالَ - فَنَفِدَتْ أَزْوَادُ الْقَوْمِ قَالَ حَتَّى هَمَّ بِنَحْرِ بَعْضِ حَمَائِلِهِمْ - قَالَ - فَقَالَ عُمَرُ يَا رَسُولَ اللَّهِ لَوْ جَمَعْتَ مَا بَقِيَ مِنْ أَزْوَادِ الْقَوْمِ فَدَعَوْتَ اللَّهَ عَلَيْهَا . قَالَ فَفَعَلَ - قَالَ - فَجَاءَ ذُو الْبُرِّ بِبُرِّهِ وَذُو التَّمْرِ بِتَمْرِهِ - قَالَ وَقَالَ مُجَاهِدٌ وَذُو النَّوَاةِ بِنَوَاهُ - قُلْتُ وَمَا كَانُوا يَصْنَعُونَ بِالنَّوَى قَالَ كَانُوا يَمُصُّونَهُ وَيَشْرَبُونَ عَلَيْهِ الْمَاءَ . قَالَ فَدَعَا عَلَيْهَا - قَالَ - حَتَّى مَلأَ الْقَوْمُ أَزْوِدَتَهُمْ - قَالَ - فَقَالَ عِنْدَ ذَلِكَ " أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنِّي رَسُولُ اللَّهِ لاَ يَلْقَى اللَّهَ بِهِمَا عَبْدٌ غَيْرَ شَاكٍّ فِيهِمَا إِلاَّ دَخَلَ الْجَنَّةَ " .
Amesimulia Abu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ):
Tulikuwa tukiongozana na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) katika safari ya (kuelekea Tabuwk). Yeye (msimulizi) alisema: “Vitu na watu vilikuwa karibu vimepungua. Yeye (msimulizi) alisema: (Na hali ikawa mbaya sana) hadi kwamba (wanajeshi) waliamua kuchinja ngamia zao.” Yeye (msimulizi) akasema: Juu ya jambo hili ‘Umar alisema: “Ee Rasuli wa Allaah, laiti kama ungejumuisha pamoja yale yaliyoachwa kwenye vifungu na watu na kisha muombe Allaah (Alete Barakah Zake) juu yake.” Yeye (msimulizi) alisema: “Yeye (Nabiy صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alifanya hivyo.: Yeye (msimulizi) akasema: “Yule aliyekuwa na ngano katika mali yake alikuja pale na ngano. Aliyekuwa na tende naye alikuja pale na tende. Na Mujahid akasema: “Aliyekuwa na kokwa za tende alikuja pale na kokwa.” Mimi (msimulizi) nikasema: “Walifanya nini na kokwa za tende?” Wakasema: “Wao (watu) walikuwa wakizifonza kuzikamua (mdomoni) na kisha wakanywa maji yake.” Yeye (msimulizi alisema): “Yeye (Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) Akaziombea (Baraka za Allaah) juu yake (hizo rizki).” Yeye (msimulizi) alisema: “Na kulikuwa na ongezeko la muujiza katika rizki) hadi kwamba watu walijaza chakula chao kikamilifu.” Yeye (msimulizi) akasema: Wakati huo yeye (Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alisema:
أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنِّي رَسُولُ اللَّهِ لاَ يَلْقَى اللَّهَ بِهِمَا عَبْدٌ غَيْرَ شَاكٍّ فِيهِمَا إِلاَّ دَخَلَ الْجَنَّةَ "
Ash-hadu an laa ilaaha illa Allaah wa anniy Rasuwlu-Allaah.
Nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah na kwamba mimi ni Rasuli wa Allaah.
Hakuna mja atakayekutana na Allaah kwazo Shahada mbili hizi, bila ya kutilia shaka ndani yake, isipokuwa ataingia Jannah.” [Muslim Kitaab Al-Iymaan]
Hadiyth Ya 3:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنْ إِسْحَاقَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي طَلْحَةَ، أَنَّهُ سَمِعَ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ، يَقُولُ قَالَ أَبُو طَلْحَةَ لأُمِّ سُلَيْمٍ لَقَدْ سَمِعْتُ صَوْتَ، رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ضَعِيفًا، أَعْرِفُ فِيهِ الْجُوعَ فَهَلْ عِنْدَكِ مِنْ شَىْءٍ قَالَتْ نَعَمْ. فَأَخْرَجَتْ أَقْرَاصًا مِنْ شَعِيرٍ، ثُمَّ أَخْرَجَتْ خِمَارًا لَهَا فَلَفَّتِ الْخُبْزَ بِبَعْضِهِ، ثُمَّ دَسَّتْهُ تَحْتَ يَدِي وَلاَثَتْنِي بِبَعْضِهِ، ثُمَّ أَرْسَلَتْنِي إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ فَذَهَبْتُ بِهِ، فَوَجَدْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي الْمَسْجِدِ وَمَعَهُ النَّاسُ، فَقُمْتُ عَلَيْهِمْ فَقَالَ لِي رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " آرْسَلَكَ أَبُو طَلْحَةَ ". فَقُلْتُ نَعَمْ. قَالَ بِطَعَامٍ. فَقُلْتُ نَعَمْ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لِمَنْ مَعَهُ " قُومُوا ". فَانْطَلَقَ وَانْطَلَقْتُ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ حَتَّى جِئْتُ أَبَا طَلْحَةَ فَأَخْبَرْتُهُ. فَقَالَ أَبُو طَلْحَةَ يَا أُمَّ سُلَيْمٍ، قَدْ جَاءَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِالنَّاسِ، وَلَيْسَ عِنْدَنَا مَا نُطْعِمُهُمْ. فَقَالَتِ اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ. فَانْطَلَقَ أَبُو طَلْحَةَ حَتَّى لَقِيَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم، فَأَقْبَلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَأَبُو طَلْحَةَ مَعَهُ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " هَلُمِّي يَا أُمَّ سُلَيْمٍ مَا عِنْدَكِ ". فَأَتَتْ بِذَلِكَ الْخُبْزِ، فَأَمَرَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَفُتَّ، وَعَصَرَتْ أُمُّ سُلَيْمٍ عُكَّةً فَأَدَمَتْهُ، ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِيهِ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَقُولَ، ثُمَّ قَالَ " ائْذَنْ لِعَشَرَةٍ ". فَأَذِنَ لَهُمْ، فَأَكَلُوا حَتَّى شَبِعُوا ثُمَّ خَرَجُوا، ثُمَّ قَالَ " ائْذَنْ لِعَشَرَةٍ ". فَأَذِنَ لَهُمْ، فَأَكَلُوا حَتَّى شَبِعُوا ثُمَّ خَرَجُوا، ثُمَّ قَالَ " ائْذَنْ لِعَشَرَةٍ ". فَأَذِنَ لَهُمْ، فَأَكَلُوا حَتَّى شَبِعُوا ثُمَّ خَرَجُوا ثُمَّ قَالَ " ائْذَنْ لِعَشَرَةٍ ". فَأَكَلَ الْقَوْمُ كُلُّهُمْ وَشَبِعُوا، وَالْقَوْمُ سَبْعُونَ ـ أَوْ ثَمَانُونَ ـ رَجُلاً.
Amesimulia Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuwa Abu Twalhah alimwambia Umm Sulaym (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) “Nimesikia sauti ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) ikiwa dhaifu, nikagundua kuwa ana njaa. Je, unacho chakula?” Umm Sulaym akajibu: “Ndiyo.” Akatoa mikate ya shayiri, kisha akatoa ushungi wake na kuifunga mikate, kisha akauingiza mkononi mwangu na kuizungusha sehemu ya ushingi kwangu. Kisha akanituma niende kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم). Nikaenda na mikate niliyoibeba na nikamkuta Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akiwa Msikitini pamoja na watu. Niliposimama mbele yake Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akaniuliza: “Je, amekutuma Abu Twalhah?” Nikasema: “Ndiyo.” Akaniuliza: “Na chakula?” Nikasema: “Ndiyo.” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akawaambia waliokuwa pamoja naye, “Amkeni, njooni!” Akaondoka (akifuatana na wale watu) nami nikaondoka upesi nikiwa mbele yao hata nikafika kwa Abu Twalhah nikamueleza kilicho tokea. Abu Twalhah akasema kumwambia Umm Sulaym: “Ee Umm Sulaym! Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) anakuja pamoja na watu nasi hatuna cha kuwalisha.” Umm Sulaym akajibu kwa kusema: “Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi.” Abu Twalhah akaondoka kwenda kumpokea Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم), akaja Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akifuatana na Abu Twalhah. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akasema: “Umm Sulaym lete ulicho nacho”. Akauleta ule mkate, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akaamuru ukakatwa katwa, na Umm Sulaym akawaletea samli ikawa ndiyo siagi yao. Kisha Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akasoma alichoweza kukisoma humo, kisha akasema: “Waruhusu watu kumi.” Akawaruhusu wakala mpaka wakashiba na wakatoka. Kisha akasema tena: “Waruhusuni kumi wengine.” Akawaruhusu watu wote wakala na wakashiba na akawa anasema hivyo na wakala wote hadi wakaisha waliokuwepo. Jumla ya watu walikuwa kati ya sabiini na themanini. [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Manaaqib]
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
08-Miujiza Yake: Shina Ya Miti Kulia Kwa Kumkosa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم)
Alhidaaya.com [4]
Miongoni mwa miujiza ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) ni shina la mtende kulia kwa kumkosa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) au kukosa kuwa karibu naye pindi alipokuwa akikhutubia katika minbari na kukosa kusikia kwa ukaribu kabisa Dhikru-Allaah. Miujiza kama hii na mengineyo ni katika alama zake Muhammad (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) za Unabii. Hadiyth zifuatazo zimethibiti:
حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيلُ، قَالَ حَدَّثَنِي أَخِي، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ بِلاَلٍ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي حَفْصُ بْنُ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّهُ سَمِعَ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ ـ رضى الله عنهما ـ يَقُولُ كَانَ الْمَسْجِدُ مَسْقُوفًا عَلَى جُذُوعٍ مِنْ نَخْلٍ فَكَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم إِذَا خَطَبَ يَقُومُ إِلَى جِذْعٍ مِنْهَا، فَلَمَّا صُنِعَ لَهُ الْمِنْبَرُ، وَكَانَ عَلَيْهِ فَسَمِعْنَا لِذَلِكَ الْجِذْعِ صَوْتًا كَصَوْتِ الْعِشَارِ، حَتَّى جَاءَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَوَضَعَ يَدَهُ عَلَيْهَا فَسَكَنَتْ.
Amesimulia Hafsw bin ‘Ubaydillaah bin Anas bin Maalik kuwa alimsikia Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) akisema: “Sakafu ya Msikiti ulijengwa juu ya mashina ya mitende yakiwa ndio nguzo. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alipokuwa akikhutubu alikuwa akisimama karibu na shina moja miongoni mwayo mpaka mimbar ilipotengenezwa kwa ajili yake, na akawa anaitumia badala yake. Tukasikia sauti kutoka kwa shina hilo kama sauti ya ngamia jike aliye na mimba mpaka Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akaujia, akaweka mkono wake juu yake, ukatulia.” [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Manaaqib]
Pia:
حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَاحِدِ بْنُ أَيْمَنَ، قَالَ سَمِعْتُ أَبِي، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ ـ رضى الله عنهما ـ أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَقُومُ يَوْمَ الْجُمُعَةِ إِلَى شَجَرَةٍ أَوْ نَخْلَةٍ، فَقَالَتِ امْرَأَةٌ مِنَ الأَنْصَارِ ـ أَوْ رَجُلٌ ـ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَلاَ نَجْعَلُ لَكَ مِنْبَرًا قَالَ " إِنْ شِئْتُمْ ". فَجَعَلُوا لَهُ مِنْبَرًا، فَلَمَّا كَانَ يَوْمُ الْجُمُعَةِ دُفِعَ إِلَى الْمِنْبَرِ، فَصَاحَتِ النَّخْلَةُ صِيَاحَ الصَّبِيِّ، ثُمَّ نَزَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَضَمَّهُ إِلَيْهِ تَئِنُّ أَنِينَ الصَّبِيِّ، الَّذِي يُسَكَّنُ، قَالَ " كَانَتْ تَبْكِي عَلَى مَا كَانَتْ تَسْمَعُ مِنَ الذِّكْرِ عِنْدَهَا "
Amesimulia Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alikuwa akisimama karibu na mti au mtende wakati anatoa khutbah ya Ijumaa. Kisha mwanamke wa ki-Answaar au mwanamme akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Je, hatukutengenezei mimbar?” Akajibu: “Mkipenda.” Wakamfanyia mimbar na ilipofika Ijumaa, aliiendelea mimbar (kwa ajili ya kutoa khutbah). Mtende ukalia kama mtoto! Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alishuka (kwenye mimbar) na kuukumbatia ilhali unapiga kite (unaugua) kama mtoto anayetulizwa. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akasema: “Kilikuwa kinalia kwa kukosa kilichokuwa kikisikia katika Dhikr (ukumbusho) karibu yake.” [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Manaaqib]
Pia
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُثَنَّى، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ كَثِيرٍ أَبُو غَسَّانَ، حَدَّثَنَا أَبُو حَفْصٍ ـ وَاسْمُهُ عُمَرُ بْنُ الْعَلاَءِ أَخُو أَبِي عَمْرِو بْنِ الْعَلاَءِ ـ قَالَ سَمِعْتُ نَافِعًا، عَنِ ابْنِ عُمَرَ ـ رضى الله عنهما ـ كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَخْطُبُ إِلَى جِذْعٍ فَلَمَّا اتَّخَذَ الْمِنْبَرَ تَحَوَّلَ إِلَيْهِ، فَحَنَّ الْجِذْعُ فَأَتَاهُ فَمَسَحَ يَدَهُ عَلَيْهِ. وَقَالَ عَبْدُ الْحَمِيدِ أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، أَخْبَرَنَا مُعَاذُ بْنُ الْعَلاَءِ، عَنْ نَافِعٍ، بِهَذَا. وَرَوَاهُ أَبُو عَاصِمٍ عَنِ ابْنِ أَبِي رَوَّادٍ، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم.
Amesimulia Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alikuwa akikhutubu akiwa amesimama karibu na pingiti la mtende. Alipoichukua mimbar, akaitumia badala yake. Pingiti hilo lilianza kulia na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) aliliendea, akilipapasa kwa mkono wake (ili liache kulia). [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Manaaqib]
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
09-Miujiza Yake: Nuru Yake Kuwaongoza Swahaba Njia Katika Kiza
Alhidaaya.com [4]
Swahaba wawili walikwenda nyumbani kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) usiku mmoja wa kiza, pindi walipoondoka, Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) Alijaaliwa Nuru ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) iwaandame kama taa mbili zikiwaangazia njia. Basi kila mmoja wao alikwenda nyumbani kwake kwa nuru ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) iliyomwongoza njia kizani.
حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ الْمُثَنَّى، حَدَّثَنَا مُعَاذٌ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبِي، عَنْ قَتَادَةَ، حَدَّثَنَا أَنَسٌ ـ رضى الله عنه ـ أَنَّ رَجُلَيْنِ، مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم خَرَجَا مِنْ عِنْدِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي لَيْلَةٍ مُظْلِمَةٍ وَمَعَهُمَا مِثْلُ الْمِصْبَاحَيْنِ، يُضِيآنِ بَيْنَ أَيْدِيهِمَا، فَلَمَّا افْتَرَقَا صَارَ مَعَ كُلِّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا وَاحِدٌ حَتَّى أَتَى أَهْلَهُ.
Amesimulia Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Mara moja watu wawili miongoni mwa Swahaba wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) walitoka katika nyumba ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) usiku wa kiza totoro. Walifuatwa na vitu viwili vinavyofanana na kandili mbili kuwaonyesha njia kwa mwangaza wake, na walipoachana, kila mmoja wao aliandamwa na moja kati ya hivyo vitu viwili mpaka wakafika nyumbani kwao. [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Manaaqib]
Na katika Riwaayah nyengine:
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُثَنَّى، قَالَ حَدَّثَنَا مُعَاذُ بْنُ هِشَامٍ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبِي، عَنْ قَتَادَةَ، قَالَ حَدَّثَنَا أَنَسٌ، أَنَّ رَجُلَيْنِ، مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم خَرَجَا مِنْ عِنْدِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي لَيْلَةٍ مُظْلِمَةٍ، وَمَعَهُمَا مِثْلُ الْمِصْبَاحَيْنِ يُضِيآنِ بَيْنَ أَيْدِيهِمَا، فَلَمَّا افْتَرَقَا صَارَ مَعَ كُلِّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا وَاحِدٌ حَتَّى أَتَى أَهْلَهُ.
Amesimulia Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ):
Swahaba wawili wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) waliondoka na kiza kilikuwa kimeingia, waliongozwa na mianga miwili mithili ya taa (kukiwatangulia kutokana na miujiza ya Allaah) ukiwamulikia njia mbele yao, na walipoachana, kila mmoja alimulikiwa na moja ya mianga hiyo mpaka walipofika majumbani mwao. [Al-Bukhaariy Kitaab Asw-Swalaah]
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
10-Miujiza Yake: Jiwe Kumsalimia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم)
Alhidaaya.com [4]
حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ أَبِي بُكَيْرٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ طَهْمَانَ، حَدَّثَنِي سِمَاكُ بْنُ حَرْبٍ، عَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " إِنِّي لأَعْرِفُ حَجَرًا بِمَكَّةَ كَانَ يُسَلِّمُ عَلَىَّ قَبْلَ أَنْ أُبْعَثَ إِنِّي لأَعْرِفُهُ الآنَ " .
Amesimulia Jaabir bin Samurah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) amesema: “Hakika mimi nalijua jiwe lilioko Makkah likuwa likinisalimia kabla sijapewa Unabiy na nalitambua hadi sasa.“ [Muslim]
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
11-Miujiza Yake:
Mlima Wa Uhud Kuwa Na Hisia Na Kumpenda Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) Na Kuwapenda Swahaba
Alhidaaya.com [4]
Kuhusu Mlima wa Uhud kuwa na hisia:
حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا يَحْيَى، عَنْ سَعِيدٍ، عَنْ قَتَادَةَ، أَنَّ أَنَسًا رضى الله عنه حَدَّثَهُمْ قَالَ صَعِدَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم أُحُدًا، وَمَعَهُ أَبُو بَكْرٍ وَعُمَرُ وَعُثْمَانُ، فَرَجَفَ وَقَالَ " اسْكُنْ أُحُدُ ـ أَظُنُّهُ ضَرَبَهُ بِرِجْلِهِ ـ فَلَيْسَ عَلَيْكَ إِلاَّ نَبِيٌّ وَصِدِّيقٌ وَشَهِيدَانِ ".
Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alipanda juu ya (Mlima wa) Uhud pamoja na Abu Bakr, ‘Umar na ‘Uthmaan na ukatikisika. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akasema: "Tulia ee Uhud!" Ninadhani aliupiga kwa mguu wake na kuongeza kusema: "Aliye juu yako si mwingine isipokuwa Nabiy, Asw-Swiddiyq (Abu Bakr) na Mashuhadaa wawili (‘Umar na ‘Uthmaan bin ‘Affaan)." [Al-Bukhaariy]
Na kuhusu Mlima wa Uhud kumpenda Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na kuwapenda Swahaba (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ):
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنْ عَمْرٍو، مَوْلَى الْمُطَّلِبِ عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ ـ رضى الله عنه ـ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم طَلَعَ لَهُ أُحُدٌ فَقَالَ " هَذَا جَبَلٌ يُحِبُّنَا وَنُحِبُّهُ، اللَّهُمَّ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ حَرَّمَ مَكَّةَ، وَإِنِّي حَرَّمْتُ مَا بَيْنَ لاَبَتَيْهَا ".
Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia: Mlima wa Uhud ulijitokeza mbele ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akasema: “Mlima huu unatupenda na sisi tunaupenda. Ee Allaah! Ibraahiym Alifanya Makkah kuwa tukufu na mimi nimeifanya Al-Madiynah kuwa tukufu (yaani, eneo la baina ya milima) milima yake miwili. [Al-Bukhaariy]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/278
[2] http://alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10928&title=Fadhila%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Miujiza%20Yake
[4] http://www.alhidaaya.com/sw/
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10929&title=01-Fadhila%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Miujiza%20Yake%3A%20Ni%20Mingi%20Muujiza%20Mkubwa%20Kabisa%20Ni%20Qur-aan
[6] http://www.alhidaaya.com/sw/node/3397
[7] http://www.alhidaaya.com/sw/node/180
[8] http://www.alhidaaya.com/sw/node/6175
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10935&title=02-Fadhila%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Miujiza%20Yake%3A%20Muujiza%20Wa%20Al-Israa%20Wal-Mi%E2%80%99raaj%20
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10947&title=03-Fadhila%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Miujiza%20Yake%3A%20Kupasuka%20Mwezi%20
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10953&title=04-Fadhila%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Miujiza%20Yake%3A%20Wanyama%20Kuzungumza%20Na%20Swahaba
[12] http://www.alhidaaya.com/sw/node/9795
[13] http://www.alhidaaya.com/sw/node/9796
[14] http://www.alhidaaya.com/sw/node/9798
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10977&title=05-Fadhila%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Miujiza%20Yake%3A%20Kuteremshwa%20%20Mvua%20Tele%20Kwa%20Du%E2%80%99aa%20Yake
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10993&title=06-Fadhila%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Miujiza%20Yake%3A%20Vidole%20Vyake%20Kutoa%20Maji%20Tele
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11000&title=07-Fadhila%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Miujiza%20Yake%3A%20Kuzidi%20Chakula%20
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11001&title=08-Fadhila%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Miujiza%20Yake%3A%20Shina%20Ya%20Miti%20Kulia%20Kwa%20Kumkosa%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%8E%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%D9%8F%20%D8%B9%D9%8E%D9%84%D9%8E%D9%8A%D9%92%D9%87%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%A2%D9%84%D9%90%D9%87%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%B3%D9%8E%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%85%29
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11003&title=09-Fadhila%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Miujiza%20Yake%3A%20Nuru%20Yake%20Kuwaongoza%20Swahaba%20Njia%20Katika%20Kiza
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11035&title=10-Fadhila%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Miujiza%20Yake%3A%20Jiwe%20Kumsalimia
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11037&title=11-Fadhila%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Miujiza%20Yake%3A%20Mlima%20Wa%20Uhud%20Kuwa%20Na%20Hisia%20Na%20Kumpenda%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%8E%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%D9%8F%20%D8%B9%D9%8E%D9%84%D9%8E%D9%8A%D9%92%D9%87%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%A2%D9%84%D9%90%D9%87%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%B3%D9%8E%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%85%29%20%20Na%20Kuwapenda%20Swahaba