Siku ya pili yake Abu Bakr (Radhiya Allaahu 'anhu) aliwasilimisha watano katika mabwana wa kabila la Kikureshi, nao ni 'Uthmaan bin Affan, Az-Zubayr bin 'Awwaam, 'Abdur-Rahmaan bin 'Awf, Sa'ad bin Abi Waqqaasw na Twalhah bin 'UbayduLLaah; akaja nao mpaka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), na wote hawa ni katika wale kumi waliokwisha bashiriwa Pepo .
Siku iliyofuata aliwasilimisha vigogo wengine wanne na kuja nao mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), nao ni 'Uthmaan bin Madh'uwn, Abu 'Ubaydah 'Aamir bin Al-Jarraah, Abu Salamah na Al-Arqam bin Abi Al-Arqam.
Nguvu ya Uislamu ikaongezeka, na Abu Bakr aliitumia mali yake yote katika kuunusuru Uislam na pia nguvu zake na daraja lake mbele ya ma-Quraysh, na vyote hivi vilisaidia sana katika kuujenga na kuuendeleza Uislamu, hata watu wakawa wanasema;
"Wasingeshikamana wawili hawa kama hivi, kwa jambo la upotovu."
Links
[1] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1456&title=06-Abu%20Bakr%20Asw-Swiddiyq%20%28Radhwiya%20Allaahu%20%27anhu%29%3A%20Abu%20Bakr%20%28%20%D8%B1%D8%B6%D9%8A%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%86%D9%87%20%29%20Anaanza%20Kazi%20Ya%20Kuwasilimisha%20Watu