Mume anaruhusiwa kustarehe na mkewe kwa njia yoyote isipokuwa sehemu zake za siri anapokuwa katika Hedhi. Kuna Hadiyth mbali mbali kuhusu jambo hili:
Kwanza:
((...اصْنَعُوا كُلَّ شَيْءٍ إِلاَّ النِّكَاحَ))
"…fanyeni kila kitu isipokuwa jimai pekee"[1]
Pili:
عن عَائِشَةَ رضي الله عنها ، قَالَتْ: كانَ رَسُولُ اللَّهِ، يَأْمُرُ إِحْدَانَا إِذا كَانَتْ حَائِضاً أَنْ تَتَّزِرََ ثُمَّ يُضَاجِعُهَا زَوْجُهَا وَقالَتْ مَرَّةً: يُبَاشِرُهَا.
Kutoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah رضي الله عنها ambaye amesema: "Tulipokuwa katika siku zetu (hedhi) Mtume alikuwa akituamrisha tuvae nguo kiunoni ili mume aweze kulala naye". Na akasema (mama wa waumini ‘Aaishah) pia …"Mumewe aweze kumkumbatia na kumpapasa".[2]
Tatu:
عن بَعْضِ أزْوَاجِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قالَتْ: إنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إذَا أرَادَ مِنَ الْحَائِضِ شَيْئاً ألْقَى عَلَى فَرْجِهَا ثَوْباً [ ثم صنع ما أراد]
Kutoka kwa mmoja wa wake zake Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ambaye amesema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alipokuwa anataka kitu (kufurahi naye) kutoka kwa wake zake siku za hedhi, alikuwa anaweka nguo katika sehemu zake za siri kisha hufanya anavyotaka".[3]
Links
[1] http://www.alhidaaya.com/sw/modules/fckeditor/fckeditor/editor/fckeditor.html?InstanceName=edit-body&Toolbar=Default#_ftnref1
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/modules/fckeditor/fckeditor/editor/fckeditor.html?InstanceName=edit-body&Toolbar=Default#_ftnref2
[3] http://www.alhidaaya.com/sw/modules/fckeditor/fckeditor/editor/fckeditor.html?InstanceName=edit-body&Toolbar=Default#_ftnref3
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1591&title=18-Adabu%20Za%20Ndoa%20Katika%20Sunnah%20Iliyotakasika%3A%20Yanayoruhusiwa%20Anapokuwa%20Katika%20Hedhi%20