TARATIBU ZA IMAAM ASH-SHAAFI'IY KWENYE KITABU CHAKE: AR-RISAALAH
Al-Imaam ash-Shaafi’iy alianza kitabu chake kwa kutanabahisha hali ya binaadamu kabla tu ya ujumbe wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa kufanya hivyo, aliwagawa kwenye makundi mawili:-
Baadaye al-Imaam ash-Shaafi’iy alisema kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Amewaokoa wanaadamu wote kwa kumleta wa Mwisho katika Mitume, na kumshushia Kitabu Chake, ili kwamba huenda wakapokea kupitia kwake, njia ya kuondokana na upofu wa ukafiri kwenda nuru ya uongofu:
{{Kwa hakika wale wanaoyakanusha mawaidha yanapowajia (Tutawaadhibu). Bila shaka hicho ni Kitabu kihishimiwacho.
Haitofikia batili (Kitabu hichi) toka mbele yake wala nyuma yake, kimeteremshwa na Mwenye hikima, Ahimidiwaye}} [41:41-42]
Baadaye al-Imaam ash-Shaafi’iy aliendelea kujadili kwa undani hadhi ya
Qur-aan ndani ya Uislamu na matamko yake mengi kuhusu nini Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Ameruhusu na kuzuia, vipi mwanaadamu amuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), malipo ya wale wenye kumtii Yeye; adhabu kwa wale Wanaomtii Yeye na namna Alivyowaangamiza kwa kuwapa habari za waliotangulia.
Baadaye, al-Imaam ash-Shaafi’iy alieleza kwamba wanafunzi wanaotafuta elimu ya Kiislamu wajifunze mengi ndani ya Qur-aan na sayansi zake, kadri watakavyoweza; na kwamba pale nia zao zitakapokuwa
Mwisho wa utangulizi wake wa ar-Risaalah, al-Imaam ash-Shaafi’iy alisema: “Hakuna tatizo litakalomshambulia miongoni mwa wafuasi wa Dini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) isipokuwa kwamba kutakuwa na muongozo ndani ya Kitabu cha Allaah kuonesha njia sahihi. Kwani, Allaah, Mtukufu Aliye Bora, Amesema:
{{Kitabu Tulichokiteremsha kwako ili uwatoe watu katika giza uwapeleke katika nuru, kwa idhini ya Mola wao, uwafikirishe katika njia ya yule Mwenye kushinda (na) Mwenye kusifika (Naye ni Mwenyezi Mungu)}} [14:1]
Na pia Amesema:
{{(Tuliwaleta) Kwa Ishara zilizo wazi na kwa Vitabu. Na Tumekuteremshia mauidha ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao, na ili wapate kufikiri}} [16:44]
Na pia Amesema:
{{Kwa hakika Mwenyezi Mungu Anaamrisha uadilifu, na kufanya ihsani, na kuwapa jamaa (na wengineo); na Anakataza uchafu na uovu, na dhulma. Anakunasihini ili mupate kufahamu (mfuate).}} [16:90]
Na:
{{Na namna hivi Tumekufunulia Wahyi kwa amri Yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini wala imani; lakini Tumefanya Kitabu hiki (Qur-aan) ni nuru, ambayo kwa (nuru) hiyo Tunamwongoza Tumtakaye katika waja Wetu. Na kwa yakini wewe unaongoza katika njia iliyonyooka.}} [42:52]
Baadaye inafuatia Sura kuhusu al-Bayaan[53] ambapo neno hili linatafsiriwa
1) Yale ambayo Allaah Ametolea maamuzi
2) Yale ambayo inayataja Qur-aan ambayo yanaweza kutolewa maana katika njia tofauti, na yale ambayo Sunnah imetoa maelezo ya kuweka wazi, ipi iliyokusudiwa.
3) Yale ambayo yameelezwa bayana kuwa yana ulazima, na yale Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ameeleza kwa matamshi ya vipi, kwanini, ni juu ya nani, na wapi kutumika na wapi kutotumika.
4) Yale ambayo yameelezwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), lakini hayakutajwa ndani ya Qur-aan. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Ameamrisha ndani ya Qur-aan kwamba atiiwe Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na amri zake zikubaliwe. Hivyo yanayotamkwa kutoka mamlaka ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), yanatambulika kuwa ni mamlaka ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).
5) Yale ambayo yanahitaji viumbe Wake kutafuta kupitia Ijtihaad. Hii ni Qiyaas. Kwa mujibu wa al-Imaam ash-Shaafi’iy, Qiyaas ni utaratibu wa kufikia ufumbuzi wa kisheria kwa msingi wa ushahidi (hukumu zilizowahi kutolewa kabla na kukubaliwa) ambapo hutumika hoja maarufu au sababu inayofaa.
Al-Imaam ash-Shaafi’iy kisha aliendelea kuelezea mafungu haya matano kwenye sura tano tofauti, akitoa mifano na ushahidi wa kila moja. Hivyo, ar-Risaalah hiyo ilikuwa na sura zifuatazo:-
Katika Sura iliyotajwa hapo juu, al-Imaam ash-Shaafi’iy alieleza uhalali wa Sunnah
Ndani ya Sura hii, al-Imaam ash-Shaafi’iy amethibitisha kwamba sehemu ya Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zimejadiliwa na kuhusishwa na Qur-aan, wakati sehemu nyengine zimeeleza masuala yaliyohusika, ambayo hakuna maandiko yanayonasibiana nayo ndani ya Kitabu. Al-Imaam ash-Shaafi’iy pia ameonesha kwamba Sunnah ipo huru na Qur-aan, na kunukuu ushahidi ili kuwakosoa wale ambao hawakubaliani naye kwenye suala
Baadaye inafuata sura iliyoitwa, “Asili ya Kutengua na Kutenguliwa”; ambayo inaeleza kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Ametumia utenguzi kuifanya (Shariah) nyepesi na yenye kubadilika zaidi. Sura hii pia inabainisha kwamba aya ya Qur-aan inaweza tu kutenguliwa kwa aya nyengine ya Qur-aan; na kwamba Sunnah inaweza tu kutenguliwa kwa Sunnah nyengine.
Kisha akajadili kwa pamoja; kutengua na kutenguliwa. Ambazo zinabainishwa ndani ya sehemu ya Qur-aan, na ndani ya sehemu ya Sunnah.
Baada ya hapo inabainishwa kuhusu Fardh-wajibu wa Swalaah na maelezo ndani ya Qur-aan na Sunnah kuhusiana na wale ambao wanaweza kuwa na udhuru wa kutoiswali, na wale ambao Swalaah haikubaliki kwa sababu ya kitendo kiovu ambacho huenda wamekitenda.
Kisha, al-Imaam ash-Shaafi’iy ameandika Kutengua na Kutenguliwa ambazo zinatajwa ndani ya Sunnah na al-Ijmaa’,
Kwenye sura inayofuata, amejadili kuhusu dosari ndani ya Hadiyth, na kueleza kwamba mgongano baina ya Hadiyth unaweza kutokea kwa sababu zilizo nyingi. Ameendelea kueleza baadhi ya sababu hizi. Kwa mfano, mgongano unaweza kutokea kwa sababu Hadiyth moja imetenguliwa na nyengine, au kwa sababu ya makosa yaliyotokea ndani ya upokezi wa Hadiyth hiyo. Ameelezea makosa ambayo huenda yamesababisha migongano ndani ya Hadiyth, na sababu nyenginezo nyingi zilizopelekea migongano
Al-Imaam ash-Shaafi’iy pia ameweka sura kuhusu elimu, na kueleza kwamba kuna aina mbili za elimu. Ya kwanza; ni aina ya elimu maarufu ambayo hakuna uwezekano wa kutoifahamu kwa mtu mzima na mwenye akili timamu. Elimu yote ya aina hii inawezekana kupatikana na kutajwa ndani ya maandiko ya Qur-aan, na kila Muislamu anaelewa yote hayo kwa sababu imeteremshwa kwake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kila kizazi kilchotangulia. Hakuna (mjadala) kuhusiana na usahihi wa elimu hii, na wote wanakubali kwamba ni lazima. Hakika, asili ya elimu hii ni kwamba, hakuna uwezekanao wa kuwepo makosa katika kufika kwake au kutafsiri.
Aina ya pili ya elimu ni ya maelezo yanayotokana na mzizi wa ulazima, na sheria mahsusi zinazotokana nazo. Hizi hazijatajwa ndani ya maandiko ya Qur-aan, na nyingi katika hizo hazitajwi ndani ya maandiko ya Sunnah achilia mbali kutokana na mapokezi ya mmoja-pekee, Ahad.
Hivyo, al-Imaam ash-Shaafi’iy ametoa utangulizi wa somo jipya, upokezi wa mmoja-pekee, Khabar al-Waahid. Al-Imaam ash-Shaafi’iy baadaye akaeleza nini kinachokusudiwa kwa neno hili, na masharti ambayo yataitambua
Baadaye, al-Imaam ash-Shaafi’iy amejadili hadhi ya Khabar al-Waahid, na kama habari hizo zinaweza kutumika kama ni ushahidi. Hitimisho lake, linakubalika kwa hoja zilizo nzuri na makini, ni kwamba; hakika zinaweza kutumika. Hivyo, al-Imaam ash-Shaafi’iy ametangulia katika kufuta mashaka yote yaliyokuzwa na wanaompinga kwenye suala hili.
Sura zifuatazo zinafuatia:-
Aina ya kutokubaliana ambazo haziruhusiwi na zile kuhusiana na masuala ambayo Allaah Ametoa ushahidi ulio wazi ndani ya maandiko ya Qur-aan au Sunnah. Kutokubalina kwa aina ambazo zinaruhusiwa, inahusiana na masuala ambayo yanaweza kutafsiriwa kwa kutumia njia tofauti na zile ambazo kila mwanazuoni anatumia aina yake ya kutoa hoja. Al-Imaam ash-Shaafi’iy kisha akatoa mfano wa aina zote, ametoa mifano ya masuala ambayo Maswahaba hawakukubaliana, kama vile ‘Iddah, viapo na mirathi. Ndani ya sura hii, al-Imaam ash-Shaafi’iy ametaja kitu kuhusiana na utaratibu wa kutumika hiari kwa maoni ya Maswahaba pale wanapohitalifiana.
Ar-Risaalah inahitimishwa kwa ufafanuzi wa mawazo ya ash-Shaafi’iy kwenye “mafungu ya ushahidi” yaliyoelezwa hapo juu.
“Tunaegemeza hukumu zetu kimsingi kwenye Qur-aan na Sunnah iliyokubaliwa kuhusiana na yale ambayo hayana mgogoro, nasema: “Hii ndio hukumu yetu baada ya kusoma kwa pamoja maana zilizo wazi na zilizofichikana ndani ya maandiko.” Baadyae,
Kutoka kwenye maandiko ya al-Imaam ash-Shaafi’iy, tunatambua vyanzo vya Maarifa ya Sheria za Kiislamu yalivyokubaliwa, na vile ambavyo vilisababisha kutokubaliana kwa wakati huo.
Vyanzo ambavyo vilikubaliwa vilikuwa ni: Kwa ujumla ni Qur-aan na Sunnah.
Vyanzo ambavyo vilihusiana na kutokubaliana vinajumuisha Sunnah yote kwa pamoja, na baadhi ya mapokezi Khabar al-Waahid (ambayo al-Imaam ash-Shaafi’iy ameitaja kama ni al-Khaaswah) mahsusi. Lakini mchango wa al-Imaam ash-Shaafi’iy ulikuwa kwamba, alichunguza masuala haya mawili kwa pamoja ndani ya ar-Risaalah na ndani ya Jima’ al-‘Ilm.
Masuala mengine ambayo yalihusiana na kutokubaliana yalikuwa ni:-
1. Al-Ijmaa’: Kulikuwepo kutokubaliana kuhusiana na uhalali wa matumizi yake
2. Al-Qiyaas na al-Istihsaan: Kulikuwa na mgogoro kuhusiana na maana ya tafsiri hizo, asili yake, uhalali wa matumizi yake kama ni sheria, uwezekano na utaratibu wa kuzitumia, na ama vitendo vya Maswahaba vinaweza kutambulika kama ni Qiyaas au Istihsaan.
3. Pia kulikuwa na kutokubaliana kulikokuwa bayana kuhusiana na uhalisi wa amri za Qur-aan na uzuiaji, maana zake na athari zake kwenye kanuni nyengine, hukumu za Fiqh. Tunaweza kutambua kwamba katika kipindi hichi, Maimamu Wanne wa Sunni hawakutumia maana ya maneno yaliyojifunga kama vile Tahriym “uzuiaji”, al-Ijaab “uwajibu”, n.k. Kwani maneno haya hayakutumika kwenye misamiati yao. Isipokuwa aina hii ya maneno ya kisheria yalijitokeza baadaye,
4. Vyanzo vyengine vya Maarifa ya Sheria za Kiislamu ambavyo vina tofauti, (ilikuwa) ni mara chache kujadiliwa kwenye kipindi cha wanazuoni wa mwanzo. Kwa mfano, kama maneno ya al-‘Urf, al-‘Aadah na al-Istis-haab yalikuwa sio sehemu ya misamiati yao.
[53] Ndani ya utangulizi wa tafsiri ya ar-Risaalah, Profesa Maajid Khadduuri anajadili maana ya al-Bayaan, na kunukuu tafsiri zilizotolewa na wanazuoni wa kuheshimika. Profesa Khadduuri ameandika:-
“Wengine wanasema, ina maana tu ya uteremsho unaojumuisha vifungu vya kisheria: Wengine wanajadili kwamba sio tu ni uteremsho, lakini pia kuwaweka wazi. Ash-Shaafi’iy, hata hivyo, anaonekana kutilia mkazo maudhui ya kisheria ya vifungu kwa hoja za kwamba mawasiliano yote ya Qur-aan yapo wazi, ‘ingawa baadhi yake yapo kwa ukali kuliko mengine’ na kwa wale tu wasiojua lugha ya Kiarabu yanakuwa baadhi ya mawasiliano yanaonekana kuwa hayapo wazi kuliko mengine.”
Kiuhakika, neno al-Bayaan linatafsiriwa na Profesa Khadduuri kama “uteremsho ulio bayana”. Angalia, Khadduuri, Islamic Jurisprudence (Maarifa ya Sheria za Kiislamu), Iliyochapishwa na Johns Hopkins Press,
[54] Ibn Qayyim, I’laam al-Muwaqqiy’in, I, uk.32.
Links
[1] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F2113&title=19-Uswuul%20Al-Fiqhi%3A%20Taratibu%20Za%20Imaam%20Ash-Shaafi%27iy%20Kwenye%20Kitabu%20Chake%20%27Ar-Risaalah%27